Sikio la kufa kweli halisikii dawa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sikio la kufa kweli halisikii dawa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 21, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,480
  Likes Received: 81,772
  Trophy Points: 280
  CCM yateua 'mafisadi' kufadhili Kikwete 2010

  Na Saed Kubenea
  MwanaHALISI

  WATUHUMIWA wa ufisadi wameteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuunda kamati ya kukusanya fedha za uchaguzi mkuu ujao, MwanaHALISI limeelezwa.

  Uteuzi huo ulifanyika Dar es Salaam, wiki iliyopita, katika kikao cha sekretarieti kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba. Kamati hiyo inaundwa na wajumbe watano.

  Miongoni mwao, wamo watatu ambao wamekuwa wakituhumiwa kwa ufisadi mara kwa mara, na wako katika kundi ambalo lilipachikwa majina ya “watafuna nchi,” na “mafisadi papa.”

  Majina yaliyochomoza sana ni ya mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Abdulrasul Aziz, Tanil Somaiya na Mbunge wa Bukoba Vijijini, Nazir Karamagi.

  Wamo pia mfanyabiashara wa Morogoro, Abood Aziz Abood na Mohammed Dewji, mfanyabiashara na mbunge wa Singida Mjini.

  Makamba alipoulizwa kuhusu uteuzi wa wajumbe hao, alisema, “Vikao vya sekretarieti ni mambo ya siri. Mimi ndiye mwenyekiti…”

  Alipobanwa zaidi akang’aka, “Ni nani kawaambia mambo ya ndani ya sekretarieti? Huyo kawapa umbea…”

  Alipoelezwa kuwa ni yeye aliyevujisha siri kwa kumweleza mmoja wajumbe waliopendekezwa, Makamba alisema, “Nani huyo? Kama kuna mtu kawapigia simu kuwaeleza kuwa tulijadili ajenda hiyo katika vikao, ambavyo mimi ni mwenyekiti, basi kaeneza umbeya. Mpigieni tena.”

  Wajumbe hao waliopendekezwa na sekretarieti, wanasubiri kuidhinishwa na vikao vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM.
  Taarifa za ndani ya kikao zinasema uteuzi huo ulizusha zogo na mgawanyiko mkubwa miongoni mwa wajumbe wa sekretarieti.

  Waliokuwa wanapinga uteuzi huo, ambao ulisimamiwa na Makamba, walidai kuwa hatua hiyo ingeendelea kukichafua chama chao, ambacho kimekuwa kinahusishwa na ufisadi mkubwa wa vigogo na maswahiba wao.

  Baadhi ya wajumbe walimkumbusha Makamba kuwa yeye ndiye amekuwa akikanusha ufisadi wa CCM kwa nguvu zote, lakini uteuzi huu unaoingiza baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi katika orodha ya wafadhili wa chama, unaweza kusimika dhana kwamba “CCM ni chama cha mafisadi.”

  Mbunge mmoja wa CCM alinumkuu mjumbe wa kikao cha sekretarieti hiyo akisema, “wakati wote ambapo ajenda hiyo ilipokuwa inajadiliwa, Makamba alikuwa akitolea macho kila aliyekuwa anaonekana kupinga mapendekezo yake.”

  Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini, wamedokeza kwamba iwapo vikao vya juu vya CCM vitaridhia uteuzi wa wajumbe wanaotuhumiwa kwa ufisadi, upinzani utakuwa umepata mtaji mkubwa kisiasa.

  Inaeleweka kuwa baadhi yao ndio waliokifadhili chama hicho kwa fedha na raslimali nyingi katika uchaguzi uliopita, uliomwingiza Rais Jakaya Kikwete madarakani na ambaye tayari anapigiwa debe kugombea tena 2010.

  Mingoni mwa wafadhili wakubwa wa kampeni za Kikwete ni Rostam, anayehusishwa na ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi ya fedha za umma kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Ni Rostam huyo huyo anayedaiwa kuwa “mwasisi wa kampuni ya Kagoda Agricultural Ltd,” iliyosajiliwa 29 Septemba 2005, na ndani ya siku tano baada ya kusajiliwa ilichotewa Sh. 30.8 bilioni kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya BoT.

