Siku 90 za CCM kuvunjika Vipande vpande. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku 90 za CCM kuvunjika Vipande vpande.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STEIN, Apr 18, 2011.

 1. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ina semekana kuwa Lowasa, Rostam na Chenge wana asilimia 60 ya mawaziri, asilimia 70 ya wabunge wa CCM, asilimia 50 ya wakuu wa mikoa, 50 ya makatibu waku, 60 ya majaji, asilimia kubwa ya watu wakubwa kule uwt, na vyombo nyeti.

  Na hali inavyooneka ni kwamba tukose wote na si wao tu. hii kwa tafsiri rahisi ni kwamba huu ni mwisho wa CCM na ni kutokana na weakness ya JK, maana JK kawadanganya wananchi akidhani mafisadi watamsaidia sasa gafla hana wananchi na mafisadi wameanza kumwandama. Uwongo wa kwanza wa JK ni pale aliposema hajui wamiliki wa Dowans kumbe ya RA na wananchi wanajua ni ya RA.

  Hii inaashiria mwisho wa CCM na kutokana na JK kupuuza wananchi huku akineemesha mafisadi
   
 2. U

  Uswe JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  sasa si ndio furaha yetu, mwache tu aharibu ili hata wale slow learners (wale walompa kura) wapate nafasi ya kumuelewa rais wao
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,840
  Trophy Points: 280
  Dk Slaa ampa JK siku 90 kudhihirisha gamba jipya Send to a friend Sunday, 17 April 2011 21:06

  Godfrey Nyang'oro, Urambo
  KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amemtaka Rais Jakaya Kikwete awataje watuhumiwa wa ufisadi na kisha kuwavua nyadhifa zao zote na kisha kuwafikisha mahakamani katika muda wa siku 90 kama kweli anataka kukivua gamba chama hicho.

  Kauli hiyo ya Chadema kwa Rais Kikwete imekuja siku chache baada ya CCM kuchukua hatua katika kile ilichokiita kujivua magamba kwa kuwataka watuhumiwa wote wanaotajwa kuhusika katika kashfa kadhaa za ufisadi, kujiondoa wenyewe katika nafasi zao ndani ya chama hicho katika kipindi cha miezi mitatu vinginevyo watawajibishwa.
  Jana, akiwa kwenye Uwanja wa Kaliua, Urambo Magharibi, Dk Slaa alisema kama kweli Rais Kikwete amedhamiria kukivua gamba chama chake, anapaswa kuuthibitishia umma kwa kufanya hivyo vinginevyo itakuwa ni ‘usanii.’
  Kwa mujibu wa Dk Slaa, endapo watuhumiwa hao watatajwa na kuchukuliwa hatua ikiwamo kuvuliwa nafasi zao na uanachama na kupoteza ubunge au kufukuzwa serikalini, dhana hiyo ya kujivua gamba itakuwa na mantiki.
  Dk Slaa alisema, Watanzania wanataka kuona fedha zao zilizoibwa na mafisadi zinarejeshwa na watuhumiwa kufikishwa mahakamani, hivyo haitoshi kusema neno kujivua gamba.
  Mwanachama mwingine maarufu wa Chadema, Frederick Mpendazoe ambaye aligombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho, Jimbo la Segerea katika Uchaguzi Mkuu uliopita, alisema endapo CCM kitashughulikia watuhumiwa hao wa ufisadi ndani ya siku 90 ni dhahiri kutafanyika uchaguzi kutokana na kile alichodai kwamba ni kuwa na wabunge wengi waliingia madarakani kwa njia ya rushwa.
  Alidai kwamba CCM imepoteza mwelekeo kutokana na kuhodhiwa na watu wenye malengo ya kibiashara ambao huchochea ufisadi unaokigharimu sasa.
  Mpendazoe ambaye aliwahi kuwa kada wa chama hicho tawala alisema miaka ya nyuma wakati wa Mwalimu Julius Nyerere, CCM kilikuwa madhubuti kutokana na kuwa na viongozi waliokuwa tayari kupambana na rushwa na ukosefu wa maadili ya uongozi, hali ambayo ni tofauti kwa sasa.
  Mpendazoe ambaye alijiondoa CCM kutokana na kile alichodai kuwa ni fitina za mafisadi alisema uongozi ndani ya chama hicho tawala kwa sasa ni uwekezaji akisema asiye na fedha ni vigumu kupata uongozi.
  Alisema kutokana hali hiyo, hata ile misingi ya waasisi iliyojengwa katika miaka ya 1960 na 1970 imebomolewa na mafisadi kushika hatamu za uongozi wa chama hicho tawala.
  Mpendazoe alisema Serikali iliyopo ni ya kidemokrasia lakini imekuwa ikiyapa kisogo matatizo ya wananchi wa tabaka la chini na kukumbatia wafanyabiashara ambao wana nguvu ndani ya chama hicho.
  Kuhusu muswada wa Sheria ya Marejeo ya Katiba, alisema hadi sasa serikali imeuondoa muswada huo bila kuweka mambo wazi na kuonya kama ukirejea kama ulivyo na tume ikiundwa na rais chama hicho kitaandamana.


