Sijui kwanini nimeumia hivi

Pole ndo ukubwa huo mi siku hizi nimekuwa na roho mbaya baada ya kupigwa vitu vizito huko nyuma yani shida za mtu wa karibu sijui ndg au nani nani hazinigusi kabisaaa ndo ije kuwa classmate,
Yaani, ila kwa namna aliyoniambia sidhani kama ungeweza kukataa mkuu, na alikua ananiambia huku namuona mtoto alivyo.. Ingekua kwenye simu nahisi ningekataa kwa jinsi ambayo nilikua sina hela
 
Yaani nashindwa kueleza ninavyojiskia,, sihitaji anilipe chochote wala chochote ila tu nimeumia ndomana najishangaa kwanini inakua hivi hadi nashindwa kujizuia.. Hata sielewi naumia nini yani
Hahaa nafikiri umejisikia sehemu ndogo ya maumivu ambayo wanaume tunajisikia kwenye swala la mapenzi, tukiwa tuna-deal na wanawake kwenye maswala ya hela Leejay49
 
Pole sana,binadamu ndivyo tulivyo na kheri umetenda wema ila hayo maumivu ni kuwa hujapata "ahsante ya mchango wako kwake"

Jitahidi kusahau ila haitokuwa rahisi,siku atakayokutafuta wabongo wanasema "MCHANE UKWELI"

Hakikisha unaongea kweli kweli hadi mishipa ya shingo ukusimame maana si dhambi kumfunza mtu kutoa ahsante ikiwa umetoa kwa moyo mweupe na maumivu yanakuja sababu ya dharau kutotambua mchango wako.
Na mimi nasema "MCHANE" hata ukikutana naye mtaani/akikutafuta.

Hope you have a good one....
 
Back
Top Bottom