Sifa za wanawake

Sifa za wanawake

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Posts
15,271
Reaction score
29,934
SIFA ZA MWANAMKE

Mwanamke kabla hajaolewa huutunza usichana wake kwani ndio taji peke la heshima pale aolewapo.

Ikitokea aliuharibu usichana wake basi hujutia na kutorudia kitendo kile kama mazoea kwake na huwa bora zaidi akijutia.

Mwanamke huanza kujifunza kwao maisha kwani kwa mume huwa ni mechi lakini mazoezi yote mke hufanyia nyumbani mfano mapishi, usafi, tabia nzuri.

Mwanamke mwema huwa mnyonge na hawezi shindana kwani sifa ya mwanamke ni utulivu sio ukorofi kama walivyo simba jike porini.

Mwanamke anaejielewa hutumia upole kuwa ndio ngao yake kwani hakuna mwanaume anaeweza kushindana na mwanamke mpole asiejali mambo mabaya anayoletewa habari kuwa mumewe kafanya kile nje mwisho mwanaume hujishusha kwa upole wa mkewe.

Mwanamke hodari haambiwi kazi za kufanya na mumewe bali mume humpa pongezi kwa kuona mazuri ndani usafi ni jambo la msingi kabisa ndani.

Mwanamke hutambua hali ya uchumi ya mumewe na humshauri katika maendeleo na humuhurumia mumewe hata kama kuna siku karudi hakupata.

Mwanamke anaejielewa humpokea mumewe katika furaha na huzuni hata kama aliokuja nayo mumewe ni masuala ya wazazi wa mume.

Mwanamke huwajali wazazi pande zote mbili wengine hutumia ujanja wakawapenda zaidi wazazi wa mume.

Mwanamke sio kujipikilisha anatakiwa kutambua kuwa hilo hatolikwepa kama kifo kupika ukiolewa na jukumu la kusaidiana ambalo mke ni vizuri kujiweka vizuri katika idara ya kumpikia mume vizuri hata kama masikini na hali yao ya kimaisha lakini hupika kikaiva.

Mwanamke humkumbusha mumewe katika amri za MUNGU licha ya magumu mume anayopitia mke hatolifurahia lakini hujitahidi katika kumuamrisha mumewe katika Sala na mambo ya kheri.

Mwanamke huwa hatoki ovyo ovyo nyumbani kutoka kwake ni kama dharura iliomlazimu au anasaidiana na mumewe katika kutafuta.

Mwisho ukitaka huyu mwanamke awe hivi basi wewe mwanaume muhudumie mwanamke kwa ulichojaaliwa na mridhishe atakavyo kimwili wala usiwe bahili katika hili.

Acha kunanufaisha vimada wa nje kimwili na kiuchumi utaacha watoto wenye wa rande rande mitaani

@ Ambiele
 
Mwanamke anaejielewa hutumia upole kuwa ndio ngao yake kwani hakuna mwanaume anaeweza kushindana na mwanamke mpole asiejali mambo mabaya anayoletewa habari kuwa mumewe kafanya kile nje mwisho mwanaume hujishusha kwa upole wa mkewe.
siku hizi hii sifa hawana ndo mana wanakula vibao sana.
 
Yaani bado tu unafikra za miaka 47 nyuma ebooo .... sikuhiz kuna sifa nyingine mkuu
 
Tusiseme Hakuna kabisa jaman

Mbona Jf Mi nawaona wapo tuu ila ni Baadhi yao
 
Wapo tatizo mnawatafuta baa,kwenye daladala nkmke mwema anapatikana kwenye nyumba za ibada kwani wana hofu ya Mungu.
 
Wapo tatizo mnawatafuta baa,kwenye daladala nkmke mwema anapatikana kwenye nyumba za ibada kwani wana hofu ya Mungu.
Mkuu hata huko kwenye nyumba za ibada ni wachache mnoo .....wengi ni walewale wanaolalamikiwa.
 
Wanaume wa enzi hizi nyie mtu akiwa mpole ndo kwanza mnamuona fala mtamuingizia hadi vidole machoni.....
Wadada wapole mnawatesa ka nini, muda wote wanalia tu utadhani wanapikia kuni.
 
Back
Top Bottom