Sijui itakuaje kama hawa wachezaji hawatacheza...

mafoleni

JF-Expert Member
Nov 18, 2016
220
371
TFF yawaondoa wachezaji wa Simba ndani ya ‘Taifa Stars’, viongozi wao kupelekwa kwa pilato
 702
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limewaengua katika kikosi cha timu ya taifa ‘Taifa Stars’ wachezaji sita wa timu ya Simba kutokana na kuchelewa kuripoti kambini kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na kocha, Emmanuel Amunike.
Katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidao
Nyota hao walitakiwa kuripoti kambini jana usiku huku wakiwa wamepewa taarifa wakati Aishi Manula pekee ndiye aliyeripoti.
Katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidao amewaambia waandishi wa habari kuwa kocha Amunike amekasirishwa na kitendo hicho na kuamua kuchukua maamuzi hayo amabayo Shirikisho hilo chini ya Rais Wallace Karia wamelipitisha.
“Wachezaji wote wa Simba walioitwa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ isipokuwa Aishi Manula wameenguliwa katika kikosi kinachojiandaa na mchezo wa kufuzu dhidi ya Uganda kutokana na kutoripoti kambini kwa muda uliopangwa,” Wilfred Kidao Katibu Mkuu TFF.
Kidao ameongeza kuwa TFF iliamua kusogeza mbele mechi za Simba, Azam na Yanga zilipokuwa zichezwe Septemba mosi na pili ili kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Afrika dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ utakaofanyika Septemba 8 jijini Kampala. “TFF imewaengua wachezaji sita wa Simba kwenye kikosi cha timu ya taifa kutokana na kuchelewa kuripoti kambini licha ya kupewa taarifa mapema,” alisema Kidao.
Wachezaji hao ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, John Bocco na Shiza Kichuya.
Mbali na wachezaji hao viongozi wa Simba, Hamisi Kisiwa na meneja Richard Robert watapelekwa katika kamati ya maadili ya TFF siku ya Jumamosi ili kuchukuliwa hatua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na kwamba itakuwa pengo ila Discipline ni kitu muhimu kwa Professional yoyote.

Ni either uripoti mda uliotakiwa, au uombe ruhusa na ukubaliwe au ukataliwe. Discipline.

Bila Discipline hakuna mafanikio au maendeleo katika Profession yoyote.

Discipline, nakazia, Discipline.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na descipline ndio inawakosesha wachezaji wa tz kucheza mpira kimataifa, watazeekea humuhumu nyumbani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lazima utazame mazingira,wote hao hawawezi kukosa nidhamu
Mzee hata mimi ni Simba damu damu. Ila unatakiwa ujiulize je imekuwaje Manula akaweza kufika kwa wakati hao wengine washindwe?

Kuna uzembe kwa hao wachezaji husika. Ingekuwa wote wa Simba hawakufika hata mmoja basi nisingekimbilia ku judge kuwa wana lack discipline.

Kama walikuwa na dharura wangetoa taarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukwel timu ikifungwa atawatambua Watanzania' kwa sababu Hao wachezaji kutokuwepo kundini ni pengo kubwa' NAMBA 6 ATACHEZA NAN?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tanzania nzima 6 ina mchezaji mmoja tu? Mama yangu tumekwisha! Hivyo kumbe alitakiwa aje hata siku moja kabla ya mechi sio mbaya maana ni muhimu sana huyo, baada ya kufungwa tutapata tiba huu upuuzi wa kwamba Fulani Ni muhimu ufe kabisa, tumpe muda akizoea atapata namba sita nyingi tu. Naomba Mungu tushinde ili hao muhimu waweze kujitathmini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom