Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,277
- 8,859
MKWAMO wa kisiasa visiwani Zanzibar umetia najisi sifa na mafanikio ya Rais John Magufuli katika siku 100 alizokuwepo madarakani zinazofikia kesho tangu aapishwe tarehe 5 Novemba mwaka jana, anaandika Faki Sosi.
Waliotoa maoni yao kwa MwanaHALISI Online wametofautiana mtazamo kuhusu siku 100 za Rais Magufuli madarakani huku wengine wakisema ameshindwa kufikia maratajio ya wengi hususani utatuzi wa mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar.
Alhad Mussa, Sheikh Mkuu wa MKoa wa Dar es Salaam amesema kuwa siku 100 za Rais Magufuli ni za baraka na neema kwa Watanzania na kwamba zimetoa nuru na heshima kubwa kwenye serikali yake.
Amesema, ameokoa kiasi kikubwa cha fedha na kwamba Watanzania watafurahia keki ya Taifa ambapo ameshauri wananchi kushikamana na kauli mbiu yake ya ‘Hapa Kazi Tu.’
“Kauli mbiu hii imeridhiwa na Mungu kwani Mungu aliumba mbingu na ardhi kwa kuashiria kuwa kazi ni wajibu,” amesema Sheikh Alhad.
Dk. Benso Bana ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amesema, siku 100 za uongozi wa Rais Magufuli amevunja rekodi ya kuwa rais pekee Afrika mwenye utendaji wa kasi lakini pia ametofautiana na watangulizi wake kiutendaji.
“Rais Magufuli amekuwa ni tumaini kwa Watanzania, ndani ya siku 100 amewawajibisha watumishi waandamiza zaidi ya 190,” amesema Dk. Bana.
Hata hivyo, kuhusu mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar Dk. Bana amesema, Rais Magufuli hapaswi kulaumiwa kutokana na kwamba yeye anajua kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ndio iliyo na mamlaka na uchaguzi huo.
Amedai kwamba ZEC inaweza kusimamia suala hilo na kwamba anazitaka nchi za Ulaya zisipewe nafasi kuingilia mgogoro huo kwa kuwa zinaweza kuuzidisha.
Profesa Abdall Sharrif ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Katiba Zanzibar (BAKIZA) amesema, katika siku 100 za Rais Magufuli hakufanya cha ajabu.
Amesema siku hizo 100 za Rais Magufuli ni kama amekuja kusalimu na kusimamisha watu kazi huku akikwepa nafasi yake ya kutatua mgogoro wa Zanzibar kwa kudai hana mamlaka wakati vurugu zitakapozuka, atatumia majeshi yake kwenda kuzizima.
“Majeshi ya Jamhuri ya Muungano ndio yaliyoua Wazanzibari mwaka 2001 na hayo hayo yanaweza kutumika tena kufanya kile kilichofanywa mwaka huo,” amesema.
Prof. Sharifu amemsifu Ibrahimu Kaduma ambaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa mkweli na kujitokeza mbele ya umma.
Amesema kuwa, hatua ya Kaduma kusema kwamba chama chake (CCM) kimeshindwa na kiwaachie walioshinda ni ujasiri ambao alipaswa kuwa nao Rais Magufuli na ingeleta tija kwa taifa.
Sheikh Ponda Issa Ponda ambaye ni Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kislamu nchini amesema kuwa, Rais Magufuli ameonesha nia ya kutaka uwajibikaji kwa watumishi wa umma.
Amesema, pamoja na hivyo lakini ameshindwa kusimamia utatuzi wa mgogoro wa kisiasa unaondelea Zanzibar na kwamba, visiwani humo kumetokea uvunjifu wa katiba uliofanywa na Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa ZEC.
Sheikh Ponda amesema kuwa, kiongozi huyo ameunda Baraza la Mawaziri bila kuzingatia usawa wa dini na kwamba, kwenye baraza hilo kuna mawaziri wanane tu ambao ni Waislamu.
Amesema kuwa, Rais Magufuli hatakiwi kusikiliza ushauri wenye ukada ndani yake kwani wanaCCM wengi hawana uzalendo na nchi.
