HI,
HABARI ZENU,NINA MDOGO WANGU(BINAMU) namchukia toka kipindi ambacho nipo ndani ya ndoa sababu ni hivi,
Nilioa mke, na yeye(dada yangu) aliolewa na mtu tajiri na kila mara akawa anamtambia mke wangu ,na mawifi wengine kwenye vitu mbali mbali vya kununua nunua (simu,kubadili gari,swiming pool ya kununua, na mambo kedekede kila kukicha) mke wangu akawa ananiendesha ile mbaya kwamba mimi simpendi /sijui ku care,mara hv mara vile mwishowe demand ya vitu na vijimigorogoro vikawa vingi na mimi sijaishi kwenye maisha ya kutatua /kusuruhisha/kushtakiwa /kulaumiwa/au kulaumu/kusingiziwa mabaya/au kutenda mabaya katika ujana wangu wote tuliachana na mke wangu,
shida nliyonayo yule dada angu kila leo anapost vitu vizuri vizuri kwenye group moja la whatsaap la familia na mimi nakumbuka vile vijigogoro vilivyopita na aliyekuwa mke wangu. sasa sijui yangu ya kumchukia kwa tabia yake hii mimi itaniisha lini maana dogo anakimbiza mpaka mawifi zake wengi kinawauma.