SIKIKA yailipua BUNGE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SIKIKA yailipua BUNGE

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sizinga, Jun 28, 2011.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,924
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Shirikisho lisilo la serikali la kufanya utetezi wa huduma bora za Afya SIKIKA limeponda mkutano wa Bunge la Bajeti liksema lifupishwe badala ya kumalizika August 30. Vikao kwa miezi 3 havina maana yoyote na ni mojawapo ya matumizi mabaya ya fedha za mlipa kodi kwani kwa mwaka jana bubget la Bajeti lilidumu kwa wiki 5 tu ili kuruhusu maandalizi michakato ya Uchaguzi na hadi hivi sasa hatujasikia madhara yatokayo na kupunguzwa kwa muda ule wa Bunge.

  SIKIKA haioni umuhimu wa hii mijadala mirefu baada ya kupitishwa kwa bajeti. Mkutano wa bajeti ni mrefu na sio wamsingi zaidi ya kumaliza fedha za umma. Kwanini wajadili kitu ambacho kimeshapitishwa??Mkurugenzi Irene Kiria alihoji.

  Bajeti ilivyowasilishwa,wabunge waliijadili kwa wiki moja na ikapitishwa juni 21 na kwa mujibu wa katiba,kama bajeti isingepitishwa basi Rais angelivunja Bunge. Aliongeza kuwa mijadala ya wizara itakoyokuwa kwa miezi hiyo 3 haina nguvu ya kuipinga/au kufanya mabadiliko yoyote ya maana katika bajeti ambayo tayari ilishapitishwa na wabunge na Mabadiliko yote ilibidi yafanywe wakati kamati za bunge zilipokutana na serikali.

  So kwa mantiki hiyo wabunge waende nyumbani na wakome kuendelea kutumbua fedha za walipa kodi kwa miezi yote hiyo 3 kwa mijadala isiyo na Tija.
   
 2. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,906
  Likes Received: 5,367
  Trophy Points: 280
  nahisi liendelee walau mwezi mmoja ili htimaye wafute posho
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nadhani kuna umuhimu wa kuangalia logic ya kuwa ni mijadala ya bajeti kwa wizara moja moja wakati ki-ukweli bajeti ya nchi imeshapita. Bajeti aliyosoma Mkullo inajumuisha wizara zote sasa kama sio kupoteza muda wabunge wanaongea nini wakati kimsingi wizara zilishawakilishwa kwenye hotuba ya Mkullo?
   
 4. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,924
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Sasa huoni posho zitaliwa sana ndani ya huo mwezi??
   
 5. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  bunge la makinda hata wasipokaa kabisa ni sawa tu
  hakuna mambo ya kujenga nchi mama anafinya kila hoja ya kizalendo.

  wanasiasa wa tanzania wamezeeka vibaya
   
 6. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Bunge letu limepoteza maana, hasa wabunge wa CCM.

  Leo nilikuwa naangalia bunge niliyoyasikia ni vichekesho, wabunge takribani wote wa CCM wameounga mkono bajeti licha ya kubaini kuwepo kwa matatizo chungu nzima. Mmoja wakati anachangia alisema hataiunga mkono bajeti ya waziri mkuu mpaka waziri mkuu ashughulikie kero kwenye jimbo lake lakini cha ajabu ni kwamba wakati anamaliza akasema anaunga mkono bajeti.

  Halafu hili la amani nani kawaambia wabunge wa CCM kila mmoja aongelee amani? Wanakela kuliko maelezo, wanadhani watanzania hawajui thamani ya amani na wanataka tuchague amani hata kama wanatuibia.... wamenoa!
   
 7. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono hoja ya Sikika hatuhitaji mavuvuzela kama bajeti imepita waende majimboni CASE CLOSED.Tunaweza kuokoa hela nyingi sana hapa.
   
 8. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  bado wanaishi kwenye mfumo wa chama kimoja lakini hawajui wananchi tunawasikiza wasije tafuta mchawi baada ya huu usaliti kwa wananchi na kutumikia chama
   
 9. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Ikulu ivunjwe ili kutanua hospitali ya saratan

  .Sisi wanaharakati wachumia asasi za kiraia tunaitaka serikali iondoe makazi na ofisi ya rais pale magogoni ili kuwezesha eneo hilo kutumika kwa shughuli muhimu za hospitali ya saratani. Uchunguzi tulioufanya tumegundua rais aliyepo madarakani ana nyumba yake binafsi mtaa wa migombani regency na pia amejengewa nyumba na serikali kijijini kwake msoga. Kwakuwa katika hali ya kibinadamu si rahisi kwa binamu kulala nyumba tatu basi ni dhahiri rais wetu anatumia vibaya rasimali za nchi. Tunatambua kuwa hospitali ya saratani imezidiwa na misongamano ya wagonjwa kutokana na ufinyu wa majengo, tunadhani sasa ni busara rais akairudisha ikulu ili itumike kama wodi za kulaza wagonjwa. Tunamtaka rais pia arudi kwenye nyumba yake ya migombani akakae kwani kwa miaka zaidi ya 25 ameishi hapo na hakuwahi kupata tatizo lolote la kiafya hivyo hakuna sababu yeyote itakayo mfanya leo ashindwe kuishi hapo. Pia tunaipa serikali siku 21 ianze kufanyia dhifa za kitaifa katika nyumba iliyo ijenga huko msoga kwani hakuna sababu yoyote kutumia pesa za walipa kodi kujenga nyumba inayotumika kwa shughuli binafsi za familia. Tunawataka pia mabalozi na wawakilishi wa nchi wahisani kuanza kuwakilisha hati zao za uwakilishi nyumbani kwa rais au watumie ofisi yeyote ya wanasheria badala ya kuendelea kutumia ikulu wakati mamia ya wagonjwa wanateseka kwa kulala chini.
  Mwisho tunakemea vikali tabia za matumizi ya hovyo ya rasilimali za umma hasa kwa shughuli za uendeshaji wa serikali wakati raia wote wanaweza kujisaidia wenyewe.

  Imetolewa na NGO njaa.

  Imesainiwa na

  Irene Kiwia.
   
 10. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Bajeti ya kila wiraza ilikwisha jadiliwa na kupitishwa ndani ya kamati zao,pili bajeti ya jumla ya mkulo imepita bila kupingwa.so far hakutakuwa na mabadiliko so bunge likae mwezi mmoja then liishe watu waendelee na maandamano na kuforce utekelezaji wake.nawasilisha.
   
Loading...