Siku 100 za Serikali ya CHADEMA madarakani

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
MAMBO YA SIKU 100 ZA KWANZA

Ndani ya siku 100 tangu siku ya kuapishwa kwa Rais na Wabunge, watakaokuwa wamechaguliwa, Serikali ya Chadema itafanya
taratibu zinazohusika ili kuhakikisha yafuatayo yanatendeka:

i) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Maridhiano, ambayo pamoja na mambo mengine itaanzisha Tume ya Maridhiano kwa lengo la kuondoa hofu ya uwezekano wa vitendo vya kulipiza visasi na kuunganisha nguvu za wananchi wote bila ubaguzi wa vyama katika kuongoza Taifa letu.

ii) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi juu ya Utoaji wa Elimu Bure kuanzia elimu ya awali hadi Sekondari.

iii) Serikali itapunguza kiwango cha marejesho ya mikopo ya elimu ya juu hadi kufikia asilimia tatu (3) ya mshahara wa mnufaika na kutanua wigo wa muda wa marejesho hadi kufikia miaka 25 tangu mnufaika apate ajira. Aidha, Serikali itafuta riba na tozo zote zitokanazo na adhabu ya kuchelewesha marejesho ya mkopo wa elimu ya juu.

iv) Serikali itashirikiana na sekta binafsi kuweka utaratibu wa kutoa huduma za afya ya msingi kwa wananchi bila malipo.

v) Serikali itarejesha mchakato wa Katiba Mpya kuanzia ilipoishia Rasimu ya Tume ya Marekebisho ya Katiba ya Jaji Warioba

vi) Serikali ya Chadema itatekeleza matakwa ya Katiba kuhusu Tume ya Pamoja ya Fedha ya Muungano ili kila nchi Mshirika wa Muungano ipate mgao wake wa fedha kwa mujibu wa Katiba na sheria.

vii) Serikali ya Chadema itarejesha uhuru wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kuruhusu vyombo hivyo kurusha moja wa moja vikao vya Kamati za Bunge, Mikutano ya Bunge na Mwenendo wa Uendeshaji wa Mashauri Mahakamani.

viii) Serikali ya Chadema itapeleka miswada ya Sheria Bungeni kwa madhumuni ya kuzifuta Sheria zote kandamizi na zinazokiuka misingi ya haki za binadamu.

ix) Kuanzisha utaratibu wa mazungumzo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Zanzibar kwa lengo la kufikia muafaka juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi, uvuvi wa bahari kuu na usajili wa meli.

x) Serikali ya Chadema itaandaa mazingira rafiki na wezeshi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari walioshindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali kama vile ugonjwa, kukosa ada, mimba n.k. kurejea kwenye mfumo rasmi wa elimu na kumalizia masomo yao.

xi) Serikali ya Chadema itapeleka bajeti ya Nyongeza Bungeni katika mwaka wa fedha 2020/2021 kwa ajili ya kuongeza Mishahara ya watumishi wote wa umma, kulipa malimbikizo; sambamba na kuwapandisha madaraja watumishi wenye sifa na kulipa mishahara inayoendana na madaraja yao.

xii) Serikali ya Chadema itaanzisha bima maalum ya afya kwa watumishi wote wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wawapo kazini na baada ya kustaafu vikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zima moto na Uokoaji.

xiii) Serikali ya Chadema itarejesha maduka yasiyotozwa kodi (Duty free shops) katika vyombo vya ulinzi na usalama vikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji.

xiv) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii ili kurekebisha kikokotoo cha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa wastaafu ili kiendane na mahitaji ya wastaafu. Aidha, Serikali ya Chadema itaruhusu wafanyakazi na watumishi waliochangia katika mifuko ya jamii kuchukua mafao yao wakati wowote (fao la kujitoa).

xv) Serikali ya Chadema itaweka utaratibu na kuwatafutia masoko wakulima, wavuvi na wafugaji ya kuuza mazao yao ndani na nje ya nchi bila kizuizi.

xvi) Kurejesha utaratibu wa awali wa ukusanyaji wa kodi, ushuru na tozo mbalimbali kwa mamlaka ya serikali za mitaa

IMG-20200831-WA0035.jpg
 
MAMBO YA SIKU 100 ZA KWANZA

Ndani ya siku 100 tangu siku ya kuapishwa kwa Rais na Wabunge, watakaokuwa wamechaguliwa, Serikali ya Chadema itafanya
taratibu zinazohusika ili kuhakikisha yafuatayo yanatendeka:

i) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Maridhiano, ambayo pamoja na mambo mengine itaanzisha
Tume ya Maridhiano kwa lengo la kuondoa hofu ya uwezekano wa vitendo vya kulipiza visasi na kuunganisha nguvu za wananchi wote bila ubaguzi wa vyama katika kuongoza Taifa letu...
Huyu akitoka usingizini atakuta watu tunaendelea na kazi tu

MAGUFULI4LIFE.
 
