ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
11/03/2013
Chanzo: Gajetek - Gajet na Teknolojia
Sifa Muhimu za Laptop Ya Leo
Chanzo: Gajetek - Gajet na Teknolojia
Sifa Muhimu za Laptop Ya Leo
Laptop imekuwa ni sehemu ya maisha ya wanajamii wengi, ni sehemu ya maisha ya kazi, ni sehemu ya maisha ya burudani, ni sehemu ya maisha ya kielimu. Pia laptop ni msaidizi wa maisha ya kila siku. Ni vigumu kuzungumzia ni sifa gani muhimu laptop iwe nazo kwa kila mmoja wetu kwa vile sote tunatumia laptop kwa madhumuni tofauti, ujuzi tofauti na hata kazi tofauti.
Makala hii itazungumzia sifa tofauti za laptop badala kuzungumzia mambo kama vile kasi ya prosesa, kumbukumbu (RAM) na ukubwa diski, sifa ambazo wengi wetu tumezizoea kwa vile ndio sifa zinazozungumzwa mara kwa mara. Hii hutupelekea kuacha mambo muhimu kutokana na mabadiliko ya kteknolojia.
1. Windows 8
Haihitaji kuwa mwanasayansi kujua kuwa Windows 8 italeta mabadiliko makubwa katika kompyuta, sababu ni kule kutumia mtindo wa metro (tiles) hivyo kufanya mguso ni jambo rahisi kuliko Windows zote zilizopita. Pia kuwekwa kwa soko la Apps (Windows Store) ambapo apps ni bei rahisi mno ukilinganisha na mtindo wa zamani wa kampuni kuuza software wenyewe. Urahisi unakuja kutokana na matarajio kwamba apps zinauzika kirahisi kwenye soko maalum, hivyo watengeza apps hufanya mauzo makubwa, hivyo faida huja kwa idadi badala ya bei. Pia tukumbushe kuwa kuna apps nyingi tu za bure.
Unaponunua laptop ya Windows 8 unatakiwa uwe makini kwa vile zipo aina mbili Windows 8 RT na Windows 8 Pro. Tofauti kubwa ni kwamba RT haikubaliani na baadhi ya software za zamani. Hata hivyo windows 8 RT hutumika zaidi katika tableti.
2. Kibodi za Kuchomoa/Kuchomeka
Kwa lugha ya mkoloni hizi hujulikana kama detachable keyboards. Aina ya kibodi hizi hupatikana kwenye kompyuta za aina mbili, ama tableti au laptop. Ambapo kwenye tableti huwa ni kibodi za kuchomeka na kwenye laptop ni za kuchomoa. Kwa uzoefu kibodi za kuchomoka kwenye tableti si zenya maana sana kwa vile hazifai kwa kazi ndefu na inachukua muda mrefu kuzizoea.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba vifungo huwa vimekaribiana sana na kusababisha mchapaji anapotumia kufanya makosa mengi mfululizo au kutoweza kutumia kwa kasi yake ya kawaida. Tunashauri zaidi kompyuta zenye kibodi za kuchomoka ziwe na ukubwa usiopungua inchi 11, lakini ukubwa sahihi kabisa ni kuanzia inchi 13. Hii hutoa nafasi kwa kibodi kuwa na upana wa kutosha na hivyo vifungo kutokaribiana.
3. Skrini Mguso
Skrini hizi zimeanza kutoka kwa wingi baada ya kuwepo kwa Windows 8 ambayo haikutimiza hata mwaka mmoja. Windows 8 kwa vile ina mtindo unaojulikana kama Metro ambapo apps zinajipanga kama tiles, hufanya mguso kuwa ni rahisi, Skrini mguso ikiwa na sifa ya juu yaani kibodi ya kuchomoka basi huhitaji tena kununua tableti ya Windows 8 kwa vile tayari una li-tableti kubwa kiasi.
4. Betri
Hili ni jambo muhimu ukizingatia matatizo yetu katika suala la umeme na mahangaiko ya maisha kuwa muda wa kutwa unaweza usiwe na nafasi ya kuchaji. Betri nyingi kwa sasa katika laptop zinafika masaa 8 zinapokuwa na chaji kamili hadi kufikia karibu na 0%. Hivyo mnunuaji anatakiwa kuwa na uwiano mzuri wa nguvu ya kompyuta na kudumu kwa betri kwa sababu katika mawili haya kuna kupishana, kila laptop inapokuwa na nguvu zaidi basi inakula betri zaidi. Laptop ya leo basi isishuke masaa 6 katika betri.
5. Mg'ao wa Skrini
Tunaweza hii tukaiita anasa (luxury), lakini kwa sasa mng'ao wa skrini ni moja kati ya jambo ambalo huwa linaangaliwa pale mtu anapochagua laptop, hii imekuja hasa baada ya Apple kuanza kutoa MacBook zenye kioo cha retina. Ni vigumu kulizungumza hili kuwa ng'ao gani ni sahihi, lakini laptop ya leo inatarajiwa kuwa na rizolushani angalau 1366 x 768.
6. Aina ya Diski
Nyingi kati ya kompyuta za leo zinatoka na diski aina ya Solid State (SSD) badala ya High Density Disk (HDD) tulizozizoea. Tatizo kubwa la SSD ni ghali mno hivyo si ajabu ukakuta laptop ya hali ya juu kuwa na 64GB iwapo diski hii imetumika. Hivyo mtumiaji anatakiwa atambue kwamba SSD huongeza kasi ya kompyuta kwa kiwango kikubwa , SSD ina kasi mara nne zaidi ya HDD. Baadhi ya laptop wamekuwa wakiweka disk zote mbili ambapo SSD inatumika kwa shughuli muhimu kama vile ku-boot kompyuta na programu ambazo zinatumika mara kwa mara, kwa upande wa mafaili makubwa makubwa kama vile movie huhifadhiwa kwenye HDD. Apple katika kompyuta zao wameanza kutoa Fusion drive. Hizi ni mchanganyiko wa SSD na HDD.
Ni matarajio yeku kwamba kampuni nyingi katika kipindi hicho cha mpito zimechanganyikiwa juu ya tofauti gani waweke baina ya laptop na tableti za windows. Hivyo mnunuaji unapotaka kununua laptop ni vyema pia ukachungulia kwenye tablet kwani hizi zina bei nafuu na unaweza ukaikuta inayofaa kwa shughuli zako. Kuna tablet kwa sasa ambazo zina ukubwa unaokaribia inchi 12. Na kuna lijitablet lililotolewa na Lenovo lina inchi 27. Hili kwenda nalo kazini inabidi uwe na mkokoteni.