   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,840
  Trophy Points: 280
  Comments
  +1 #9 mkilima 2011-04-18 07:55 SISIEM ilishaoza kuanzia kwenye matawi,watanzan ia wa sasa sio wale miaka ya 80,redio moja kijiji kizima unasikiliza maoni ya mtu mmoja, vingozi tulio nao sasa hakuna asiye fisadi,kama yupo na aseme hadharani kwa kupitia vitabu vya dini waliyoapa na waonyesha hadharani mali walizonazo na walizomiliksha watoto wao, CCM imeharibu kila kitu na kutubwaga watanzania bwaaa,na umasikini uliokisiri,tuna kula mlo mmoja harafu tunadanganywa uchumi unakua, huo uchumi unakua matumboni mwao.Wapinzani shikamaneni tupo pamoja nanyi mwisho wa SISIEM ndio huu.
  Quote


  0 #8 kahangwa 2011-04-18 06:54 Quoting Massawe:
  chadema mmezidi kuropoka. Tumieni muda huu kujenga chama. chadema bado kichanga sana acheni porojo/
  Massawe unamtofautishaj e mchanga na mtu mzima kama mtu mzima anafanya madudu? Kumbuka mwanafunzi wa darasa la sita anapimwa kwa mtihani wa darasa la sita na siyo wa form six.Ninawashangaa mnaowataka kuilinganisha ccm na chama kingine cha siasa kwani kumbuka tangu enzi za tanu chama kilikuwa kimoja na kilijengwa na watanzania wote,kumbuka hata kujiunga chuo ilibidi uwe na kadi ya umoja wa vijana,tuvipime vyama vya upinzani kwa umri wake kwani vinajengwa na wachache na siyo nchi nzima kisha kuporwa na wachache na kujisifia kwa mafanikio yaliyoletwa na wale waliokuwa na nia ya kuijenga nchi enzi za siasa ya ujamaa na kujitegemea.
  Quote


  +3 #7 genekai 2011-04-18 06:52 Hawa ccm hawana nia thabiti ya kujivua magamba manake mfumo mzima wa ccm ni ufusadi mtupu, itakuwani sawa na kujitoa damu yote halafu uendelee kuishi!
  Quote


  -2 #6 smartboy 2011-04-18 06:46 Tuliambiwa kuwa Dr Slaa atatoa orodha ya Mafisadi huko Tabora, mbona hajatoa? Au naye ni msanii tu wa siasa.

  Ufisadi hauko CCM tu hata huko Chadema umejaa tele. Akina Mpendazoe si dhani km leo wanajiita wasdafi baada ya kuondoka CCM. Ni kuwa wamezidiwa ujanja na mafisadi wenziwe ndo maana wamekimbilia upinzani.


  Kumtaja mtu tu kuwa fisadi pasina ushahidi haitoshi na itakuwa ni kiroja kuwa kila mtu akisimama na kusema fulani ni fisadi basi, afukuzwe kazi, afungwe pasina kuthibitika dhahiri shahiri kuwa ni fisadi. Ikiwa itakuwa hivyo, basi hii serikali itakuwa ni ya kidikteta. Mbona hatujawahi kusikia fisadi kafungwa enzi za huyo mnayemfagialia (Nyerere), ina maana hapakuwa na ufisadi? Mbona Nyerere kaiacha nchi imkufa, mashirika ya Umma yote yamefulisika wakati wake. mbona hakuwakamata na kuwafunga walioifilisi nchi???