Inherent monopoly ya mabeberu walio iyacha africa bado itaendelea kututafuna sio kwa upinzani wala kwa CCM bado ukombozi wa maisha ya mwananchi wa tabaka la chini ambae ndie mnyonge wa nchi hii itachukua mda sana kukombolewa!. Kama ilani ya vyama ndio hizi yaani hayo ndio maono ya wanasiasa wetu! Kazi ipo.
MAMBO YA SIKU 100 ZA KWANZA

Ndani ya siku 100 tangu siku ya kuapishwa kwa Rais na Wabunge, watakaokuwa wamechaguliwa, Serikali ya Chadema itafanya
taratibu zinazohusika ili kuhakikisha yafuatayo yanatendeka:

i) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Maridhiano, ambayo pamoja na mambo mengine itaanzisha Tume ya Maridhiano kwa lengo la kuondoa hofu ya uwezekano wa vitendo vya kulipiza visasi na kuunganisha nguvu za wananchi wote bila ubaguzi wa vyama katika kuongoza Taifa letu.

ii) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi juu ya Utoaji wa Elimu Bure kuanzia elimu ya awali hadi Sekondari.

iii) Serikali itapunguza kiwango cha marejesho ya mikopo ya elimu ya juu hadi kufikia asilimia tatu (3) ya mshahara wa mnufaika na kutanua wigo wa muda wa marejesho hadi kufikia miaka 25 tangu mnufaika apate ajira. Aidha, Serikali itafuta riba na tozo zote zitokanazo na adhabu ya kuchelewesha marejesho ya mkopo wa elimu ya juu.

iv) Serikali itashirikiana na sekta binafsi kuweka utaratibu wa kutoa huduma za afya ya msingi kwa wananchi bila malipo.

v) Serikali itarejesha mchakato wa Katiba Mpya kuanzia ilipoishia Rasimu ya Tume ya Marekebisho ya Katiba ya Jaji Warioba

vi) Serikali ya Chadema itatekeleza matakwa ya Katiba kuhusu Tume ya Pamoja ya Fedha ya Muungano ili kila nchi Mshirika wa Muungano ipate mgao wake wa fedha kwa mujibu wa Katiba na sheria.

vii) Serikali ya Chadema itarejesha uhuru wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kuruhusu vyombo hivyo kurusha moja wa moja vikao vya Kamati za Bunge, Mikutano ya Bunge na Mwenendo wa Uendeshaji wa Mashauri Mahakamani.

viii) Serikali ya Chadema itapeleka miswada ya Sheria Bungeni kwa madhumuni ya kuzifuta Sheria zote kandamizi na zinazokiuka misingi ya haki za binadamu.

ix) Kuanzisha utaratibu wa mazungumzo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Zanzibar kwa lengo la kufikia muafaka juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi, uvuvi wa bahari kuu na usajili wa meli.

x) Serikali ya Chadema itaandaa mazingira rafiki na wezeshi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari walioshindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali kama vile ugonjwa, kukosa ada, mimba n.k. kurejea kwenye mfumo rasmi wa elimu na kumalizia masomo yao.

xi) Serikali ya Chadema itapeleka bajeti ya Nyongeza Bungeni katika mwaka wa fedha 2020/2021 kwa ajili ya kuongeza Mishahara ya watumishi wote wa umma, kulipa malimbikizo; sambamba na kuwapandisha madaraja watumishi wenye sifa na kulipa mishahara inayoendana na madaraja yao.

xii) Serikali ya Chadema itaanzisha bima maalum ya afya kwa watumishi wote wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wawapo kazini na baada ya kustaafu vikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zima moto na Uokoaji.

xiii) Serikali ya Chadema itarejesha maduka yasiyotozwa kodi (Duty free shops) katika vyombo vya ulinzi na usalama vikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji.

xiv) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii ili kurekebisha kikokotoo cha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa wastaafu ili kiendane na mahitaji ya wastaafu. Aidha, Serikali ya Chadema itaruhusu wafanyakazi na watumishi waliochangia katika mifuko ya jamii kuchukua mafao yao wakati wowote (fao la kujitoa).

xv) Serikali ya Chadema itaweka utaratibu na kuwatafutia masoko wakulima, wavuvi na wafugaji ya kuuza mazao yao ndani na nje ya nchi bila kizuizi.

xvi) Kurejesha utaratibu wa awali wa ukusanyaji wa kodi, ushuru na tozo mbalimbali kwa mamlaka ya serikali za mitaa

View attachment 1554779
Yesu kama masih, alizaliwa kwenye zizi la ng'ombe hiyo ilikuwa ni hatua ya ukombozi wa mwanadamu ili kufikia wanyonge na watu wachini kabisa.

Tazama leo hi sera za vyama vyetu vya siasa kama mkombozi wa wanyonge wa taifa hili.

Wanataja mambo kama
1. Bima ya afya .....wanamlenga mnyonge?
2. Ongezeko la mishahara...... inalenga kuongezeka kwa pembejeo za wanyonge?
3. Ajira........ matreka, mabomba mangapi ya kilimo watayaleta kwa ajiri ya aridhi tamu na ya kuvutia ambayo MUNGU katuzawadia

Ngoja niishie hapo hasira zipungue kwanza kwani wanatia kichefuchefu ukombozi wa mwafirika utatoka wapi? Yale mawazo ya mwalimu na kwame hivi walizikwa nayo? Jameni leo kampeni tunafanya fasheni vua ni kuvae, panda shuka nipe ni kupe kweli?

Sisi ambao tupo Gosiba MUNGU atusaidie sana.
 
MAMBO YA SIKU 100 ZA KWANZA

Ndani ya siku 100 tangu siku ya kuapishwa kwa Rais na Wabunge, watakaokuwa wamechaguliwa, Serikali ya Chadema itafanya
taratibu zinazohusika ili kuhakikisha yafuatayo yanatendeka:

i) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Maridhiano, ambayo pamoja na mambo mengine itaanzisha Tume ya Maridhiano kwa lengo la kuondoa hofu ya uwezekano wa vitendo vya kulipiza visasi na kuunganisha nguvu za wananchi wote bila ubaguzi wa vyama katika kuongoza Taifa letu.

ii) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi juu ya Utoaji wa Elimu Bure kuanzia elimu ya awali hadi Sekondari.

iii) Serikali itapunguza kiwango cha marejesho ya mikopo ya elimu ya juu hadi kufikia asilimia tatu (3) ya mshahara wa mnufaika na kutanua wigo wa muda wa marejesho hadi kufikia miaka 25 tangu mnufaika apate ajira. Aidha, Serikali itafuta riba na tozo zote zitokanazo na adhabu ya kuchelewesha marejesho ya mkopo wa elimu ya juu.

iv) Serikali itashirikiana na sekta binafsi kuweka utaratibu wa kutoa huduma za afya ya msingi kwa wananchi bila malipo.

v) Serikali itarejesha mchakato wa Katiba Mpya kuanzia ilipoishia Rasimu ya Tume ya Marekebisho ya Katiba ya Jaji Warioba

vi) Serikali ya Chadema itatekeleza matakwa ya Katiba kuhusu Tume ya Pamoja ya Fedha ya Muungano ili kila nchi Mshirika wa Muungano ipate mgao wake wa fedha kwa mujibu wa Katiba na sheria.

vii) Serikali ya Chadema itarejesha uhuru wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kuruhusu vyombo hivyo kurusha moja wa moja vikao vya Kamati za Bunge, Mikutano ya Bunge na Mwenendo wa Uendeshaji wa Mashauri Mahakamani.

viii) Serikali ya Chadema itapeleka miswada ya Sheria Bungeni kwa madhumuni ya kuzifuta Sheria zote kandamizi na zinazokiuka misingi ya haki za binadamu.

ix) Kuanzisha utaratibu wa mazungumzo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Zanzibar kwa lengo la kufikia muafaka juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi, uvuvi wa bahari kuu na usajili wa meli.

x) Serikali ya Chadema itaandaa mazingira rafiki na wezeshi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari walioshindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali kama vile ugonjwa, kukosa ada, mimba n.k. kurejea kwenye mfumo rasmi wa elimu na kumalizia masomo yao.

xi) Serikali ya Chadema itapeleka bajeti ya Nyongeza Bungeni katika mwaka wa fedha 2020/2021 kwa ajili ya kuongeza Mishahara ya watumishi wote wa umma, kulipa malimbikizo; sambamba na kuwapandisha madaraja watumishi wenye sifa na kulipa mishahara inayoendana na madaraja yao.

xii) Serikali ya Chadema itaanzisha bima maalum ya afya kwa watumishi wote wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wawapo kazini na baada ya kustaafu vikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zima moto na Uokoaji.

xiii) Serikali ya Chadema itarejesha maduka yasiyotozwa kodi (Duty free shops) katika vyombo vya ulinzi na usalama vikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji.

xiv) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii ili kurekebisha kikokotoo cha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa wastaafu ili kiendane na mahitaji ya wastaafu. Aidha, Serikali ya Chadema itaruhusu wafanyakazi na watumishi waliochangia katika mifuko ya jamii kuchukua mafao yao wakati wowote (fao la kujitoa).

xv) Serikali ya Chadema itaweka utaratibu na kuwatafutia masoko wakulima, wavuvi na wafugaji ya kuuza mazao yao ndani na nje ya nchi bila kizuizi.

xvi) Kurejesha utaratibu wa awali wa ukusanyaji wa kodi, ushuru na tozo mbalimbali kwa mamlaka ya serikali za mitaa

View attachment 1554779
Kwenye nchi gani?
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom