Sifa kuu ya Madikteta ni kulazimisha kupendwa, kutukuzwa na kusujudiwa...ole wako ukatae kumpenda, kumtukuza na kumsujudu!

Huyu wa kwetu sio dikteta kama hao kina Eyadema na Mzee wa Cameroon, anainyoosha nchi ambayo iliufuga uzembe na ufisadi kwa miaka kama thelathini ya uhai wa taifa hili.

Huyu wa kwetu ataondoka 2025 Mungu akitujalia uhai, tulimhitaji mtu wa aina yake, ambaye anayo hulka isiyowapendezesha watu wanaopenda mazabe na maisha ya uonevu unaotokana na jeuri ya pesa.

Huyu ataongoza ndani ya muda wa kikatiba, kinachohitajika kufanywa na baadhi yetu ni kuondoka na fikra za malalamiko, maisha ni mafupi na muda huwa hauendi mapumziko.
 
Afadhali hata Hitler alikua dikteta kamili, kuna chizi mmoja yeye ni "dikteta uchwara" lakini anapenda kusifiwa mno na mafisi wote hata wale waliookotwa jalalani wanasifu hata wakati wa kuomboleza!
 
Na bila ya kumsahau Yahaya Jammeh.

Yaani ni ajabu ya watu kuwa na mfanano kiasi hiki huku wakiwa umbali kiasi kile. Nadhani tabia hizi zimo kwenye DNA. Kuna watu wanazaliwa pengine pakiwa na kasoro fulani katika muundo wa DNA zinazohusisha tabia.

Kutaka kupendwa, ukatili na kujigeuzageuza kitabia wawapo sehemu za watu; kuonekana wapenda dini na kutaka waonekane wao ni wazalendo zaidi na kwa hiyo raia wengine wote waige mifano ya uzalendo kutoka kwao.

Fikra hizi zinanipeleka kwenye 'movie' ya "A Beautiful Mind". Hawa watu ni halisi na uchizi wao au umashuhuri wao unatokana na DNA zao.

La ajabu ni kwamba vijana kama huyo aliyeandika hayo tayari tunao, hata hapa JF. Nikitaka ntaorodhesha, lakini, aah, acha tu!

Mkuu hapo chini umeandika kwa hisia sana
 
Afadhali hata Hitler alikua dikteta kamili, kuna chizi mmoja yeye ni "dikteta uchwara" lakini anapenda kusifiwa mno na mafisi wote hata wale waliookotwa jalalani wanasifu hata wakati wa kuomboleza!
Mkuu Hili tatizo la kumuona Hana madhara tangu mwanzo ndio limetufikisha Hapa

Mambo yanazidi kuwa mabovu, Lissu alikosea Sana

Huyu Sio Dikteta uchwara Kama wengi mnavyodhani,Huyu ni Dikteta haswa,katili na hatanii

Tuamkeni
 
Huyu wa kwetu sio dikteta kama hao kina Eyadema na Mzee wa Cameroon, anainyoosha nchi ambayo iliufuga uzembe na ufisadi kwa miaka kama thelathini ya uhai wa taifa hili.

Huyu wa kwetu ataondoka 2025 Mungu akitujalia uhai, tulimhitaji mtu wa aina yake, ambaye anayo hulka isiyowapendezesha watu wanaopenda mazabe na maisha ya uonevu unaotokana na jeuri ya pesa.

Huyu ataongoza ndani ya muda wa kikatiba, kinachohitajika kufanywa na baadhi yetu ni kuondoka na fikra za malalamiko, maisha ni mafupi na muda huwa hauendi mapumziko.
Pambana na hali yako.
 
Utasikia kwenye awamu hii tumetekeleza uchumi umepanda kwa 8%.

Tumetekeleza

Ndege
Daraja
Bara bara.
Ajira.

Sasa hizo ajira sasa ukija kitaa ulizia majibu utakayo yapata.

