Je! Kama mtu hana CHALE na yu safi, anaweza akarogwa?

TuntemekeSanga

JF-Expert Member
Jan 15, 2015
1,346
861
Wakuu, heshima mbele.

Ninaimani kubwa katika jukwaa hili (hususan watu wanaoshiriki mijadal humu ndani).

Mimi sina Chale wala sijawahi kwenda kwa mganga yeyote kutafuta uchawi wala kujiganga kwa namna yoyote. Kiufupi, sina interests wala passion yoyote juu ya mambo haya ya kishirikina mpaka sasa.

SWALI LANGU: Je; wachawi wanaweza wakaniroga? maana huwa naambiwa kuwa,wachawi huenda kudhuru wale ambao wanaona kuna baadhi ya vitu vinavyoendana na mambo hayo miilini mwao.

Nimewahi kutembea na ndugu zangu wawili kijijini kwetu wakati wa usiku wa manane, (wao wamekwisha chanjwa vitu kadhaa hususan mambi ya biashara).

Tulipofika pahala fulani, wote wawili walisimama kimya kwa muda hivi. Mimi nikaendelea na porojo zangu nikitembea na kuwauliza kulikoni(tulikuwa tumepata kidogo!). After several minutes,walianza ku'move nakunieleza "we, hujaona hicho kitu kilichokuwa kinapita?" .Nikawajibu hapana kwani ndio ulikuwa ukweli wangu.

Wakasema "basi tulia, wewe bado mtoto mdogo" (huku wakiwa na hofu sana.

Nikajipa moyo kuwa, basi mchawi hawezi kunigusa.

Naombeni sasa jibu la swali langu la msingi pale juu.

ASANTENI.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom