Ocampo four
JF Senior Expert Member
- Feb 28, 2014
- 5,789
- 2,159
Mhhhh!! Hayo yote ndani ya siku 100. Nadhani hata baraza la mawaziri litakuwa bado halijaanza kazi.
1. Uhakika wa dawa na vifaa vya uzazi.
2. Umeme wa uhakika nchi nzima.
3. Kuanzisha mchakato wa katiba mpya.
4. Kupunguza foleni Dar-Es-Salaam na miji mikubwa.
5. Kuondoa kero kwa wafanya biashara ndogondogo (Machinga), Mamantilie na bodaboda.
6. Kuweka mipango kabambe ya Kumaliza tatizo la maji nchi nzima.
7. Mfumo bora na rafiki kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa.
8. Kufuta ada na michango kwa wanafunzi kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.
9. Kupunguza kodi ya mshahara kwa wafanyakazi (PAYE).
10. Kufuta kodi zote za mazao kwa wakulima, wavuvi na wafugaji.
11. Mkakati wa kukuza michezo, sanaa na utamaduni.
12. Kuunda tume maalum ya kutatua migogoro ya wafugaji na wakulima.
13. Kuanzisha kituo kila wilaya kutoa huduma za serikali (one~stop centre).
14. Kuboresha maslahi ya watumishi wa vyombo vya usalama (polisi, wanajeshi, Takukuru). Kuboresha maslahi ya walimu, watumishi wa afya na watumishi wa serikali kwa ujumla.
15. Kuweka dira na mipango ya kuelekea katika uchumi wa kipato cha kati.
Baada ya hizo siku. Atuibie tena? # hapa ni kazi tu.
Ukiangalia yote hayo katibu 8 yanawezekana hata ndani ya siku 20.... Tatizo kubwa viongozi wa CCM wanakosa utashi wa kisiasa...
Kiongozi mzuri anapimwa ndani ya siku 100 duniani kote
Hatuhitaji mtu ambaye utawala wake ni wa siku 100 tu. kiongozi mzuri ni yule anayepanga mikakati ya zaidi ya muongo mmojaMzee wa pushup hajui atafanya nini ndani ya siku 100. Anasubiri maelekezo kutoka kwa WAMA Family
Sasa kama alikaa madarakani kwa muda wa siku 800 akiwa Waziri Mkuu na hakufanya hayo atawezaje ndani ya siku 100? Tumia akili. Lowasa ni sumu iliyojificha ndani ya asali
Sio kosa lako maana hata hizi sio akili zakoHatuhitaji mtu ambaye utawala wake ni wa siku 100 tu. kiongozi mzuri ni yule anayepanga mikakati ya zaidi ya muongo mmoja
Mhhhh!! Hayo yote ndani ya siku 100. Nadhani hata baraza la mawaziri litakuwa bado halijaanza kazi.