Siku hizi hata mke ukweni ni interview?

Siku hizi hata mke ukweni ni interview?

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2016
Posts
2,584
Reaction score
1,886
Salaam sana waungwana..

Last weekend nilipelekwa na mwenzangu ukweni kutambulishwa kua Mimi ndio Yule niliyesubiriwa kuvika pete chanda chema.

At first tuliongea Mimi na mwenzi wangu juu ya khali itakavyokua na nin lakin akaniambia kuna mengine hawezi sema sababu ni maswali yanayotokea papo Kwa hapo.

Ofcorse haikunipa tabu sana kabla ya kufika sababu nilijua nia yangu plus binti kanielewa nikawa sioni tatizo wala hofu.

nlipofika nilipokelewa vizuri,maongezi ya hapa na pale na mama mzaa chema huku nikisubiri mzee mwenye nyumba yani baba mkwe kwa mazungumzo zaidi as in kutambulishwa rasmi na nini.

Wakati nabuy sometimes kwa kusoma Jf huku nikipotezana mawazo na wadogo wa mwenzi wangu na mama mzazi kwa bahati nzuri yule mzee akafika.

Nilisimama tukasalimiana wazee wasomi ambao bado wanaitumikia serikali miaka ya lala salama wakingoja kipenga cha mwisho.

Kiukweli sikuwaza kama ningekutana na interview ngumu vile maana ilikua as if naomba nafas ya kazi au naomba mkopo Bank ya CRDB.

Ilikua kijana unaelimu? nikajibu, tena Ilikua anaandika sababu niliona amekuja na notepad, sijakaa sawa naulizwa occupation status ya wazazi wangu, namaliza kujibu hili napewa nyundo nyingine vipi how do you see your self after five years.
Kimoyo moyo nikawa naona nachefukwa. Ila ndio ukweni nikajikaza kiume tu.

Ilikua anaandakika kama mwanafunzi na lecturer kiukweli binafsi sikupenda, sema mke namtaka ikabidi niwe mpole najibu, sasa mwishoni mzee akauliza unafanya kazi gani, nilipo jibu akawa anahoji juu mambo yanayoendelea katika wizara yetu mwisho akatoa simu akapiga ofisi niliyopo na kuwasiliana na baazi ya seniors personnel,

sikujua Kama kapiga uko at first nakuja kugundua mwishoni niliposikia akisema aaah nna kijana wangu yupo hapo akataja jina langu uku akiniangalia na kutaja ofis niliyopo baada ya mazungumzo akakata simu nikaona amejawa na furaha kma mtu aliyefurahishwa na kitu.

Akanigeukia na kunikaribisha rasmi nikabaki nikiitika huku nikivunga kana kwamba niko saw a..ila nilishangaa sana..

Wakuu tujipange tusikurupuke `hii maisha mazuri mindset wanatoka nazo kwa babu na bibi zao hivi hivi utakula KO UKWENI
 
Vijana wamekuwa wadanganyifu sana siku hizi.

Naona wazazi nao wamekuwa makini sana kuhakikisha hawawakabidhi mabinti zao kwenye mikono isiyo salama.

Ila ni jambo zuri pia.
Hawa wazushi ndio ovyo kabisa wana aribu sana
 
...sasa mwishoni mzee akauliza unafanya kazi gani, nilipo jibu akawa anahoji juu mambo yanayoendelea katika wizara yetu mwisho akatoa simu akapiga ofisi niliyopo na kuwasiliana na baazi ya seniors personnel,

Bila shaka namba ya ofisini kwako ulimpatia, au? Hakukuuliza kama wewe pia ni mdaiwa sugu wa HESLB?
 
ha ha ha siku hizi wababaishaji wako wengi inaonekana mkwe alizisikia sifa toka kwa mwanae muda tu ndio maaana akajiandaa na uhakiki.....ila mkwe anakuuliza ""how do you see your self after five years"" hii inamana anamfananisha mwanae na kiwanda au ni uelewa wangu mdogo.....
Ndo nilichoka hapo
 
ha ha ha siku hizi wababaishaji wako wengi inaonekana mkwe alizisikia sifa toka kwa mwanae muda tu ndio maaana akajiandaa na uhakiki.....ila mkwe anakuuliza ""how do you see your self after five years"" hii inamana anamfananisha mwanae na kiwanda au ni uelewa wangu mdogo.....
hayo ndio mambo ya siku hizi wakati wa 4G usikurupuke kuoa kabla hujajipanga wala huna future utaumbuka.....anauliza hivyo ili ajue wewe ni mtu wa aina gani
 
Back
Top Bottom