  Quote


  +2 #5 kushake 2011-04-18 06:15 Masawe pole. Kujenga chama ni pamoja na hizi agenda za ufsadi ambazo akina mafisadi wanajengea mahekau majuu
  Quote


  +2 #4 Jabir 2011-04-18 05:42 Kama IPTL inamhsu mzee wa kaya nae pia ni fisadiiii.ajivue gamba,vinginevy o ni usanii mtupu
  Quote


  -5 #3 Massawe 2011-04-18 05:08 chadema mmezidi kuropoka. Tumieni muda huu kujenga chama. chadema bado kichanga sana acheni porojo/
  Quote


  +4 #2 LENGAI 2011-04-18 04:22 CCM KWISHNEY!!!!. KAMA UNAMJUA MTU MWIZI UNAMPA SIKU TISINI ZA NINI NA WEWE NI MKUBWA WA NCHI. MAFISADI WOTE MUMESHATAJIWA NA CHADEMA HOJA ZA SIKU TISINI ZINATOKA WAPI?. WATANZANIA SASA TUNAMPA JK SIKU TISINI ATAIFISHE MALI ZA MAFISADI NA KUWAFUNGA VINGINEVYO TUNAINGIA IKULU KWA MAANDAMANO TUKUTOE.TANZANIA NI YA WATANZANIA SIO YA UKOO WAKO WALA MARAFIKI ZAKO.
  Quote


  +5 #1 Bakari 2011-04-18 03:35 Hizi ndio propaganda za ukweli na uwazi... CCM walitaka kudanganya waTZ kuwa ina MAFISADI WATATU TU!!

  Kujivua gamba ndio mwanzo wa mwisho wa CCM maana kimekubali wazi kwamba kina UFISADI na wala hawawezi kuuvua! CCM Kwisha!!

  Quote
  Refresh comments list
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,840
  Trophy Points: 280
  Slaa anatumiwa-CCM

  Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Zanzibar; Tarehe: 18th April 2011 @ 07:40 Imesomwa na watu: 198; Jumla ya maoni: 0

  CHAMA Cha Mapinduzi kimesema Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa na chama chake, wanatumiwa na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi waliotakiwa kujiuzulu wenyewe ndani ya chama hicho.


  Akihutubia umati wa watu katika viwanja vya Mwembe-Kisonge Zanzibar, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema kwa sasa watuhumiwa hao wameamua kutumia baadhi ya vyama vya siasa, magazeti na asasi za dini kujibu mapigo.


  "Tumewapa miezi mitatu watuhumiwa wote wa ufisadi katika chama chetu wajiondoe wenyewe. Baadhi wanajaribu kupinga na kujibu mapigo kwa kutumia magazeti, vyama vya siasa na taasisi za dini...tunajua tutashinda na wao lazima waondoke," alisema Nnauye.


  Alisema, "Tumeandaa mkakati wa kusafisha chama kutoka ngazi za chini mpaka katika ngazi ya Taifa. Tumechunguza na tunajua wanaotakiwa kuondoka ndani ya chama chetu. Lakini baadhi ya watu wamejitokeza kutaja majina ya watuhumiwa ndani ya chama chetu, hiyo si kazi yao."


  Aprili 16 Dk. Slaa akiwa mkoani Tabora, aliwatuhumu baadhi ya viongozi wastaafu wa CCM na waziri mmoja kuwa miongoni mwa aliowaita orodha mpya ya watuhumiwa wa ufisadi.


  Lakini Katibu huyo wa Chadema, alifanya hivyo siku chache baada ya CCM katika mkakati wake wa kujivua gamba, kuwataka watuhumiwa wa ufisadi ndani ya chama hicho kujiuzulu wenyewe ndani ya miezi mitatu ijayo kabla ya kuondolewa kwa nguvu na Halmashauri Kuu ya

  Chama hicho Taifa (NEC).

  Dk. Slaa alifanya hivyo akijua kuwa sekretarieti mpya ya CCM, ikiwa na viongozi wapya imeanza ziara kutambulisha uongozi mpya kwa wanachama wake na kuelezea uamuzi mgumu wa kujivua gamba walioufanya mkoani Dodoma.


