Siku kikiingia chama kingine madarakani, CCM mtasemaje kuhusu sheria hizi za habari na cybercrime?

  • Thread starter OKW BOBAN SUNZU
  • Start date

OKW BOBAN SUNZU

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2011
Messages
25,922
Likes
25,928
Points
280
OKW BOBAN SUNZU

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2011
25,922 25,928 280
Huwa nikikifikiria sana Chama cha Mapinduzi na kuona kimejaa unafiki wa hali ya juu sana. Hakina aibu kabisa wala soni.Leo hii mwenyekiti wake anatamba kwa kuorodhesha orodha ndeeeefu ya matatizo ya kupiga dili kana kwamba nchi ilikuwa ikijiongoza yenyewe

Hakuna ubishi kwamba chama kilibariki haya,na waziri wake akiwemo na mwenyekiti wa sasa wakiyatazama tu kama video. Kuna ufisadi wowote nchi hii unakosa wanasiasa?Kuna uamuzi wowote mbaya unakosa wanasiasa?Umeona mwanasiasa yeyoye anafuatwa fuatwa?

Sasa kibao kimewageuka eti nao wanasikitika sana kwa mambo yaliyokuwa yakiendelea!!!

Hii ni sasa na kutumia upande wa taulo kujifutia makalio halafu kesho utatumia upande huohuo kujifutia usoni.

Kosa hilohilo wanalifanya kwa kutunga sheria za ajabu ajabu. Hivi kesho kikiingia chama kingine madarakani,mtasemaje kuhusu sheria za habari na cybercrime? Mtawapa sera gani kama chama pinzani wanafunzi wa elimu ya juu na wasaka ajira ikiwa Leo hii mmesaini sheria ya kuwakata 15% wanufaika wa bodi ya mikopo?
 

Forum statistics

Threads 1,274,855
Members 490,833
Posts 30,526,000