Siku saba za kamati kuu mpya ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku saba za kamati kuu mpya ya CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Apr 17, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Nimekuwa nikifuatilia mwelekeo wa hii kamati kuu mpya ya CCM tangu iingie madarakani, kwa sasa ina muda kama wa siku saba hivi, na kwa upande wangu nimeona yafuatayo.

  1. Uropokaji na kuongea bila kufikiria madhara yake ni kukubwa mno, hawana tofauti na akina Makamba na Tambwe, ukifuatilia kauli za Nape Nnauye na Katibu wake wakiwa Dom, Manzese DSM, Chalinze, Kibaha nk.
  2. Hawajui wanapambana na nani, na kama wanajua wanatupumbaza watanzania, kwa hiyo wanatapatapa kila kona bila mwelekeo.
  3. Bado ni waoga, wanachama mafisadi wanawajua, badala ya kuwachukulia hatua wanaropokaropoka kwa umma. Sasa tuwaelewe je?
  Kwa mwanzo huu nadhani wanatuonyesha kuwa gamba bado lipo, linahitaji kulowekwa kwa muda mrefu kabla ya kuvuliwa.
   
 2. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Si walisema CCM haina Mafisadi?? Hata wakiwepo mafisadi si wezi wa mali ya umma ni wezi wa wake za watu!!
  Shule ya Dr Slaa ni ya uhakika na somo limewaingia CCM ipasavyo wanatamani kutoana LOHO.
   
 3. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,902
  Likes Received: 12,042
  Trophy Points: 280
  Hivi wewe bado unachukulia serious mambo ya CCM pole hata hizo siku 90 walizosema zitakwisha wataongeza zingine zitakwisha and business continue as usual, ni usanii kwa kwenda mbele.

  Hao unaowasikia sasa sijui Nnauye na Mukama wamewekwa pale kwa maslahi ya kikundi fulani si kwa maslahi ya wanaCCM. Na kosa kubwa wanalolifanya ni kuendelea kufanya yale yale yaliyokuwa yanafanywa na Makamba kukipaka rangi chama kwa nje ilhali mioyoni hali ni ile ile.

  Mfano wa juzi kusomba wanafunzi wa Central na kuonyesha wamegawa kadi wakati wanafunzi wenyewe mioyo yao haipo kwenye chama, ni yale yale tuliyoyazoea. Nnauye akitoka hapo atakuwa anajidanganya kuwa chama kinapendwa which is not, i think they are repeating same mistakes Makamba was doing.
   
 4. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,152
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  wewe WAACHE WAENDELEE KUCHEZA KIDUK√ô MAJUKWAANI,wanafurahia mapinduzi ndani ya machakachuzi sasa tumepata jumuia nyingine ndani ya CCM.
  UMOJA WA WATOTO WA MAKATIBU WA CCM (nape moses nauye,january yusuph makamba).jipya hakuna zaidi ni minyukano zaidi ndani ya ccm.
   
 5. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu, ni vema ukaelewa ni nini kinachoendelea; mkakati uliowekwa na CCM unalenga katika kuwahadaa wananchi watenganishe makosa yanayofanywa na viongozi binafsi wa chama hicho na chama chenyewe. Na hivyo katika hizi siku saba waheshimiwa hao wamekuwa wakijaribu kujenga hoja ya kuwa CCm kama chama kinachukia ufisadi na kimepania kufanya kila kiwezalo kuwatosa wanachama wake wote wenye harufu ya ufisadi. Kutokana na mtandao mkubwa wa chama hicho, kinayo matawi zaidi ya 2300, pamoja na uelewa mdogo wa wananchi, mkakati wao huo uenda ukafanikiwa- angalau kupunguza kasi ya kuporomoka umaarufu wake. Hivyo CHADEMA haina budi kujipanga upya. Kuna haja kubwa kwa chama hicho kufikiria sana ili suala la kuanzisha matawi ya chama hicho angalau katika baadhi ya mikoa muimu yenye idadi kubwa ya wananchi.
   
 6. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ndiomaana ukaambiwa CCM inabomoka chama kinakwisha mchwa unakitafuna ujue hapo hili kundi la mafisadi nalo litaanza kukitafuna chama wewe unadhani wamefurahia walivyoondolewa madarakani na chamani pia wanavyotangazwa vibaya!!!CCM makundi hayatoisha labda kusiwepo na upinzani na ni kitu ambacho hakiwezekani tujiandae kuendelea kusherekea makundi yanavyomeguka chamani!
   
Loading...