Mahunguchila
Member
- Jun 11, 2012
- 74
- 34
Hii ni story ya kweli ambayo imenitokea mimi personally.
Mwaka jana mwanzoni, mwezi wa 2 au 3 hivi nilikutana na baba mmoja mtu wa makamo hivi. Kiumri anaweza kuwa sawa na baba yangu mdogo (last born kwao baba) kama 49-50s hivi. Nilikutana nae pale Sokoine drive karibu na New AFrica Hotel.
Wakati tunakaribiana alitoa tabasam fulani hivi, na kwa kuwa mimi simfahamu nilimsalimia 'shikamoo' nikitegemea atanijibu marahaba. Ajabu akaniambia' nakuhitaji'! Ni kama sikumsikia vizuri vile, nikasimama kumshangaa ila yeye akaendelea na safari tena bila hata kugeuka. Nikafikiri kwa haraka haraka nikadhani atakuwa hayupo sawa (kichaa)lakini nikashangaa mbona msafi?? Nikaachana nae.
Mara ya pili nikakutana nae maeneo yale yale kama baada ya mwezi na wiki hivi. Wakati anakuja kwa mbali nikawaza, ebu ngoja nione kama ataniongelesha, nikamkazia macho na aliponikaribia akasema tena 'nakuhitaji'! Nilishangaa kwa kweli ila nikapotezea tu.
Tokea hapo nikawa naonana nae mara kibao na kila nikimuona ananiambia the same words! Nilitatizika sana. Kuna siku nilikuwa na rafiki tangu (mdada) nilipomuona kwa mbali nikamwambia atangulie mbele nione kama atamwambia hayo maneno ajabu hakumsemesha ila mimi akaniambia 'nakuhitaji'!
Kweli nilikosa amani sana na nikawa nikimuona anakuja natamani akinisemesha nimuulize kwa nini huwa ananiambia yale maneno ila kila nikimsimamisha alikuwa hanijibu wala hageuki. Mara ya mwisho nikakutana nae posta mpya akiwa anaongea na rasta man mmoja ivi anaumza miwani, nikapita karibu yao maana ni njiani na yule baba akasema vile vile then akaondoka.
Nikamuuliza yule muuza miwani kama anamfahamu akaniambia eti yule ni mtu mkubwa sana apa nchini!! Sasa hapo jirani alikuwepo mama mmoja hivi akataka kujua kwa nini namuulizia yule baba. Nikampa story kwa ufupi basi yule mama akasema kama wewe ni Mkristu kemea sana na uombe humu mjini kuna mapepo/majini mengi yanatembea kama watu. Hapo ndipo nilipofunguka akili yangu kwa mara ya kwanza.
Nilimshirikisha Mungu na kuomba sana, nakumbuka ilikuwa kama mwezi wa 8 au 9 hivi! Tokea hapo sijawahi kumuona yule mtu hadi leo!! Huwa najiuliza kama kweli yule ni mtu au!!!