Sifahamu mimi ni nani

pharaoh_2

Senior Member
Joined
Jun 25, 2015
Posts
143
Reaction score
123
Habari za leo wana forum,

Mimi ni kijana at late 20's toka nimezaliwa mwanzoni mwa miaka ya 90 nilikuwa nafahamu kuwa baba na mama yangu ndio hawa waliokua wakinilea lakini mwaka 2015 wakati nimemaliza chuo na kurudi nyumbani niliipata taarifa ambayo ilibadili mtazamo wangu kuhusu hawa wazazi wangu na siri kubwa waliyo nayo.

Iko hivi kwa mama yetu mzazi tuko watoto wa nne, mimi ni wa pili kuzaliwa kuna wa kwanza wa kiume na wadogo zetu wawili wa kike na kiume ambao sina shaka juu ya uhalisia wao kwa kua wamezaliwa nikiwa na akili timamu.

Baba yetu tunae mfahamu ni askari wa jeshi la wananchi na mama yetu kipindi hicho alikua ni mwalimu wa shule ya msingi. Kusema ukweli mzee huyu ametulea ki- dictator mpaka inafikia stage unamuogopa and you cannot make story with him or express yourself to him as your father lakini tukazoea na kuona labda tunalelewa kijeshi and by then we lived in a military Barack.

But the good thing about the oldman ni kwamba amekuwa na moyo wa kujitolea kuhusu maisha yetu like taking us all to the most expensive school in town and supplying all our basic needs abundantly, inshort he is Generous nadhani hii ndio sababu iliyotuaminisha kua he is our biological father kwa kua mpaka ada ya kulipia chuo kikuu amenilipia bila kua na mkopo kutoka HESLB.

Sasa wakati nimemaliza chuo nilirudi kijijini kumsalimia bibi (mama wa mama) huko nilikutana na mzee mmoja ambae alinitambua kwa jina la asili ambalo sikuwahi kulijua kabla nilishangazwa na lile jina nikaamua kumuuliza yule babu vipi mbona tunaitana majina ya ajabu.

Mzee akaniuliza kwani wewe unaitwa nani nikamtajia jina langu kwa kudhani kua amenifananisha, akasema "nakufahamu tokea ukiwa mtoto wa umri wa siku moja" yaani kabla mama yetu hajaolewa na huyu mzee tunaemuita baba, honestly he ruined my day and i almost slapped him on his face but thank God i managed to conceal my true feelings.

Nikamwambia mzee kabla sijaondoka nitakuja nikuone tuongee vizuri. Hata sikutamani tena kukaa kwa yule bibi yetu muda wote nilikua nafikiria maneno ya yule mzee baada ya siku 3 niliamua nimuage bibi and i went straight to the oldman's house.

Yule mzee alinieleza kwa masharti kua nimekua mtu mzima nahitaji kujitambua mimi ni nani, na asingeweza kuniambia hizo taarifa wakati wa kipindi cha nyuma labda nisingeweza kumuheshimu huyu mzee wetu ukizingatia anatusaidia kwa mambo makubwa ambayo mama yetu as a single parent asingeweza ku afford like taking us all to international schools.

Nikamuuliza mzee vipi kuhusu hili jina ninalotumia? Akanieleza kua baba yetu (sisi watoto wawili wa kwanza) alikuwa ni dereva wa magari makubwa alikua akija pale nyumbani kwa msimu na hakua akituhudumia.

Sasa huyu askari alipohamishiwa kwenye mji ule kikazi ndipo akakutana na mama yetu akiwa na watoto wawili (mimi na kaka yangu) akafanya kutu adopt na kutubadilishia majina yetu na kuanza kutumia majina ya ukoo wake, kuna muda baba yetu alikuja pale nyumbani alipata kichapo akaenda mahakamani akashindwa kesi kua hana mchango kwa familia kwa hiyo akatoweka mpaka Leo, mimi mpaka sasa hivi sijijui kua ni nani.

Nikimaanisha kabila wala ukoo, ndugu zangu wote hawajagundua hili and we all live like brothers, namuheshimu sana huyu mzee na amefanya kila kitu kuhakikisha tunasoma ili tujitegemee kiasi kwamba nilivyomaliza tu chuo akanitafutia nafasi jeshini moja kwa moja and to be honest I was just glad.

Naomba mnishauri hapa kwa kua niliamua kumkabili mama anieleze ukweli kwa njia ya kumdadisi kwa kua sifanani na mama wala na baba huyu tofauti na wadogo zetu. Lakini mama amekua mkali kua namkosea heshima maswali hayo ni ya kumvua nguo na nimekosa nini kwa baba huyu mpaka kuulizia mtu nisiye mfahamu wala asiyenisaidia lolote.

