Kuanzia tarehe 16 hadi 25 Oktoba 2015 ziwe ni siku kwa wanaomsapoti Edward Lowassa kuwa Rais kuhakikisha wanamsaidia kufikia ndoto yao hiyo ambayo pia ni ndoto yake. Ni lazima wenyewe wahakikishe kuwa wamemuombea kura kwa watu wote wanaohusiana nao mpaka kufikia kizio (Limit) chao cha juu kabisa.
Kama kuna mtu ulisoma naye, jirani yako, ndugu zako, waumini wenzako, wafanyakazi wenzako,mashabiki wenzako na watu wengine wote unaowafahamu hata kama hauna mahusiano nao ya moja kwa moja, hakikisha kuwa wote waliojiandikisha katika kundi hilo wanakwenda kupiga kura na wanampigia Lowassa.
Jambo lingine ni lazima watu wajue kuwa siku ya kupiga kura ni mhuhimu kuhimizana kwenda kupiga mapema kwani wengine wanasubiria mida ya kuanzia saa 9 kwenda kupiga kura wakati kama wakati huo yakitokezwa matatizo ya kiufundi hakutakuwa na uwezekano wa kupiga kura.
Kufuatilia mikutano ya Kampeni ni jambo zuri lakini siyo muhimu kama vile kutafuta kura za Mgombea wako. Wengine badala ya kutafuta kura za wenza wao wameishia kuwatishia au kuwaacha na "Ubozi" wao, Jambo ambalo ni kosa kubwa sana kulifanya. Kura ya "House Boy au Girl" kura ya kuli, kura ya teja, kura ya mswalihina au Mlokole, kura ya Profesa au Kura ya aliyeiishia darasa la Kwanza hizo zote zina thamani sawa wakati wa kuhesabiwa, hivyo ni muhimu kuiipata kura ya kila mtu.
Mtu baki akiomba kura kwa ndugu yako ni tofauti na wewe ukiomba kura hiyo. Badala ya kuwashutumu watu wasiotaka kumchagua Lowassa kutokana na "Ugonjwa" au "Ufisadi" hakuna haja ya kubishana nao badala yake waelimishwe waelewe kuwa hizo ni Propaganda za kisiasa na wala hazina uhalisia wowote ule!
UMESHAONGEA NA HOME LOWASSA AWE RAIS?