Sijui Watanzania Tutaamshwa na nani....?

Thegreatcardina

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2009
Posts
406
Reaction score
182
Watawala wetu wameyaishi maisha yao wakayamaliza kabisa. Wakaamua kuishi maisha ya Kizazi chetu nayo wameyamaliza kabisa. Kwa kuwa bado wapo hai sasa wameanza kuishi maisha ya watoto wetu. Sisi tupo tunawaangalia tu na kulalamika. Kama hatuchukui hatua sasa kwa sanduku la kupigia kura mnafikiri nani atakuja kutuokoa? Watayamaliza na maisha ya watoto wetu waishi maisha ya Wajukuu wetu. Tuambiane sasa hatua za kuchukua. Wakati ndio huu. hakuna wakati mwingine. Tukikosea leo, tumekosea milele.
 
Wewe uko nyuma sana. Madini, ardhi, mbuga na wanyama wake vinayoyoma, mashule na elimu kwa ujumla havina hadhi, mahospitali unaenda tu kufia hapo. Barabara za mabilioni ni vichochoro na rangi ya lami, halafu unasema hawajamaliza hadi kizazi cha nne kijacho. Wewe ni mtanzania kweli? Ni nchi gani duniani ambapo viongozi wanamaliza kabisa mahaspitali then wanafungasha kila leo kwenda kutibiwa ng'ambo kwa gharama za wapiga kura wao? Tusijidangane wajukuu zetu, watoto wao, na majukuu zao hawana kitu hapa Tanzania. CCM na genge lake limeshakomba kila kitu. Ni wapi uliona viongozi wakihonga bodaboda, daladala, malori, nk kuwapeleka watu kwenye mikutano ya hadhara? Ni wapi uliona polisi wakiua waandishi wa habari na raia wasio na hatia kisha serikali isichukue hatua stahiki? Angalia Kamuhanda na wenzake wako wapi? Tunajidanganya sana sisi watanzania. Tumeshawaingiza vizazi vinne vijavyo matatani kwa kuwaruhusu mafisadi kuiongoza nchi. Tunadidimia kama watu wanaozama na vizazi vyao kwenye mafuriko na hawadhubutu kuchukua hatua hali wakijua mauti hayataepukika. Yako wapi hata yale maadili ya kawaida tu kati yetu? Tujikubali, tubadilike na kuchagua viongozi wenye utu.
 
Mkuu umemwelewa vizuri mtoa mada? Ana hoja na mawazo kama yako pia!!
 
Back
Top Bottom