Siku 100 za SUK: Zanzibar yahitaji msaada wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku 100 za SUK: Zanzibar yahitaji msaada wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Feb 14, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  [​IMG] [​IMG]
  Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, akihutubia kwenye Maadhimisho ya 20 ya Jumuiya wa Mataifa na Watu Wasiowakilishwa Kwenye Umoja wa Mataifa, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa kimataifa wa Kasri ya Amani, mjini The Hague, Uholanzi, tarehe 11 Februari 2011 (Picha kwa hisani ya Deutsche Welle)
  Linapokuja suala la Zanzibar, ninachukia sana kile kibaya ninachokiandika dhidi yake kikaja kikathibitika kuwa cha kweli. Nakhiyari nisutwe kwamba, nilikuwa mtoto au nilikwenda mbali mno katika hoja na hukumu zangu, kuliko kuja kupongezwa, kwamba: “Lakini hata Mohammed Ghassany alisema!”
  Ukiniuliza kwa nini, nitakwambia sababu. Ninaipenda sana Zanzibar yangu, kiasi ya kwamba ninaishi kwa ajili yake, na kama itakuja kubidi, sitasita kufa kwa ajili yake.
  Wala si kwamba mimi ni mzalendo sana kuliko wengine. Siko peke yangu. Wenye mapenzi kwa nchi iliyotuzaa, ikatulea na kutupa kila fursa ambayo leo hii tunayo, tuko mamia kwa maelfu ndani ya ardhi ya Zanzibar na nje yake.
  Na ni malaki haya ya Wazanzibari, ndio ninaozungumza nao kwenye makala hii. Wapendwa, Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUKZ) inahitaji kusaidiwa halan wajiban, kusudi ifanikiwe kuifanikisha Zanzibar yetu, tunayokubali kwamba tunaipenda.
  Na labda hapa tungeliweka vigezo vya hayo tunayotaka yaitwe kuwa mafanikio ya SUKZ. Mimi naviona vitatu:
  Cha kwanza, ni kuweza kwake kudumu kwenye umoja wa kweli kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Katika hili, wala tusiwe watu wenye kutaka nyingi nasaba, tukaangukia kwenye mwingi msiba.
  Tukubaliane kwamba Zanzibar yetu iligawanywa (kwa sababu yoyote iwayo na yeyote awaye) kwa zaidi ya nusu karne. Ndani ya nusu karne hiyo, hasara tuliyoipata si ndogo. Kwa maneno ya Muyaka Haji Al-Ghassany, ilikuwa ni “ngome intumiiza naswi tu mumo ngomeni!”.
  Kwa hivyo, vile kuweza kukaa tu viongozi wa SUK pamoja, wakawa wanatazamana tu, wanazungumza na kusalimiana, kama ndugu wamoja, hayo yatakuwa ni mafanikio makubwa sana. Na hii SANA naomba niitilie mkazo.
  Kigezo cha pili, ni kuwa katika mikakati ya utekelezaji wa sera zake, ama ikiwa itakuwa na kile kinachoitwa minimum policy, ambao ni mchanganyiko wa sera za vyama vinavyounda serikali, au wakiwa wamekubaliana na matakwa ya katiba, ambayo yanataka sera ya chama kinachotoa rais, ndiyo itekelezwe katika uendeshaji wa serikali, basi kwetu tuipe asilimia 30 tu ya utekelezaji.
  Ikiwa kila mwaka, SUK itafanikiwa kutekeleza asilimia 30 ya mipango yake katika kila sekta, basi hayo ni mafanikio makubwa. Muhimu iwe asilimia hiyo ndogo imefikiwa kwa ufanisi wa hali ya juu, kwa kila maana ya neno hili, yaani gharama ndogo, uzalishaji wenye kiwango na, kwa hivyo, faida kubwa.
  Kigezo cha tatu, SUK iweze kuufanikisha uchaguzi wa 2015 kwa vigezo vyote vya uchaguzi wa kidemokrasia. Kuanzia uandiishaji wapiga kura hadi utangazaji matokeo na ukabidhianaji madaraka, pawepo na uwazi, uadilifu na haki. Hayo yatakuwa mafanikio makubwa sana ya serikali hii.
  Sasa, katika kila kigezo kati ya hivi vitatu, pana kazi ya kufanywa. Na nimegundua kuwa, kazi kubwa zaidi kumbe iko mikononi mwa wale walio nje ya SUK, kwa maana ya baraza la mawaziri na viongozi wake wakuu, Rais na Makamo wake wawili.
  Kazi kubwa zaidi iko kwetu. Na hapa nitapiga mfano wa kigezo cha kwanza. Ili SUK iweze kukaa miaka mitano, bila kutetereka, kunawezekana tu, ikiwa sisi tulio nyuma yao tunajenga mazingira hayo. Msingi wa SUK ni Maridhiano, ambayo yalitokana na imani. Kwa hivyo, ni sawa kusema kuwa msingi hasa wa SUK ni imani.
  Tafauti na mahusiano yaliyojengwa kwa damu au maslahi ya kifedha, mahusiano yaliyojengwa kwa msingi wa imani yana tabia ya kuathirika haraka. Ni pale tu imani hiyo inapotoweka. Na pana mstari mwembamba sana baina ya kuamini na kukana. Mstari ambao ni rahisi kuuchupa na shetani ni hodari sana wa kutuchupisha. Dhana ya serikali kwa Zanzibar si ya jana na leo, lakini dhana ya serikali ya umoja wa kitaifa ni changa sana. Yahitaji kulelewa na walezi ni mimi na wewe!
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Feb 15, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Hivi Zanzibar nayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Mataifa na Watu Wasiowakilishwa Kwenye Umoja wa Mataifa!! Kuna kipindi fulani Tanzania iliwakilishwa huko na Salim Ahmed Salim tena kwa muda mrefu sana, hivi yeye hakuwa na interest za Zanzibar pia.?


  Kuwa na serikali ya umoja (mseto) na kuondoa upinzani ni kudumaza demokrasi. Kulikuwa hakuna haja ya kuunda serikali ya mseto, bali kilichotakiwa ni kwa serikali iliyoko madarakani kuheshimu na kuwatendea haki raia wote bila kujali vyama vyao. Inapofika wakati wa uchaguzi, basi kila mgombea anaheshimiwa kama mgombea na kura zake zinahesabiviwa vizuri bila kuchakuchuliwa, aliyeshindwa kihalali anajipanga upya na aliyeshinda kihalali anaongoza Taifa lote kwa haki tu. Nchi zote za magharibi zinazotupatia misaada zina vyama vingi na mambo yao yanaenda vizuri bila kuumizana, iweje sisi ndiyo tuwe tunaumizana kwa sababu za kisiasa?
   
Loading...