  Naye Katibu wa Itikadi, Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa, January Makamba alisema wamejipanga kufanya mageuzi makubwa kwa ajili ya kukiendeleza chama hicho na Taifa na kuahidi kuwa mabadiliko hayo yatamfurahisha kila mmoja.


  Pia Naibu Katibu Mkuu, Tanzania Bara John Chiligati alisema mabadiliko yaliyofanyika hivi karibuni, yanalenga kuokoa chama hicho kutokana na hali ya kupoteza kukubalika kwake kwa jamii.


  Kwa upande wa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Vuai Ali Vuai aliwataka wanachama kujitolea kujenga chama hicho, ikiwa ni pamoja na kuacha migogoro ya makundi ndani ya chama hicho na kujenga umoja.


  Kabla ya viongozi hao kuzungumza na wapenzi wa chama hicho, Katibu Mkuu wa mpya wa CCM, Wilson Mukama aliwaambia wafuasi wa chama hicho kwamba Sekretarieti mpya

  imejitoa kuleta mabadiliko ndani ya chama hicho.

  Mapema kabla ya kuwatambulisha viongozi wapya katika mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa, alisema wamefanya mabadiliko katika kanuni za chama hicho, ili Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar awe Mjumbe wa NEC kutokana na nafasi yake badala ya Waziri Kiongozi ambaye nafasi hiyo kwa sasa haipo.


  Msekwa alieleza sababu zilizosukuma chama hicho kufanya mabadiliko hayo kwa lengo la kurudisha kukubalika kwake kwa wananchi na wanachama wake.


  "Huku ni kuzaliwa upya baada ya Februari 1977 wakati Tanu na ASP zilipoungana," alisema Msekwa.


  Akihutubia mamia ya wafuasi wa chama hicho na wananchi waliojitokeza kuwakaribisha viongozi hao, Msekwa alisema matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita yalikuwa ishara ya wazi kwamba chama kilianza kupoteza mvuto wake kwa wananachi.


  Alisema hali hiyo ilisababaisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuunda Kamati Maalumu ya watu sita ikiongozwa na Mukama ambaye aliwaaalika wataalamu (ambao si wanachama wa CCM) kutafuta mzizi wa tatizo hilo.


  Kamati hiyo kwa mujibu wa Msekwa, ilieleza kuwa CCM imebebeshwa mzigo wa kuwa na baadhi ya wanachama wake ambao wanatuhumiwa na wananchi kwa kuhusika katika rushwa.


  Alisema kutokana na mzigo huo, CCM ilichafuka kwa kuonekana chama cha walarushwa na mafisadi.
   
 6. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Umesahau: wana asilimia 80 ya UVCCM.
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,840
  Trophy Points: 280
  Nape: Orodha ya mafisadi ni mchezo wa kuigiza Send to a friend Sunday, 17 April 2011 21:08

  [​IMG]Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye

  Ramadhan Semtawa, Dar na Salma Said, Zanzibar
  SIKU moja baada ya Chadema kutangaza orodha mpya ya watu, kinachodai kuwa ni mafisadi ndani ya CCM, Katibu wa Uenezi na Itikadi wa chama hicho tawala, Nape Nnauye amesema orodha hiyo ni sawa na mchezo wa kuigiza.
  CCM katika vikao vyake vya Nec na Kamati Kuu vilivyofanyika Dodoma wiki iliyopita, kilifanya mageuzi makubwa ya uongozi na maazimio kadhaa yenye lengo la kuwaondoa wote wenye tuhuma nzito za ufisadi na ukosefu wa maadili katika kile inachokiita kujivua gamba. Lakini juzi, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alirusha kombora jingine akiongeza orodha ya watuhumiwa wa ufisadi ndani ya chama hicho.
  Akizungumza kabla na baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika jana mjini Zanzibar, Nape alisema; "Huo ni sawa na mchezo wa kuigiza. Hatua hiyo haina lolote katika mchakato wa kung'oa mafisadi ndani ya chama chetu tena nawaambia wanachofanya ni sawa na kuwasha moto juu ya petroli."
  "Bahati nzuri tumeshajua mipango yao yote ya kujaribu kuendesha kampeni ya kuchafua watu wasafi ndani ya chama akiwamo Rais na familia yake.""Tunajua wamepanga kutumia baadhi ya vyama

  vya siasa vya upinzani, viongozi wa dini, baadhi ya vyombo vya habari na waandishi. Kwa hiyo hata hiyo orodha mpya tunajua ni sehemu ya mchezo huo."

