SIKITIKO LANGU! Tanzania itabadilishwa na Watanzania wanaothubutu mabadiliko! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SIKITIKO LANGU! Tanzania itabadilishwa na Watanzania wanaothubutu mabadiliko!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ras, Sep 8, 2010.

 1. Ras

  Ras Senior Member

  #1
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu Watanzania, nawasalimu sana. Niandikapo thread hii najisikia uchungu sana moyoni. Hapo awali kabla sijatoka Tanzania na kutembelea nchi zingine niliona maisha yapo sawa tu kwa hapo Tanzania.

  Lakini kwa sasa nipo nje ya nchi kwa kweli maisha ninayoona wanaishi wenzetu huku ni yale ambayo wengi wetu hapo nyumbani na tunaoamini dini twajipa moyo kuwa tutajaishi tukifa huko Paradiso!! I WAS VERY WRONG THINKING THAT GOOD LIFE CAN BE FOUND ONLY IN PARADISE!! PARADISE twaweza itengeneza sisi wenyewe kwa kuwa na MAAMUZI YENYE BUSARA KWA WAKATI MUAFAKA.

  Tuachane na zile fikra kuwa pengine chama fulani kisipokuwa tawala kutatokea vita na amani haitokuwepo, NINI MAANA YA AMANI IWAPO WATU WANAKUFA KWA NJAA HUKO VIJIJINI?? Hospitali huduma hafifu!! Ujambazi unashamiri!! Nadhani ni wakati muafaka sasa wa kubadili mfumo! Hebu tuthubutu na tuone, uzuri ni kuwa miaka mitano tunafanya tena uchaguzi,

  Tuchague na viongozi toka vyama vingine tuone mabadiliko! kama hayapo then uchaguzi mwingine tunachagua mwenye sera nzuri na zinazotekelezeka tukumbuke usemi kuwa "HE WHO DARE TO RISK SUCCEEDS" Wenztu huku hawaangalii sera za kusadikika! wanaangalia sera zenye kujenga uchumi wa Taifa!!

  Hebu angalia thamani ya pesa ya Tanzania inavyoporoka kila kukicha!!! ni dalili mbaya. Kwa kweli ukiangalia wenzetu huku nje(Nipo bara la Asia) wanavyo-manage kodi zao na kuzitumia katika mambo ya maendeleo yanayoonekana, inatia uchungu sana sisi kwa nini tushindwe!! Si kwamba hakuna viongozi ambao ni Wazalendo wanaoweza kutufisha hapo lah! ni vile tu hatuthubutu kuwachagua.


  WITO WANGU! TUBADILIKE, TUCHAGUE MTU AMBAYE ANA UWEZO NA UZALENDO PIA, TUJARIBU KUWAPA AU KUKIPA CHAMA KINGINE HATAMU TUONE MAMBO YATAENDAJE, WAKISHINDWA UCHAGUZI MWINGINE HATUWAPI TENA. KWA NJIA HII TUTAENDELEA. INASIKITISHA KUITWA NCHI MASKINI WAKATI TUNA KILA KITU ISIPOUWA TWAKUMBATIA MFUMO NA VIONGOZI WABOVU NA WEVI!

  Samahani kama ntakuwa nimemkwaza yeyote ila huo ni uchungu wangu kama mzalendo! Laiti kama kila Mtanzania angeweza pata fursa ya kutoka na kuona nchi za Wenzetu zilivyopiga hatua! LAITI KAMA...nadhani tungefumbuka macho.
   
 2. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ras you have spoken well! unadhani basi kuna haja ya kila Mtanzania kutoka nje ya hapa ili kuona hayo uyasemayo! la siku hizi kwa maendeleo haya ya teknolojia watanzania tunayaona hayo usemayo kwenye Runinga na siku hizi kupitia tovuti/wavuti. Tatizo tulilonalo ni udumavu wa kufikiri, uwoga wa kuthubutu na ujinga wa kupandikizwa kuwa bila CCM nchi haitawaliki! jana nilimsikia mgombe a mmoja wa Ubunge jimbo la Arusha alinena vyema sana, kuwa moja ya sera zake ni kuamsha uwezo wa kufikiri wa waTanzania, atafanyaje sijajua, lakini nilifarijika kusikia tu kuwa ameliona tatizo la msingi hapa ni uelewa duni na uwezo wa kuthubutu tulionao. lakioni usijali sana mapambano ndio yameanza sasa, hatudanganyiki tena na kama haitakuwa leo basi kesho yaani Ras ninachosema hapa ni Mdogomdogo hadi Ikulu!
   
 3. Ras

  Ras Senior Member

  #3
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 4. M

  Maluo Member

  #4
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Do, tuwape na vyama vingine tuone! Just five or ten years
   
Loading...