Yuko sahihi lakini mimi natumia majina ya kichaga ambayo kiuhalisia nimepewa tu hayana mahusiano na mizizi yangu mie and what disturbs me the most ni wanangu, hawa wanangu watakua kabila gani? Si nitakua nimewapa kabila ambalo sio lao? Na wajukuu zangu pia?

Naombeni ushauri this is killing me inside whenever it comes to my mind because I'M A STRANGER TO MYSELF

Regards

Pharaoh_2
 
Wewe ni wewe, majina unapewa tu, hayana maana.

Kama kweli una elim ya chuo kikuu alafu unamfuata Mama yako akujibu maswali ambayo sidhan majibu yake yanaweza kuwa msaada kwako basi naona hiyo elim haikukusaidia.

Tuliza boli, fanya maisha.

Sent from my MI 5s Plus using JamiiForums mobile app
 
Mmmh touching, ngoja wakubwa waje watoe maneno yao ya busara....
Ila suala la kujijua ww ni nani ni muhimu sana ongea na bibi yako na yeye umsikie atakwambiaje.

Culture Gal.
 
Nikwambie kitu bro? Baba yako ni huyo aliyekuhudumia na kukusaidia hadi sasa unajitambua. Acha kabisa kumuwaza huyo mwanaume mwingine aliyekuona wewe huna thamani. Endelea na maisha hapo hapo ulipoishia usirudi nyuma asilani!

Baba yako ni aliyekutunza kwenye shida na raha, ubaba ni zaidi ya 'kumkojoa' mtu sorry to say...........
 
Daaah pole sana mkuu...vipi ukijaribu kumuuliza huyo mzee Baba yako alikuwa kabila gani??
Lakini naamini Mama yako ana siri kubwa ameificha
The oldman doesn't have any detail about our father he just told me about his career

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Wewe ni Mwana JF usiyejitambua.
Find the truth And it will set you free
It's okay you are still entitled to your opinions, i don't blame you anymore

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Asante ndugu

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Ndugu, piga magoti tubu kwa dhambi ya kumkana baba mwenye upendo aliyekupa kila kitu cha kidunia na kiroho kadri ya uwezo wake. Baada ya sala ya toba nenda katoe shukrani. Sadaka yako peleka kwa watoto yatima, watoto wasio fahamu walikotoka wala kesho yao hawajui itakuwaje.

Kama bado utaona kuwapa watoto wako kabila lisilo lao ni issue ya kuumiza akili ilihali wewe umeishi bila shida hadi ukawa na uwezo wa kutunga mimba njoo hapa nitakuambia cha kufanya.

Sent from my E5306 using JamiiForums mobile app
 
wewe bado unawaza kuhusu ukoo ukoo

ukoo hauna faida yeyote maishani mwako

baba yako ni huyo aliyekuwepo na wewe hadi unapata akili
Sure! But i just needed atleast to know my tribe for the sake of an identity, i just thought knowing oneself matters, isn't it?

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Hapana nadhani hujanielewa i respect him as my father lakini kama kutaka kujua mimi ni nani at a first place ni makosa then God the almighty will forgive me, you just got me wrong i guess

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
utakuwa mpumBavu

Sent from my HUAWEI VNS-L21 using JamiiForums mobile app
Ntakua mpumbavu kwa lipi, hv kutaka kujitambua wewe ni nani ni upumbavu? You just can't be serious, right?

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Basi baki na huyohuyo aliyekulea
Sijasema kua simuhitaji huyu mlezi, i'll have to be a devil to say that, but thank you for your cents on this one

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Naamini mama yako aliangalia na fursa ya watoto wake ili msije kuwa na maisha ya tabu katika hatua hii uliyofikia sasa hivi. Nakuhakikishia laiti kama huyu malaika mzee mkuda asingewashukia wewe , mama yako na huyo kaka yako sasa hivi huenda mingekuwa mnahesabika kati ya wale watu wanaoishi katika mazingira magumu.

Au mngekuwa eidha wasaidizi wa biological father kwenye kazi zake za udereva huko au mngekuwa gereji mnajifunza ufundi ili muweze kujihudumia katika maisha yenu ya kujitegemea.

Ila kiuhalisia huyo mzazi unayehisi ndio damu yako hana umuhimu wowote hata ukimjua as long as baba aliyehakikisha katika maisha yako ya baadae unakuwa na good status yupo na bado anawapa ushauri where unapo hitaji.

Usitafute kuchimbua mambo ambayo yatakupa ukweli mchungu katika maisha yako ,ishi kwa amani na puuza hizo rumors alizokupa huyo kibabu wa huko kijijini kwa bibi yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…