Ukitaka kufurahi zaidi ngoja usikie figure za kwenye makaratasi, utasikia tumepandisha bajeti ya afya toka 32b mpaka 200b, jaribu kufuatilia pesa zinazoenda hazifiki hata 20b@yr!
 
Hata Mwalimu Nyerere alisema, 'ukiwa kiongozi halafu ukaona kila mmoja anasema maneno ya kukusifu tu, ujue umekuwa dikteta'. Lazima uwe.mjinga hasa kuamini kuwa wewe ni mzuri sana kiasi cha kusifiwa na kila mtu.

Kibaya zaidi yeye ndio kaunda hicho kitengo cha propaganda, ila jinsi hata wenye elimu zao walivyopokea na kuimba kiitikio cha hizo sifa za uongo, hata yeye anafikia mahali anaamini uongo wake kwa kudhani ni kweli!
 
Huyu wa kwetu sio dikteta kama hao kina Eyadema na Mzee wa Cameroon, anainyoosha nchi ambayo iliufuga uzembe na ufisadi kwa miaka kama thelathini ya uhai wa taifa hili.

Huyu wa kwetu ataondoka 2025 Mungu akitujalia uhai, tulimhitaji mtu wa aina yake, ambaye anayo hulka isiyowapendezesha watu wanaopenda mazabe na maisha ya uonevu unaotokana na jeuri ya pesa.

Huyu ataongoza ndani ya muda wa kikatiba, kinachohitajika kufanywa na baadhi yetu ni kuondoka na fikra za malalamiko, maisha ni mafupi na muda huwa hauendi mapumziko.

Hata ukienda huko kwa kina Eyadema na Paulo Biya kuna watetezi wake kama ww, na wao wanamisamiati kama hii ya kwako, tena yakwao ni mitamu zaidi ya hii. Anapambana na ufisadi lakini kafunga mahakama ya mafisadi kwamba haina wateja, ukiuuliza fisadi aliyefungwa mpaka sasa hakuna. Ukihoji sana, anahitimisha kwa kusema hafukui makaburi, wapambe mkisikia hivyo mnawahi humu jukwaani kwamba hatujawahi kupata kiongozi wa hivyo!
 
Na bila ya kumsahau Yahaya Jammeh.

Yaani ni ajabu ya watu kuwa na mfanano kiasi hiki huku wakiwa umbali kiasi kile. Nadhani tabia hizi zimo kwenye DNA. Kuna watu wanazaliwa pengine pakiwa na kasoro fulani katika muundo wa DNA zinazohusisha tabia.

Kutaka kupendwa, ukatili na kujigeuzageuza kitabia wawapo sehemu za watu; kuonekana wapenda dini na kutaka waonekane wao ni wazalendo zaidi na kwa hiyo raia wengine wote waige mifano ya uzalendo kutoka kwao.

Fikra hizi zinanipeleka kwenye 'movie' ya "A Beautiful Mind". Hawa watu ni halisi na uchizi wao au umashuhuri wao unatokana na DNA zao.

La ajabu ni kwamba vijana kama huyo aliyeandika hayo tayari tunao, hata hapa JF. Nikitaka ntaorodhesha, lakini, aah, acha tu!
Wataje hao Malofa in mkapa's voice
 
Kuna siku kwny ziara mojawapo maza mmoja hivi sijui ni mkurugenzi wa wilaya gani huko akaambiwa haya Mama serikali iliwapa sh. Ngapi kujenga vituo vya afya.

Maza akaanza kumwaga sifa mh.Rais kwanza tuseme kwny awanu hii ya 5 tumeshuhudia mambo makubwa na yasiyo wezekana kama elimu bure,mabarabara yanajengwa sijui nini nikaona mzee baba amemkatisha fasta tu akamwambia Mama hebu nijibu swali langu mmepokea fedha kiasi gani,hahah

Nahisi kama mzee baba sometimes na yeye anajua kabisa kua wanamchora tu na kumsifia sifia.

Back
Top Bottom