Hata aliyeanzisha fb hakupiga domo kuwa nataka nianzishe app ya marafiki, vipi mtaipenda? Mtajiunga wadau? Itakuwa hivi, vile na vile. Hapana.
Nafikiri kama wewe si staff wa jamii forum, basi nenda uwaone, kwakuwa lengo ni kutumia platform yao katika kupata members. Au vinginevyo anzisha saccos yako uje ututangazie hapa.
Kama ukienda kuwaona, mkaianzisha, kisha mkaja na taarifa kuwa uongozi wa jamii media pamoja na wadau wake, unawatangazia kuanzishwa kwa jamii saccos yenye malengo hayaaaa, sifa za mwanachama ni hiziiiii, kiingilio ni hikiiiii, mgao utakuwa calculated hiviiiiii. Hiyo ni rahisi zaidi, kwasababu jamii forum ni platform ambayo imeshajijengea imani katika jamii, hatuamini kama wanaweza zima hii platform kwa ajili ya 1Bilioni na kutembea, haiwezekani.
Ni wazo zuri, ila itapendeza kama likafanyiwa kazi na taasisi na sio individual.