Siku kumi muhimu kwa ushindi wa Lowassa

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,032
33,512
Kuanzia tarehe 16 hadi 25 Oktoba 2015 ziwe ni siku kwa wanaomsapoti Edward Lowassa kuwa Rais kuhakikisha wanamsaidia kufikia ndoto yao hiyo ambayo pia ni ndoto yake. Ni lazima wenyewe wahakikishe kuwa wamemuombea kura kwa watu wote wanaohusiana nao mpaka kufikia kizio (Limit) chao cha juu kabisa.

Kama kuna mtu ulisoma naye, jirani yako, ndugu zako, waumini wenzako, wafanyakazi wenzako,mashabiki wenzako na watu wengine wote unaowafahamu hata kama hauna mahusiano nao ya moja kwa moja, hakikisha kuwa wote waliojiandikisha katika kundi hilo wanakwenda kupiga kura na wanampigia Lowassa.

Jambo lingine ni lazima watu wajue kuwa siku ya kupiga kura ni mhuhimu kuhimizana kwenda kupiga mapema kwani wengine wanasubiria mida ya kuanzia saa 9 kwenda kupiga kura wakati kama wakati huo yakitokezwa matatizo ya kiufundi hakutakuwa na uwezekano wa kupiga kura.

Kufuatilia mikutano ya Kampeni ni jambo zuri lakini siyo muhimu kama vile kutafuta kura za Mgombea wako. Wengine badala ya kutafuta kura za wenza wao wameishia kuwatishia au kuwaacha na "Ubozi" wao, Jambo ambalo ni kosa kubwa sana kulifanya. Kura ya "House Boy au Girl" kura ya kuli, kura ya teja, kura ya mswalihina au Mlokole, kura ya Profesa au Kura ya aliyeiishia darasa la Kwanza hizo zote zina thamani sawa wakati wa kuhesabiwa, hivyo ni muhimu kuiipata kura ya kila mtu.

Mtu baki akiomba kura kwa ndugu yako ni tofauti na wewe ukiomba kura hiyo. Badala ya kuwashutumu watu wasiotaka kumchagua Lowassa kutokana na "Ugonjwa" au "Ufisadi" hakuna haja ya kubishana nao badala yake waelimishwe waelewe kuwa hizo ni Propaganda za kisiasa na wala hazina uhalisia wowote ule!

UMESHAONGEA NA HOME LOWASSA AWE RAIS?
 
Ushindi muhimu ni kuing'oa CCM hivyo kura zisiishie kwa Lowassa tu bali ngazi zote kuanzia diwani, mbunge na hata rais...
 
Mimi ninatoa mpaka na elimu ya wapiga kura kwamba kwa mgombea urais wampigie mgombea wa chadema anayeitwa Edward Lowassa na kwa ubunge na madiwani wawapigie wagombea wa ukawa kutoka vyama vya chadema, cuf, nccr mageuzi na nld.
 
Mkuu ni vizuri kukumbushana hata hivyo mie tayari nishajihakikishia mtandao mpana takribani raia 500 nilio karibu nao.
 
Morogoro jimbo la kusini mashariki nimeambiwa huko watu hawajui kitu inayoitwa mabadiliko yani hadi imeniuma, kuna jamaa yangu yupo huko anampigia campaign mgombea wa CCM jimbo hilo, anasema kule wana vijiji ukiwapa T-shirt za CCM wanakuona wewe ni mungu mtu, hivyo kwa tafiti yake anasema CCM bado wana mtaji wa kura nyingi sana mkoa wa Morogoro hususa maeneo ya ndani ndani huko
 
mkuu huko ndo kule ambako mtoto wa marehemu celina kombani amerithi jimbo ili agombee ubunge. kama ukawa wangeongeza vikosi vya ardhini moro ilibidi ungekuwa mkoa wa kimkakati wa kikampeni...
 
Wajasiliamali wenzangu,wasomi wenzangu,maclassmate ,ndugu, jamaa na marafiki zangu kura ni kwa Lowassa! ondoa shaka!
 
Morogoro jimbo la kusini mashariki nimeambiwa huko watu hawajui kitu inayoitwa mabadiliko yani hadi imeniuma, kuna jamaa yangu yupo huko anampigia campaign mgombea wa CCM jimbo hilo, anasema kule wana vijiji ukiwapa T-shirt za CCM wanakuona wewe ni mungu mtu, hivyo kwa tafiti yake anasema CCM bado wana mtaji wa kura nyingi sana mkoa wa Morogoro hususa maeneo ya ndani ndani huko

Sahihi kabisa,
Moro bado ni ngome imara ya ccm.
 
Mimi kila nikikaa na mtu iwe kwenye kibasi iwe wapi namuuliza kwanza yy team nani ,km upande wa pili najaribu kumwelewesha kama tunatakiwa tupate mabadiliko kwa sbabu hii na hii,nashukuru tunakuwa tunaelewana na ntafanya hvyo hadi cku ya mwsho
 
hujakutana na vichwa maji kama akina simiyu , unaweza kuhama wewe baada ya kumhamishia yeye upande wa mabadiliko
 
Morogoro jimbo la kusini mashariki nimeambiwa huko watu hawajui kitu inayoitwa mabadiliko yani hadi imeniuma, kuna jamaa yangu yupo huko anampigia campaign mgombea wa CCM jimbo hilo, anasema kule wana vijiji ukiwapa T-shirt za CCM wanakuona wewe ni mungu mtu, hivyo kwa tafiti yake anasema CCM bado wana mtaji wa kura nyingi sana mkoa wa Morogoro hususa maeneo ya ndani ndani huko

Acha uongo wewe Morogoro kusini mashariki ipi unayoisema?

Kuanzia Kisaki...Duthumi...Mgazi...Kongwa...Dakawa....Mirengwerengwe...Kolelo...Matombo kote huko nilipita watu wanataja UKAWA kwa wingi sana wewe unataka potosha umma!!

Upepo wa mabadiliko upo nchi nzima.
 
hahahahaha aha wapi bana najitahid kadri ya uwezo wangu kukata tamaa/au kushindwa ni vibaya sana,wapo wengine hadi wanakutukana ila sikati tamaa
 
Morogoro jimbo la kusini mashariki nimeambiwa huko watu hawajui kitu inayoitwa mabadiliko yani hadi imeniuma, kuna jamaa yangu yupo huko anampigia campaign mgombea wa CCM jimbo hilo, anasema kule wana vijiji ukiwapa T-shirt za CCM wanakuona wewe ni mungu mtu, hivyo kwa tafiti yake anasema CCM bado wana mtaji wa kura nyingi sana mkoa wa Morogoro hususa maeneo ya ndani ndani huko
Ulitegemea jamaa yako anayempigia kampeni ccm aongee tofauti na haya..
 
Back
Top Bottom