Sheikh Ponda amemtaja Benard Membe ambaye alikuwa Waziri Mambo ya Nje katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwa, alimshauri Rais Magufuli njia sahihi ya kutatua mgogoro wa Zanzibar.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Benson Bagonza amesema kuwa, Rais Magufuli anafukia shimo kwa kuchimba shimo lingine kutokana na kushindwa kupata ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzaibar.
Amesema kwamba, mgogoro huo hauwezi kutatuliwa kwa kutumia majeshi wala silaha za moto pia kurudia uchaguzi isipokuwa maafikiano.
“Kuvurukiga kwa uchaguzi wa Zanzibar sio suala geni na kwamba kwanini chaguzi za nyuma hazijarudiwa,”amehoji Askofu Bagonza huku akionesha kushangazwa na Rais Magufuli kushindwa kupata ufumbuzi wa mgogoro huo mpaka sasa.
Akitoa maoni yake juu ya utendaji wa siku 100 za Rais,Tundu Lissu amesema Rais Magufuli amevuruga bunge na kamati zote muhimu na wala kamati hazikuvurugwa na spika wa bunge kama ambavyo wengi wanavyoaminishwa.

Nianze kwa kusisitiza kuwa ni siku 100 kati ya takribani zaidi ya siku 1825 za miaka mitano(5).
Aidha nami nianze kwanza kukupongeza Mheshimiwa rais Dr. John Pombe Magufuli, siku 100 ofisi umefanya mambo makubwa na mazuri. Nchi ilikuwa imefikia pabaya siyo rahisi uwafurahishe wote lakini katika mazingira hayo, wengi watakuwa wamefurahia hizi siku 100 na katika mazingira hayo hayo siku zote wachache lazima waumie kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Tembea kifua mbele rais wetu, umepongezwa na hata wale ambao kumpongesa mtu huwa ni miujiza. Pamoja na pongezi zao kama kawaida yao neno LAKINI halikosekani vinywani mwao.
Baadhi ya wachache wasio na mazoea ya kumpongeza mtu hata akifanya vizuri vipi na maneno yao ni pamoja na:
1. Zitto Zuberi Kabwe(Kiongozi Mkuu wa ACT-WAZALENDO na Mbunge wa Kigoma mjini.)
Anasemaje: "Nilitarajia Mgufuli angekuwa Kiongozi atakayeweza kubadili mfumo wa nchi yetu katika maeneo muhimu lakini hadi sasa nilichokiona ni KUBANA matumizi , kufukukuza watumishi na kuongeza juhudi za kukusanya mapato lakini bila kufanya mabdiliko ya vyombo husika kimkakati. Siku 100 ni chache kumhukumu kiongozi ambaye amepewa miaka mitano ya kutawala, ingawa zinaweza kuonyesha picha ya aina gani ya kiongozi ambaye taifa linaweza kuwa naye katika kipindi hicho.*
Tafakuri: Kwanza ni jambo jema Zitto kutambua kuwa rais anabana matumizi, kufukuza watumishi wahujumu uchumi na kuweka juhudi katika kukusanya mapato na kwamba siku 100 ni chake kumhukumu rais. Kwa upande mwingine, Zitto ambaye kati ya Wabunge wa Upinzania waliobaki Bungeni wakati Rais analihutubia Bunge ni yeye, lakini zake zinatokana na mambo makuu mawili ambayo hayana tija kwa taifa. Moja ni kutaka kukubalika ndani ya UKAWA, dalili ambazo zilianza kuonekana wakati kiongozi wa Upinzani Bungeni akijiandaa kutangaza bazara kivuli. Jambo la pili ni kinyongo tu kwa sababu rais ameona faida kubwa kuliko hasara za kumrejesha Waziri Muhongo katika Wizara ya Nishati na Madini pamoja na kwamba aliiongoza Wizara hiyo wakati wa ESCROW. swali la msingi tu ambalo ningependa kumuuliza Zitto ni je ndani ya siku 100 za uongozi wa rais kipi kilitakiwa kutangulia kati kuwatimua wahujumu uchumi na kubadili mifumo katika vyombo ambavyo wahujumu hao walihudumu?
2. Prof. Kitila Mkumbo(Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam na mshauri wa mambo ya siasa ndani ya ACT-WAZALENDO)
Anasemaje: "Rais Magufuli amejipambanua vizuri kama Kiongozi atakayepambana vizuri na kero za kijamii kama vile rushwa na ufisadi. Hata hivyo rais bado hajajipambanua katika maeneo mengine matatu muhimu ya Kiongozi , ambayo ni falsafa, dira na ulinzi wa tunu za kitaifa.
Kipimo cha siku 100 kinachowekwa kwa marais wapya, kilianza kutumika nchini Marekani kutokana na mafanikio ya Rais Franklin Delano Roosevelt aliyeapishwa Machi 4, mwaka 1933 na ndani ya siku 100 alikuwa amepitisha sheria mpya 15 zilizosaidia kufufua uchumi wa Marekani.*
Tafakuri: Bado Prof. Anacheza ndani ya aliyotangulia kuyasema Kiongozi wake wa chama au inawezekana yeye ndiye ametembea ndani ya maneno ya Prof. Kutolea mfano wa Rais wa Marekani eti alitumia siku 100 kufanya mageuzi ndano ya Taifa hilo bila kusema aliikuta nchi ikiwa na hali gani, watu gani walikuwa wanamzunguka ni kutomtendea haki rais.
3. Shekh Ponda Issa Ponda(Katibu Mkuu wa jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini).
Anasemaje: Rais Magufuli anaonesha nia ya kutaka uwajibikaji kwa watumishi wa Umma. Pamoja na hayo ameshindwa kusimamia utatuzi wa mgogoro wa Zanzibar.
Tafakuri: Rais anatengenezewa mazingira ya kauli za wabaya wake kuwa ni DIKTETA zihalalishwe. Rais aingilie mgogoro wa Zanzibar kwa kipengele gani cha Katiba au kipengele gani cha sheria ya Uchaguzi? Kuingilia ZEC kuna tofauti na kuingilia Maamuzi ya Mahakama, Bunge n.k?
4. Benson Bagonza(Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Dayosisi ya Karagwe Mkoani Kagera.
Anasema: -Rais Mgufuli anafunika shimo kwa kuchimba shimo lingine kutokana na kushingwa kupata ufumguzi wa mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar.
Tafakuri: Itashangaza sana kuona Kiongozi yeyote wa KKKT nchini akisifia uongozi wa awamu ya tano chini ya rais Dr. John Pombe Magufuli. Kufanya hivyo ni kumsaliti LOWASSA ambaye amewekeza nguvu na mali zake nyingi kwenye kanisa hilo. Nisharti WALUTHERI waendelee kuamini rais wao ni LOWASSA na si vinginevyo. Wanayoyasema viongozi wake yanaakisi ukweli huo.
5. Prof. Abdall Sharrif(Mwenyekiti wa Baraza la Katiba Zanzibar(BAKIZA)).
Anasema: Katika siku 100 za rais Magufuli hakufanya cha ajabu. Ni kama amekuja kusalimu na kusimamia watu kazi huku akikwepa nafasi ya kutatua mgogoro wa Zanzibar kwa kudai hana mamlaka wakati vurugu zitakapozuka , atatumia majeshi yake kwenda kuzizima.
Tafakuri: Matumizi ya vyombo vya ulinzi kwenye vurugu ni haki ya kikatiba ya rais(yeye ndo Amri jeshi mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa nchi). Rais hawezi kuingilia vyombo vingine kama Mahakama, Bunge na tume za uchaguzi. Kufanya hivyo ni UDIKTETA ambao watu wasio wajua dikteta ni nani wanamuita rais wetu hivyo. Polisi, jeshi na vyombo vongine vya ulinzi wataingia hata ikulu endapo rais ataanzisha vurugu . Ndiyo maana wanaingia Bungeni, Mahakamanin.k. huko ndiko mahali pao pa kujidai.
NARUDIA TENA: RAIS USIKATISHWE TAMAA NA HIZI LAKINI zao, Watanzania wasa wanyonge tuna imani nawe.