Sijawahi kujihusisha na uchawi, Je! naweza kulogeka?

IPO hivi umeme hauwezipenya kwenye kizuizi mfano plastics au Mbao ,lzm kuwe na kiunganishi( hofu,woga,kutenda dhuluma nk maouvu yote).uchawi upo uamini usiamini lkn ili ukudhuru ni lazima uwe na connection yaani kwanza ni lazima uwe na uoga au hofu ya kuamini katika kurogwa,huwezi logeka km hauamini ktk ulozi,hakuna MTU mwenye uwezo wa kumloga MTU isipokuwa anaerogwa lazima aamini ya kuwa anaweza logwa au anaejihusisha na mambo ya kishirikina kuwa mchawi au kwenda Kwa waganga au kujihusisha na mambo ya madawa pale unakuwa umeweka connection, yaani kuruhusu wwe kuunganika na nguvu hasi unaziruhusu mwenyewe kujidhuru,ndo maana mchawi usumbua waoga akiingia ndani ukaogopa akutishapo ndo Furaha yake, lkn akiingia ukawa unamuangalia tu unamuacha afanye yake hawezi rudi tena,kinga ya uchawi ni kushikamana na imani yako ya dini,au kuyapuuzia kutoyaamini mambo ya kishirikina unaishi Kwa amani.Mifano hai wengine tumerogwa tangu hatujazaliwa had leo tunarogwa lkn mambo yetu yanatunyookea ni Kwa sababu atuamini hayo.Cha kukusaidia tafuta Vitabu au elimu za nguvu za asili uone zitendavo Kazi .power of positive thinking. Ungekuwa na nguvu ungeweza kuwasaidia waafrica wasichukuliwe utumwani au kutawaliwa na wakoloni ,lkn hawakurogeka sababu wale hawakuamini ktk uchawi.
Umetoa maelezo marefu kama gazet la siasa lakin sijaona point...Mtoto mdogo asieujua uchawi hawezi kuwa na hofu ya kulogwa lakin mbona wanalogwa
 
haukusikia wale walimu wakike shinyanga kila wanapoamka asubuhi wanakuta mbegu za kiume ukeni
 
Umetoa maelezo marefu kama gazet la siasa lakin sijaona point...Mtoto mdogo asieujua uchawi hawezi kuwa na hofu ya kulogwa lakin mbona wanalogwa
Ndio analogeka kupitia udhaifu wa nafsi ya wazazi wake Kwa hio wazazi ndo huwa connection km ujuavo uchawi hauwezipita Kwa MTU lazima kuwe na connection ya imani ya kurogeka.Ndo maana nilikupa mfano wachawi wangekuwa na nguvu ya kuroga wasioamini wangeweza kuwaroga wakoloni wakadhurulika lakini hawakurogeka sababu uchawi aupiti Kwa asiyeuamini,we unalogeka sababu tayari unahofu ambayo misingi yake ilipandikizwa kwako kupitia mazingira uliyokulia au unayoishi,sababu uchawi ustawi zaid penye ufinyu mdogo wa elimu na hofu
 
Ndio analogeka kupitia udhaifu wa nafsi ya wazazi wake Kwa hio wazazi ndo huwa connection km ujuavo uchawi hauwezipita Kwa MTU lazima kuwe na connection ya imani ya kurogeka.Ndo maana nilikupa mfano wachawi wangekuwa na nguvu ya kuroga wasioamini wangeweza kuwaroga wakoloni wakadhurulika lakini hawakurogeka sababu uchawi aupiti Kwa asiyeuamini,we unalogeka sababu tayari unahofu ambayo misingi yake ilipandikizwa kwako kupitia mazingira uliyokulia au unayoishi,sababu uchawi ustawi zaid penye ufinyu mdogo wa elimu na hofu
Sio kweli watu wakiamua kukushughulikia wanakushughulikia vyema tu hayo mambo ya hofu ukiona hivyo we ushajikinga kwa njia nyingine
 
Me naelewa nguvu za asili zifanyavyo Kazi wala sihitaji mganga au mchungaji.Kinga kubwa ya wachawi ni kusimama binafsi kiimani,nasema hivo sababu tumerogwa tangu hatujazaliwa na tunaendelea kulogwa na mambo yanaenda vizuri tu kielimu,kiuchumi karibia kila kitu,sababu siamini katika nguvu hasi. Ungekuwa unauelewa kuhusu power of nature tungeweza elewana.Uwezilogeka hadi kuwe na chanzo au connection ya nguvu hasi yaani uchawi uweze kupenya kwenye mfumo wako yaani kuhurusu.
 
Wakuu heshima mbele,

Nakuombeni mnisaidie sana ktk jambo hili. Mimi ninaumri wa wastani tu japo unatosha(ni kijana). Mpaka sasa, sijawahi kwenda kwa mganga kutafuta uchawi wa kujiganga, sina chale hata moja(labda ya kujikwaruza mahali tu, sio ya uganga),wala sina destiny au interest kabisa na mambo ya uchawi mpaka sasa.

Ninaimani yakutosha ktk dini & Mungu wangu. Pia, nimewahi sikia kuwa, wachawi au uchawi/urozi humdhuru yule ambaye kwa namna moja au nyingine naye anajishughulisha na mambo ya kiganga au amewahi kuwatembelea kina Sangoma walau!

Sijawahi fanya hivyo na sina chochote cha kiganga/kishirikina nafsini au mwilini mwangu.

Sasa je! MCHAWI ANAWEZA KUNIDHURU AU KUNIROGA? (mfano kuniwangia au kuniua).

Msaada tafadhari wanaJamvi.
Dawa huwa inapambana na dawa nyenzake. Kama huna dawa yoyote, hutendi dhambi, unaenda Kanisani kwa kumaanisha na kwa moyo wa dhati kabisa, unampenda Mungu (watu), hakipo kitu kinachoweza kukudhuru kutokana na uchawi. Wewe kupata madhara inabidi mpaka Mungu aridhie, hawezi kuridhia kama wewe una sifa hizo. Kitachotokea ni kwamba wewe ndiyo utakuwa unaonekana mchawi zaidi kwa hao wanojaribu kufanya ujinga wao kwako.

The fact is, mchawi anatumia TEKINIKI zile zile ambazo Mungu huwa anatumia katika kuwasaidia watu wake, isipokuwa Sheteni yeye alishaongeza uharibifu katika mbinu hizo. Kumbuka shetani alikuwa malaika mkuu mbinguni, hivyo ana ufahamu mkubwa (knowledge) inayotokana na Mungu isipokuwa yeye sasa aliamua kuongeza uharibifu katika ufahamu huo. Ni kama kwa mfano, umfundishe mtoto wako kupika ugali kwa ajili ya watu nyumbani, halafu akakuasi akawa akipika huo ugali, anachangaya sumu kwenye unga. Hicho ndicho hasa shetani anafanya. Anatumia knowledge ya Mungu hiyo hiyo aliyoipata wakati akiwa malaika mkuu, kwa ajili ya kutenda uharibifu.

Ukiwa ndani ya Yesu, kwanza: mwili wako unakuwa ni hekalu la Kristo, pili: unakuwa kiungo katika mwili wa Kristo (maana yake ni kwamba mchawi kukushambulia wewe anashambulia kiungo cha mwili wa Kristo, aliyemuumba,......, kesi mbaya kuliko hata pre-meditated self murder), tatu: wewe unakuwa mzaliwa wa pili baada ya Kristo (Yaani Yesu anakuwa ni kaka yako aliyezaliwa kwanza halafu wewe ukafuata baada ya yeye kuwa amezaliwa-Soma the Doctrine of Adoption). Sasa katika hali hii, tulia uache wakuchokonoe halafu UONE WATANAVYOPIGWA! Yaani ni uhakika wala siyo stori!

Kama uko hivi kweli kama unavyosema, ningekushaui uwe mlokole, mimi ni mlokole, na inaonyesha tumefanana sana. Wakati bado sijaokoka, kuna mtu alikuja nyumbani kwangu akasema maneno haya huwa siyasahau "HALAFU WEWE KAMA UKIOKOKA"! Baada ya kuokoka Roho Mtakatifu akaja akanishuhudia kuwa huyu mtu amekuwa akinitafuta miaka mingi nyuma pamoja na wenzake wengi tu lakini hawakuweza. Kilichokuwa kinawashangaza ni kwamba kwa nini wanshindwa wakati kwa waganga wa kienyeji sijawahi kukanyaga mguu, sina dawa yoyote na kanisani kipindi hicho ilikuwa ni kwa mama mkwe! Una chance nzuri sana ya kuwa na mahusiano na Mungu ambayo ni watu wachache sana duniani wanabahatika kuwa nayo. Wewe ukimtafuta kwa mfano, Mwalimu Mwakasege anaweza akakusaidia sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom