Sijawahi kuishi kinyonge (bila madeni) tangu 2013

Sijawahi kuishi kinyonge (bila madeni) tangu 2013

Udochi

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
1,077
Reaction score
1,581
Tangu nianze job, kuanzia benki, vikundi, dukani, na kwa wana.
Baada ya hapo nikahamia microfinance, huko kwa kuwa hakuna kipengele cha kuzingatia kuwa ibaki 1/3 ya mshahara, ndo najilipua muda wowote.

Yaani akaunti yangu haijawahi kukaa kinyonge, bila deni. Imefikia hatua sasa nikiwa na madeni matatu najiona niko free sana, lazima nivute mikopo hata ya miezi 6 tu ili akili ichakate data.

Kwa sasa kausha damu zimenizoea kiasi kwamba nikichelewesha siku kadhaa, inabidi tu waelewe.
Nikimsikia mtu ana mkopo mmoja, halafu analalamika, namshangaa sana. Kimoyomoyo namwambia ''ukipewa mikopo yangu unazimia kenge wewe.''
 
😂😂

Mimi nafikri JF nzima ina hitaji msaada
Screenshot_20250826-163938.png
 
Unajisifia mikopo mibovu hii ya mtaani wanabeba sijui TV,makochi na Pasi ?

Kuna jamaa wa kimara nadhani mkewe alikopa kaisha damu, walimpiga wakaua !
 
Hiyo sio nzuri, ni kama inaakisi huwezi jisimamia mpaka usimamiwe, yaani bila kudaiwa akili haifanyi kazi ipasavyo mpaka ipate shinikizo la madeni, bila deni hufanyi kazi kwa ufanisi
 
Issue siyo mikopo, bali unakopa ili ufanyie nini na hiyo pesa ya mkopo
 
Back
Top Bottom