  Nape alisema mkakati huo wa kuwachafua makada wa CCM na Rais Kikwete hautafanikiwa akisema kila kitu kiko wazi."Ni mchezo wa kuchafua watu tu lakini nawaambia mkakati huo hautaweza kukigharimu chama wala kukifanya kiachane na mchakato wa kuwashughulikia mafisadi ndani ya CCM ," alisisitiza Nape.

  Mkutano wa hadhara
  Akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kisonge, Mjumbe huyo wa Nec ya CCM alisema, uamuzi uliochukuliwa na chama hicho wa kujivua gamba ni mgumu na ulihitaji ujasiri mkubwa.

  Alisema uamuzi huo ni sawa na mwenge ambao umewashwa Dodoma na kwamba utazunguka nchi nzima na kumulika maeneo yote ili kurejesha imani ya wananchi na wanaCCM ambao kwa muda mrefu wamekata tamaa na chama chao ambacho kinazuliwa mambo mengi machafu ikiwamo madai kuwa ni chama cha mafisadi na chama cha matajiri jambo ambalo halina ukweli.
  Aliwataka wanachama wa CCM Zanzibar, kurejesha matumaini kwa chama chao huku akisisitiza kwamba uamuzi wake wa kujisafisha, unawalenga wote wenye kukidhoofisha hivyo kuwataka wale wote wenye shutuma wajitose wenyewe kabla hawajatoswa kwani wakichelewa watatoswa kwa lazima ili boti iendelee na safari yake.
  "Tunawaambia kabla boti yetu haijaondoka wale wote wanaotuhumiwa ndani ya chama chetu tunataka watoke. Kama hawataki basi tutawatosa kabisa ili sisi tuendelee na safari," alisema Nape.
  Akifafanua sababu za kutoa miezi mitatu, kwa wale wote wanaotajwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kashfa mbalimbali za ufisadi zilizokitia doa chama hicho, Nape alisema lengo la uamuzi huo ni kuwapa nafasi ya kujitathmini wenyewe.
  Alitoa mfano wa hatua hiyo kwamba ni ; "Sawa na pweza unapotaka kumla lazima umpige na michanga hivyo miezi hiyo mitatu ni kujisafisha kabla ya kuliwa."
  Kwa upande wake, Katibu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Januari Makamba, amesema chama hicho hivi sasa kitaendeshwa kisiasa kwa lengo la kujiimarisha vyema kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.
  Alisema hivi sasa chama hicho kimepata wataalamu na wenye kufanya mipango kisomi zaidi kuliko kilivyokuwa mwanzo, hivyo hakuna sababu ya vijana kuvunjika moyo hasa kwa kuzingatia kuwa ndiyo waliopewa majukumu ya kukiendesha.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai alisema moja ya majukumu yake ni kukiunganisha na kukiimarisha chama hicho. Aliwataka wanachama wanaokwenda kwake kupeleka maneno yenye kukijenga na siyo fitina na majungu.
  Awali, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa alisema mabadiliko hayo yana lengo la kukirejesha chama katika mstari lakini akiwataka wananchi kuridhika na uamuzi huo mgumu ambao alisema hakuna chama kingine ambacho kinaweza kuiga mfano huo.
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,840
  Trophy Points: 280
  Comments
  0 #13 OSAMA 2011-04-18 08:07 CCM NI MA-STAGE SHOW WA CHADEMA,NA BADO.
  Quote

  +1 #12 mkilima 2011-04-18 08:03 Kelele za wapangaji za wanyima usingizi wenye nyumba, sasa hakulaliki, wapangaji jipeni moyo mtashinda tuu, hata yakivuliwa magamba na hata wachune ngozi mwisho wa huooooo, ufisadi kila kona na hata huyo Nape naye alikataliwa iweje sasa wlambe matapishi yao na kumrudisha? orodha iliyotajwa nikweli kama wanakataa wataje mali zao hadharani na pesa walizoweka huko ng'ambo.
  Quote

  +3 #11 Najaribu 2011-04-18 07:45 Nape, hata mwaka 2007 CCM ilisema mengi tu ya kuikosoa orodha ya mafisadi 11 waliotajwa na Dr. Slaa na wenzake. Kikwete mwenyewe alitumia msemo wa mipasho kuwa "kelele za mpangaji hazimnyimi usingizi mwenye nyumba" Wengine wakatishia kushtaki mahakamani.

  Leo hao mafisadi mnaoserma CCM inayo wametoka wapi? Baba yako Moses Nnauye alikuwa mwadilifu asiyelinda ufisadi. Sasa wewe umelewa madaraka mapema sana kiasi cha kuanza kuwalinda mafisadi akiwemo JK. Hailipi hiyo! Yusufu Makamba alifanya hivyo kwa nguvu zake zote, ameishia kulazimishwa kujiuzulu kwa kile kinachosemwa na CCM kushindwa kumsaidia JK.

  Utendaji kazi wa katibu huakisi utendaji kazi wa mwenyekiti wake. Sasa Nape usianze kwa mbwembwe nyingi, wenzako wanakushangaa tu unavyokubali vidole vyako kutumiwa kuchukulia kitu kwenye kaa la moto

  Quote

  +4 #10 genekai 2011-04-18 06:47 Sasa utanambia kuwa ccm wana nia thabiti kweli ya kuikomboa tanganyika kwa kujivua magamba? Waacheni wazidi kujimaliza na ufisadi wao!
  Quote

  +3 #9 kushake 2011-04-18 06:23 Kuna [NENO BAYA] wengi sana tz. Mwanasiasa akimtaja fisadi anayetakiwa kumpeleka mwenzake mahakamani ni mtajwa na siyo mtaja. Wewe Jegu ni mmoja wa mafisadi au ni familia yao. Otherwise usingesema shut up kwa Dr Slaa. Pole sana, mda wenu unayoyoma
  Quote

  +3 #8 Sam 2011-04-18 06:21 Nape unacheza makida wewe! Unatetea mafisadi kwa staili hiyo. Maneno ya CCM na vitendo vyenu tofauti kabisa.
  Hizo propoganda za ki ji nga zimepitwa na wakati. Nasema CCM yote chafuuuu, hakuna msafi hapo, hata wewe mwenyewe Nape hufai.
  Nyerere mwenyewe aliwahi kusema CCM imeoza!!!

  Quote

  -7 #7 jegu 2011-04-18 05:47 Bw Slaa, haya uliyoanzisha ni majungu.Unatuambia vitu ambavyo tunafahamu.Kama una solid proof,kwa nini usiwafungulie mashitaka?You are not a common man like me.If you can't do it,then shut up.You are not an angel,free from all these things.Sidhani kama unaweza kumfikia Mr Pombe kiutendaji wa kazi.Do your part in a gentleman way and we'll support you.
  Quote

  +7 #6 mtu kwao 2011-04-18 05:08 kikwete ni fisadi no.1 HILO HALINA UBISHI NA ccm inafia kwake sio muda tusubiri ,,watu wabishi kweli nyie.
  Quote

  +5 #5 LENGAI 2011-04-18 04:16 TATIZO LA VIONGOZI WA CCM NI KULINDANA.KAMA MTU KAITWA FISADI TUNATAKA AKANUSHE MWENYEWE NA SIO NAPE AMSAIDIE KUKANUSHA. CCM MMELEA WENYEWE UCHAFU NDANI YA CHAMA. KAMA MNAWAJUA MAFISADI MNASUBIRI NANI AWATAJIE AU KUWASHITAKI. TUNATAKA MAGEUZI YA KWELI TANZANIA NA KWA UCHAFU MLIO NAO LAZIMA MUONDOKE. TANZANIA WATU WAMEENDELEA SIKU HIZI NA KILA MTU AMESHAWAJUA CCM KUWA HAWAWEZI LETA MAENDELEO TENA. CHAMA KIMEKUWA CHA KUJALI MASILAHI BINAFSI NA KURUSHIANA MADONGO. TOKENI HAMTUFAI TENA KUONGOZA NCHI. INGEKUWA MNA NIA YA KUJISAFISHA MUNGEONYESHA KWA VITENDO NA SIO MANENO.
  Quote

  +4 #4 LENGAI 2011-04-18 04:15 TATIZO LA VIONGOZI WA CCM NI KULINDANA.KAMA MTU KAITWA FISA TUNATAKA AKANUSHE MWENYEWE NA SIO NAPE AMSAIDIE KUKANUSHA. CCM MMELEA WENYEWE UCHAFU NDANI YA CHAMA. KAMA MNAWAJUA MAFISADI MNASUBIRI NANI AWATAJIE AU KUWASHITAKI. TUNATAKA MAGEUZI YA KWELI TANZANIA NA KWA UCHAFU MLIO NAO LAZIMA MUONDOKE. TANZANIA WATU WAMEENDELEA SIKU HIZI NA KILA MTU AMESHAWAJUA CCM KUWA HAWAWEZI LETA MAENDELEO TENA. CHAMA KIMEKUWA CHA KUJALI MASILAHI BINAFSI NA KURUSHIANA MADONGO. TOKENI HAMTUFAI TENA KUONGOZA NCHI. INGEKUWA MNA NIA YA KUJISAFISHA MUNGEONYESHA KWA VITENDO NA SIO MANENO.
  Quote

  +7 #3 Bakari 2011-04-18 03:46 NAPE lazima mtaendelea kucheza mziki wa CHADEMA, mlitaka kuwadanganya waTZ kuwa CCM ina mafisadi WATATU pekee!!!

  Sababu ya kila FISADI aliyeongezwa imetanabahishwa . MAGUFULI arudishe nyumba za Serikali kama hataki rekodi chafu, uwezo huo ANAO!

  Quote

  +6 #2 kiroboto 2011-04-18 02:46 Mimi si mpenzi wa chama chochote ila nachukia mafisadi popote walipo. Hivi wewe Nape, napewa kweli umepewa. Huoni hapa tulipo? wewe ni kati ya ngiri wa mshipa na ngiri wa porini. Mimacho mikubwa na masikio lakini huoni wezi? yaani hata umeme huoni? huoni pesa zinavyochuja? huoni umasikini wa watu na wizi.
  Quote

  +8 #1 mbiligi 2011-04-18 02:15 Nape acha U J I N G A. Mh Jk ni mchafu wa tabia,Afya na ni Fisadi. Familia ya JK ilipata wapi pesa za kuzunguka nchi nzima kwa kampeni? (Maana kila mmoja alikuwa kivyake na kundi lake)
  CDM ni chama makini chenye hoja za nguvu na sahihi na ni changamoto tosha kwa serikali ya CCM.
  Nape ulikuwa makini lakini hako kacheo sasa katakuharibia heshima yako. Naomba fanyieni kazi orodha ya CDM na muisafisheni serikali ya CCM

  Quote  Refresh comments list
   
 9. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  furaha yeni nani mkuu?
   
 10. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Kazi kwelikweli... Mi naomba nionyeshwe mabaki ya hilo gamba nilitunze manake hata nyoka akijivua gamba huwa linabakia pale na yeye anahamia sehemu nyingine kwa usalama. Au hilo gamba ni Makamba??
   
 11. mkatofa

  mkatofa Member

  #11
  Apr 18, 2011
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umetoa chanzo kipi?
   
 12. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sisi WaTZ
   
 13. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Chanzo kimoja matendo ya UVCCM, waTZ wa Kawaida
   
 14. d

  demokrasia Member

  #14
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hawa jamaa (ccm) ni wasanii sana.inawezekana hawa wanaowaita mafisadi wanawapiga vita kisanii tu ili kuvuta "public attention" kwenye chama chao.ni usanii tu huo. mtajionea.
   
 15. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #15
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nadhani watahama chama na kuna chama kinachosifika kuwapokea wahanga wa kisiasa kutoka CCM sasa sijui watatumia sabuni gani kuwasafisha tungoje tuone....................
   
 16. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #16
  Apr 18, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,909
  Likes Received: 12,066
  Trophy Points: 280
  Can Rutashubanyuma STOP posting unnecessary many and long articles as you are distorting the flow of the motion, plse do the needful things.
   
 17. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Thanks Ruta, Quinine and others
   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Apr 18, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Nccr na cuf.....
   
Loading...