SIKU ITAKAPOFIKA...................

Kalamu Yangu

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
1,093
1,027
SIKU ITAKAPOFIKA

Hiyo siku ikifika, nafsi kuuacha mwili,

Kalamu zitaandika,mara lile mara hili,

Wengi watahuzunika,na kushindwa kuhimili,

Siku itakapofika, mwili utapumzika.


Sijui ni kwa ajali, ama homa kunishika,

Wengi wanaonijali, kweli watahuzunika,

Na tuliotoana mbali, watabaki kukumbuka,

Siku itakapofika, mwili utapumzika.


Yale ninayoandika, yatawaaingia kweli,

Kalamu itadondoka, na kuipoza akili,

Ninani ataandika, mtajiuliza swali,

Siku itakapofika, mwili utapumzika.


Walojipa uadui, na kuziweka hila,

Watawazaje sijui, mie namwachia mola,

Nitakuwa sitambui, shimoni nimeshalala,

Siku itakapofika, mwili utapumzika.


Wale wa visa vya penzi, pesa pia roho mbaya,

Wataowaza ushenzi, na kunakili mabaya,

Wachongee kwa mwenyezi, nikome mwanaizaya,

Siku itakapofika, mwili utapumzika.


Itafika nende zangu, nikizitamani ndoto,

Nizeeke na mwanangu, na mapenzi motomoto,

Nisimuumize mamangu, baba kuzika mtoto,

Siku itakapofika, mwili utapumzika.


Nimuache Vaileti, Joshua na Khalfani,

Wabaki na vyangu vyeti, nikavidai njozini,

Niyaache magazeti, na vyote vya duniani,

Siku itakapofika, mwili utapumzika.


Nisisikilize nyimbo, mpya zitazoimbwa,

Wala nisihisi jambo, na vyote vilivyoumbwa,

Yaani ni mwisho wa mambo, kama gugu lilosombwa,

Siku itakapofika,mwili utapumzika.


Sala ya matumaini, siku moja tutaishi,

Na wengi tunatamani,ili na wote tuishi,

Tuirudishe amani, kwote kusifuke moshi,

Siku hiyo yetu sote, huja bila taarifa.




19748423_1556433647806813_1188673521698457323_n.jpg
 
Tupia zingine kama hizi ili tupate kukumbuka maana kila unaoingia yanayojadiriwa yanafanya tusahau huku

Sent from my Dell Laptop using Jamii Jorums mobile app
 
Back
Top Bottom