Sifa ya Bunge letu la sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sifa ya Bunge letu la sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Seacliff, May 5, 2012.

 1. S

  Seacliff Senior Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Hata kwa wale ambao hawakubaliani na baraza jipya la mawaziri, inabidi tukubaliane kwamba hatua hii aliyochukua Raisi ni acknowledgement kuwa Bunge letu lina sauti na sauti yake ni muhimu. Afterall, sidhani kama kuna team yeyote ambayo JK angeweza kuileta ikaturidhisha tulio wengi kwa sababu tunajua kuwa atakaowaleta watakuwa na jukumu la kumfichia madudu yake aliyofanya yeye kwanza, taifa next. Wabunge wa upinzani ni wachache ukilinganisha na wale wa chama tawala lakini just imagine kwa kupata support ya wabunge chini ya kumi kutoka kwenye chama tawala, wapinzani wameweza kutikisa serikali ambayo kwa muda mrefu sana imekuwa arrogant na viongozi wake (watawala) wamekuwa wakorofi shauri ya pesa ambayo wamewaibia wananchi. Nampa heshima nyingi sana Mhe. Zitto kwa kuweka pembeni personal feelings na uhusiano mzuri ambao anao na hawa viongozi wa CCM (pamoja na hao mawaziri anaowapiga vita) kwa ajili ya kutetea taifa letu. Ila wabunge wa CCM waliokubaliana na hoja ya upinzani kwa risk waliyochukua lazima tuwape heshima zao pia. Ninachotaka sisi wananchi tuendelee kusukuma ni ile hoja ya kuwaadhibu hawa wezi kisheria na pia tuendelee kumbana Raisi ili awachukulie hatua wateule wake wanaoongoza mashirika na vitengo vingine ambavyo vimeonekana kuwa na wizi wa pesa ya umma. Nina wasiwasi kwamba hao wanaweza kuishia hivi hivi bila adhabu kama wale waliotuibia kwenye EPA, wakina Jairo, etc.
   
 2. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,938
  Likes Received: 37,436
  Trophy Points: 280
  Hujakosea mheshimiwa,nakuunga mkono asilimia mia moja.
   
Loading...