-----------------------------------
Jeshi la Polisi lipo kwa ajili ya kulinda usalama wa raia na mali zao.
Usalama wa raia ni kwa maana ya kusimamia haki za raia,kwa maana kila raia anayo haki ya kuishi kwa amani na Usalama.
Kila raia anayo haki na mipaka inayo zunguka haki zake.
Jeshi la Polisi kazi yake ni kulinda na kusimamia haki za raia zisivunjwe ndani ya mipaka yake na zisivuke nje ya mipaka yake.
Ni wajibu wa Jeshi la polisi kulinda mali halali za raia na kuzuia Mali hizo zisitumike kuvunja sheria na kuharibu haki za watu wengine.
Maana halisi ya Jeshi la polisi ni kusimamia uiano wa haki katika jamii,
Haki ambayo itamuweka kila raia aishi kwa amani na Usalama ndani ya mipaka ya haki zake.
Msingi mkuu wa sifa zinazoweza kukidhi wajibu wa kutekeleza majukumu ya polisi ni uadilifu.
Kwa bahati mbaya Jeshi letu la Polisi katika mchakato wa kutafuta vijana wa kujiunga na Jeshi hilo hawakuweka namna bora ya uteuzi kwa kutumia kigezo cha uadilifu.
Vitu vilivyopewa umuhimu ni Elimu,Kimo,afaya,taaluma, Lakini Uchunguzi makini juu ya tabia za kimaadili za muombaji hazipewi nafasi ya kwanza.
Lau Jeshi la Polisi lingeweka kigezo cha maadili kuwa ni sifa ya lazima kwa waombaji wa nafasi katika jeshi hilo, bila shaka Jeshi hilo lingeng'ara kwa uadilifu.
Leo hii utakuta mchezaji wa mpira anapata ajira ya kuwa polisi kwa sababu tu jeshi la Polisi lina timu ya mpira,! Mara nyingine utakuta mchezaji huyo hana maadili,mlevi, mgomvi,mpenda rushwa n.k.
pamoja na sifa ya uchezaji anaingia mitaani kufanya kazi za kipolisi !
Unategemea nini kitatokea kwa Polisi huyo?
Hakuna Uadilifu wa kweli nje ya hofu ya Mungu.
Mtu akijengeka kwa hofu ya Mungu hawezi kufanya hata uhalifu wa Siri kwa sababu anajua kuna nguvu inayo muoana hata sirini.! hivyo hofu ya Mungu inakuwa ni kidhibiti cha maazimio ya kutenda uovu.
Hofu ya kuogopa mkono wa Serekali haina nguvu kwa sababu Serekali haijui maazimio maovu yanayo fanyika sirini.
Kwa hivyo Jeshi la polisi litafute namna ya kushirikisha vyombo vya kiroho(kidini) katika kuwaandaa vijana kwa ajili ya kulitumikia Jeshi hilo.
Na kuwepo na vyeti vya kufuzu maadili vinavyo tolewa na vyombo hivyo vya kiroho, Na mtu yoyote asipate nafasi ya kujiunga na Jeshi bila kuwa na cheti hicho.
Ikiwa askari atakiuka maadili baada ya kuwa na elimu ya maadili atapoteza sifa ya kumiliki cheti hicho .
Na kwa kuwa atakuwa amepoteza sifa ya kumiliki cheti hicho Basi itakuwa amepoteza pia sifa ya kuwa askari.
Kama ni kosa la kustahili onyo! adhabu iwe ni kurudi katika vyombo vya kiroho kupigwa msasa kwa Muda wa miezi mitatu kwa gharama zake.
Na kuwepo na ukomo wa maonyo kuwa ni mara tatu, baada ya hapo ni kupoteza ajira moja kwa moja.
Kwa hivyo cheti cha Maadili kiwe ndiyo kigezo muhimu na kipewe nguvu.!
Na vyuo vya maadili vya kiroho viundwe kwa ajili ya kuwaandaa vijana watakao kuwa na sifa za kimaadili kuweza kupata nafasi ya kujiunga na Jeshi hilo.
Na hata Kama Jeshi hilo linapo hitaji kuwa na watu wenye taaluma fulani ,iwe ni lazima kwa mwana taaluma huyo kwenda kupigwa msasa kwenye vyombo vya kiroho kwa muda usio pungua miezi mitatu na kupata cheti cha kufuzu.!
Na cheti hicho kipewe nguvu ya kuamua mustakbali wa ajira yake pindi inapo tokea ukiukwaji wa kimaadili .
Taaluma isiyo na maadili isiwe kitu cha kumbakisha mtu katika ajira,
Kwa njia hii naamini tutapata Jeshi la polisi bora Sana.