Sifa za mwanamke wa Kirombo

Sifa za mwanamke wa Kirombo

Vatican

Member
Joined
Feb 18, 2013
Posts
22
Reaction score
4
Habari wana JF naomba kujua sifa za mwanammke wa rombo hasa wa sehemu ya keni . naomba kuwasilisha:A S kiss:
 
We oa tu unataka sifa za nini ? kabila halina sifa ila kila mwanamke ana sifa zake !!!
 
Umeona eh. Muda si mrefu watahamia Marangu. Nlimwambia Mentor akawa anabisha.

Kuwa mchaga kazi kweli
yaani bestie nilipoona heading ya hii thread nilikukumbuka manake kwenye ule wa wanawake wa machame uliyasema haya.
nimejikuta nakuona ghafla kufungua tu ndani nakuona wewe.
tusubiri tuone kesho watakuja na wachaga wepi.
Kweli wanawake wa kichaga tunakazi.
 
Wanawaita makobota yani wanafanya kazi kama trekta
 
anataka sifa gani , shape maumbile au tabia...na ni kwa ajili gani nianze kumdalalia dada angu..fasta kama ni kuolewa aolewe
 
Hizi hapa!
31.10 Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
31.11 Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.
31.12 Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.
31.13 Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.
31.14 Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.
31.15 Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao.
31.16 Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
31.17 Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu.
31.18 Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.
31.19 Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.
31.20 Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
31.21 Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
31.22 Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
31.23 Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
31.24 Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.
31.25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.
31.26 Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake.
31.27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.
31.28 Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema,
31.29 Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.
31.30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa.
31.31 Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.
 
Ukijua zitakusaidia nini cv ya kila mwanamke zinatofautiana na sio kwa ujumla kama unavyotaka. Wewe oa tu hayo mengine ni ya kurekebishana ndani kwa ndani siri yenu. Ebo unafikiri zinaandikwa mahali kila mtu ajue!!!
 
Back
Top Bottom