  Vile vile amekuwa anahusishwa na kashfa ya kampuni ya kitapeli ya kufua umeme wa dharura, Richmond Development (LLC).

  Somaiya anahusishwa na ufisadi kwenye ununuzi wa rada na ndege ya rais, huku Karamagi akihusishwa na mikataba kadhaa ya madini, kashfa ya Richmond na mkataba tata wa kampuni ya Kupakia na Kupakua Makontena katika Bandari ya Dar es Salaam (TICTS).
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Hivi wewe KUBENEA huna habari zingine za kuandika?Mambo ya CCM yanakuwasha nini,leave them alone whether wanachangua mafisadi or what is that of your interest?? ni binafsi nimekuchoka bana una kuwa na mambo ya umbea umbea sana
   
 3. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hawawezi kuwatupa Mafisadi, maana wakiwatosa hata pesa za kununulia kanga na kofia hawatapata. Pesa za kina Mengi pekee hazitoshi!
   
 4. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Na wathubutu kumtupa Rostam kama nchi haijawashinda
   
 5. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kigogo unasema mambo ya ccm yanamuwashia nini KUBENEA? unadhani kuna kitu kinaitwa mambo ya ccm? Siamini kama haujui implication ya mambo kama haya kwa taifa letu. Ingekuwa ccm ni kundi linaloishi mahali fulani halitegemei kodi wala rasilimali zetu tungewaachia waendelee na wanalotaka kufanya. Lakini ukitamka ccm kama chama tawala unatamka juu ya mustakabali wa nchi yetu kwani wao ndio wamepewa dhamana ya kuongoza kwa sasa...haya unayaju sana ila nadhani una sababu zako za kutuma post kama hii!

  Post hii ni kejeli kwa kina mama ambao wanajifungulia sakafuni katika hospitali zetu....ni kejeli kwa watoto waliozagaa mtaani wakisaka maisha baada ya kukimbia familia zao zilizoshindwa kuwalisha na kuwasomesha, ni kejeli kwa familia ambazo wameshindwa kulipa ada ya sh 20,000 kwa mwaka wa shule za kata na wamekamatwa wamewekwa katika ofisi za kata, ni kejeli kwa watoto wanaokufa na magonjwa yanayozuilika kama malaria, ni kejeli kwa wanafunzi wa chuo kikuu waliopangiwa kulipa asilimia 40 ilihali uwezo huo hawana na wenye uwezo wanalipiwa asilimia 100....HII NI KEJELI KWA SISI WAKULIMA AMBAO MSIMU WA KILIMO UMEFIKA HATUNA UHAKIKA WA PEMBEJEO...TUNATEGEMEA BADO KUDRA ZA MWENYEZI MUNGU KATIKA MSIMU UJAO WA KILIMO.

  Kama kigogo unadhani sikuzote utaendelea kushiba na wanao,na kuwasomesha shule nzuri na kutibiwa nje ya nchi wakati walipa kodi na watanzania wengine wanasota! kwani Mungu unampikia chai???????

  Yana mwisho haya


  NANYI MTAIFAHAMU HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU
   
 6. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2009
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mkuu Kigogo

  CCM ni chama tawala hivyo kila mtanzania anaathirika na maamuzi yanayotolewa.

  Makamba naona amekuwa kiongozi mzuri wa kuhakikisha anasambaratisha nchi hii kwa kutumia/kukumbatia mafisadi lakini akumbuke kuna siku atatafuta wa kumuokoa na hataweza kumpata.

  Kuna siku mafisadi wenye uraia zaidi ya nchi mbili watamkimbia nayeye atabaki hapa tanzania na kwenda kujenga makazi yake kule Keko na Segerea.

  Kama hasomi alama za nyakati hili haliko mbali na haliwezi kuwa zaidi ya miaka either mitano au kumi.

  Masikini mzee Makamba sijui nini kilimuingia kichwani? Hivi ukiwa kiongozi wa CCM unapoteza akiri gafla? Makamba akiwa mkuu wa mkoa wa DAR ni tofauti kabisa na makamba general Secretary wa CCM. Mzee huyu anatakiwa kuombewa.
   
Loading...