Sijui mtego huu?

Sijui mtego huu?

matamba1

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2015
Posts
233
Reaction score
84
Jumapili iliyopita niliamua kumtoa out mpenzi wangu katika moja ya hotel zile za wenye nazo, nikamjulisha akaniuliza naweza kuja na rafiki yangu? Nikamuuliza yupi, maana kuna mmoja hata huwa simuelewielwewi.

Bahati nzuri hakumtaja huyo, akasema mimi simjui nikamwambia aje nae tu. Kweli wakaja. Uongo mbaya, wangu alipendeza lakini hakumpita rafiki yake. Zikapita salamu mbili tatu na utambulisho wa juu juu zikaja stori za hapa na pale ukiongeza na mvinyo wa kwenye hizi hotel ambao majina yake magumu sana kuyashika.

My love akaja na stori ya hivi utakuja kunisaliti kweli? Majibu niliyompa hata itokee nini siwezi nikajiapisha na miungu yangu yote pale. Sasa jana na mvua ile niko kwenye foleni bampa tu bampa mbele yangu kuna mak x ile natanua nikaikwangua ikabidi niwe mstarabu nikasimama kwenda kuomba msamaa nikagonga kioo kikashushwa kutaamaki ni yule rafiki wa mchumba wangu akaniambia usijali shemu wangu twende pale tuongee (pembeni pana pub moja maarufu) tukavuta kiti akaAnza kwa mbwebwe za jeuri shemu agiza kinywaji nikaagiza. Akanikazia macho na kuanza kunipa maelezo.

Najua umeharibu gari yangu, umevunja taa. Sitaki ununue ila nataka uwe mpenzi wangu. Yalinitoka macho nikaropoka, we si unajua nina mchumba wangu ambae ni rafiki yako akijua!? Akajibu kwa jeuri "utamwambia wewe" kama hutak,i lipa. Nikipiga hesabu na hela saivi ilivyonipiga chenga taa ya mark x na fundi rangi lazima 1 mil vinitoke nikamwambia aniache nikajifikirie, akasema kesho yaani leo anataka jibu na saivi kanipigia na kuniambia nimkute hotel flani. Sasa kinachoniuma ni usaliti kwa mpenzi wangu afu niliapa sitamsaliti mbele ya huyo huyo anaetaka nikamsaliti
na kiuchumi saivi siko vizuri sana. Au mtego? Yaani ananivuruga huyu mdada.

Nipeni ushauri,

Nawasilisha kwenu wanaJF.
 
mkuu kula mzigo huo usiache aiseee

Dhambi ya usaliti ni mbaya sana mkuu,... Hata wale wa CHADEMA wanajua. Ila hofu nyingine nahisi mpenzi wangu atakuwa kamfanya rafiki yake awe shushushu... Nikikumbuka swali la Jumapili alivyouliza utanisaliti? Aliuliza ghafla afu kama ana agenda ya siri hivi.
 
Back
Top Bottom