EvilSpirit
JF-Expert Member
- Jun 15, 2017
- 13,664
- 21,584
Kwa siku takribani 2 nilikuwa kifungoni baada kupewa ban.Ban uisikiage tu kwetu tulio wahi kuipata.Kwa siku hizi mbili nimeteseka sana,kitu ambacho huwa kinafanya ninunue bando ni Jamii forums sasa safari hii baada ya kununua bando na kutaka kuingia JF nikakuta kuna mbinyo.Kuepuka bando langu kuisha bila sababu za msingi ikanibidi niangalie pilau kwa siku zote mbili,na kujiongezea mazambi.Hakika nimejifunza jambo.Shukrani zangu za kipekee zimueedee bwana PAW kwa kutoa adhabu stahiki .Kuanzia sasa nahaidi kuwa mwanajamvi mwenye kufuata kanuni na taratibu,pia nawaasa wanajamvi wengine wasiofuata kanuni na taratibu kuwa watashughulikiwa kikamilifu.Imagine ban tu ya siku 2 ni kima miaka mwaka,sasa inakuaje ukipewa mbinyo wa mwenzi mmoja.Nawasilisha