Sijui nieleze ukweli kwa mumewe?

Sijui nieleze ukweli kwa mumewe?

mwenye mke tayari kashaupata ukweli kupitia sredi hii, na kashajua kuwa wewe ni adui yake namba mbili baada ya huo mchepuo Wa mkewe. Hivyo hatokupigia tena simu.
 
Sijui watu huwa wanajiamini vipi kuja hapa kuweka details za jambo husika na kuassume kwamba wahusika hawapo humu. Njemba ilikuja hapa kuandika kuhusu kunyimwa papuchi na mkewe hadi kutoa chozi. Mkewe akamsoma kupitia hili jamvi wakakaa wakayamaliza kiungwana. Watu wawe wanafikiria mara mbili mbili kuweka details za jambo husika humu vinginevyo watakuwa wanamwaga mchele kwenye kuku wengi.

mwenye mke tayari kashaupata ukweli kupitia sredi hii, na kashajua kuwa wewe ni adui yake namba mbili baada ya huo mchepuo Wa mkewe. Hivyo hatokupigia tena simu.
 
umekataliwa unataka kutumia nafasi hiyo kufanikiwa ........ungekuwa na busara ungeshirikiana na mkeo kumkanya huyo shemjio kwa jambo analolifanya......yawezekana ndio mambo wanayofanya na dadake (mkeo) ukiona mwenzako ananyolewa nawe jiandae kutia maji

Jana mke wangu kakesha usiku kucha anamkanya mdogo wake wakigombana mm ndo nilikua muamuzi, sasa zaidi ya hapo tufanye nn?
 
Una uwezo mzuri sana wa "kubaini fursa"
Scratch my back I will scratch yours! mkeo na mdogo wake!
 
Hizi stori zenu zinawakatisha tamaa mabinti ambao hawajaolewa kila siku thread za matatizo ya ndoa tu, shemeji yako alienda Kwa mchepuko Moro na wewe hapo hapo Unataka kutembea naye na wewe una mke.

Ndoa ni majanga.

Cc....
 
Mbona jamaa ameshasoma apa na amejua,mtapata aibu kwa kutetea uongo
 
Wakuu poleni na majukumu
Mdogo Wa mke wangu ameolewa arusha, anaishi huko na mumewe na familia yake

Wiki iliyopita alimuomba ruhusa mumewe kuwa anakuja dar kwa Dada yake yaani kwangu, kwamba Dada yake ni mgonjwa hivyo lazima aje, akaruhusiwa

Cha kushangaza hakua kwangu hiyo wiki nzima in fact kaja Jana, wakati arusha ameondoka wiki nzima iliyopita
Kumbe alienda Moro kwa mchepuko wake amemalizana nao ndo Jana kaja dar
Sasa inaonekana kuna mtu Wa karibu na mumewe kamuona Moro, hivyo
Mume Wa huyu binti ameongea na mke wangu kujua ukweli na ni wazi kwamba hakumuamini mke ktk utetezi

Huyu jamaa mm na yeye huwa haziivi kiviile tunaweza kumaliza mwaka ndo tuonane au kuwasiliane, hujiona matawi ya juu hivyo nikampotezeaga

Tangu Jana jioni wanawasiliana na mke wangu, nawasikia wakizozana sana, sasa wife kamwambia kama haamini mkewe alikua hapo wiki nzima Basi aongee na mimi
Wife anashauri tudanganye tu kuokoa ndoa ya huyu binti ingawa kakosea sana

Sasa wakuu huyu ndugu akinipigia simu niseme uongo kweli? Ni haki hiyo?

Mwaka Jana niliwahi kumuomba huyu binti tufahamiane akakataa, sijui nitumie nafasi hii kufanikiwa hilo jambo?

Lakini pia kama mumewe hatajua jambo hili si huyu binti ataendelea? Tuombe mungu huyu jamaa asiniulize

Tufahamiane?
 
Wazinzi bhana yan story zao hazibadilikagi ,zote huwa na mwisho sawa.
 
ngoja na wewe mkeo akuage kuwa mdogo wake anaumwa anakwenda kumuona arusha halafu unasikia ameonekana mtwara
 
Ni kama watu wamejiegesha katika mwavuli wa ndoa huku wakijifanyia upumbavu wao. Sasa huu nao tuuiteje??
 
Ni bora kunyamaza kuliko kusema uongo...muambie mkeo asilete upuuzi,leo kwa huyo jamaa kesho kwako....wamalizane wenyewe na ikiwezekana mtimue hapo huyo binti arudi kwa mumewe...
 
michepuko ni tatizo katika ndoa nyingi na ni tabia iliyojengeka, hacha kutumia nafasi hiyo kujishushia heshima bali muelimishe shemejio juu ya umuhimu na thamani ya ndoa.
 
Wakuu poleni na majukumu
Mdogo Wa mke wangu ameolewa arusha, anaishi huko na mumewe na familia yake

Wiki iliyopita alimuomba ruhusa mumewe kuwa anakuja dar kwa Dada yake yaani kwangu, kwamba Dada yake ni mgonjwa hivyo lazima aje, akaruhusiwa

Cha kushangaza hakua kwangu hiyo wiki nzima in fact kaja Jana, wakati arusha ameondoka wiki nzima iliyopita
Kumbe alienda Moro kwa mchepuko wake amemalizana nao ndo Jana kaja dar
Sasa inaonekana kuna mtu Wa karibu na mumewe kamuona Moro, hivyo
Mume Wa huyu binti ameongea na mke wangu kujua ukweli na ni wazi kwamba hakumuamini mke ktk utetezi

Huyu jamaa mm na yeye huwa haziivi kiviile tunaweza kumaliza mwaka ndo tuonane au kuwasiliane, hujiona matawi ya juu hivyo nikampotezeaga

Tangu Jana jioni wanawasiliana na mke wangu, nawasikia wakizozana sana, sasa wife kamwambia kama haamini mkewe alikua hapo wiki nzima Basi aongee na mimi
Wife anashauri tudanganye tu kuokoa ndoa ya huyu binti ingawa kakosea sana

Sasa wakuu huyu ndugu akinipigia simu niseme uongo kweli? Ni haki hiyo?

Mwaka Jana niliwahi kumuomba huyu binti tufahamiane akakataa, sijui nitumie nafasi hii kufanikiwa hilo jambo?

Lakini pia kama mumewe hatajua jambo hili si huyu binti ataendelea? Tuombe mungu huyu jamaa asiniulize

Asee we jamaa unataka kutumia iyo chance kugegeda na wew? ?
 
Back
Top Bottom