Awe anakupenda kwa dhati kama anavyojipenda mwenyewe na wewe uwe unampenda kwa dhati kama unavyojipenda mwenyewe. Hapo mtaunganishwa na Mwenyezi Mungu na kuwa kitu/mtu mmoja na hakuna kitakachoweza kuwatenganisha isipokuwa kifo! Kwenye dhiki na raha mtakuwa kitu kimoja.
NB: You both must be compatible. Haiwezekani kuwa na mume bora kwa wanawake wote au mke bora kwa wanaume wote. Aliye bora kwako (mume au mke) si bora kwa wenzio. Hivyo tafuta wa kwako ambaye naye atakuona ni mke bora kwake si kwetu, ebo! Yaani umemkosa hadi uje utuulize sisi huku Jf, sisi tutajuaje unapenda kipi kwenye midume? Tafuta kile roho yako inapenda wee binti, utakipata tu. Kila la heri. Humu Jf hutakipata. Mume/Mke sharti amchunguze mchumba wake kwa kina na kwa muda wa kutosha ili kujiridhisha kama anamfaa kuwa mume/mke wako kabla ya kuoana.