SoC03 Sifa kuu ambayo mwajibikaji anaendeshwa nayo ni hii

Stories of Change - 2023 Competition

dennistheodory

New Member
Oct 4, 2021
2
1
.
Sio kila mtu anaweza akawa mwajibikaji kama hajajua vitu muhimu ambavyo mtu mwajibikaji anapaswa kuwa navyo. Mtu mwingine hujaribu kuwa mwajibikaji kwa mda fulani, lakini kwasababu hajazoea hayo maisha, mbio zake huishia ukingoni.

Kwa mfano, tukiwa mashuleni kwa wale ambao hawakuwa na tabia ya kujisomea, matokeo ya mtihani yakishatoka na kwa bahati mbaya yamekuja vibaya kwake, unakuta kabisa ndani yake anadhamiria, kuanzia leo naamka mapema nawahi darasani, nakesha kusoma, siendi kuangalia tv, naachana na marafiki fulani na fulani, kusema kweli mwanzoni atakuwa anafanya kwa uaminifu, lakini baada ya siku kadhaa anarudi kule alipotoka.

Uwajibikaji ni tabia, ambayo mtu anaijenga ndani yake. Sasa ni kitu gani au sifa gani kuu ambayo mwajibikaji anaendeshwa nayo? Jibu ni jepesi, muda ni hiyo sifa kuu. Unaweza ukashangaa muda kivipi? Mtu ambaye ameweza kuujali mda, basi ameweza kujenga tabia ya uwajibikaji. Sasa kwasababu mtu hajazoea kujali mda, mwanzoni atapata changamoto kuijenga hii tabia.

Kwanini muda? Biblia inatuambia hivi “utunzeni wakati” ukisoma kwa kingereza inasema “redeem the time..” muda ni kitu muhimu mno katika maisha ya mwanadamu, mtu yeyote ambaye ameweza kuiba muda wako, basi ameweza kuiba kesho yako, kivipi, angalia wazee wazamani waliogundua mambo makubwa, mfano Isaack Newton, Charles Darwin n.k. hivi umewahi jiuliza aliwezaje kugundua umeme? wakati umeme hata haukuwepo, yani kulikuwa na mishumaa au moto ndo ilikuwa chanzo cha mwanga.

Watu halo walichukuwa mda mwingi kukaa peke yao kuwaza nini chakufanya, namna gani itumike, na ni watu gani nishirikiane nao. Mfano mwingine tena, hiyo kampuni ambayo umeajiriwa (ikiwa umeajiriwa) umewahi uliza ilianzaje? Muda ni kitu ambacho watu wengi wameshindwa kutunza hivyo hata uwajibikaji haupo. Ukijua muda ni mdogo na mambo ya kufanya ni mengi, utajua umuhimu wa muda katika maisha yako.

Sekunde moja ikiondoka hairudi tena, watu amabo sio wawajibikaji wanaona muda bado upo bwana, ngoja nikajirushe na masela, ngoja niende club, ngoja nikamsalimie fulani, ngoja nilale, ngoja ngoja yaumiza matumbo.

Sifa moja kuu inayomfanya mtu aanze kuwajibika, ni lale anapogundua muda alionao ni mchache na mambo anayopasa kufanya ni mengi, vitabu vya kuandikwa ni vingi, ugunduzi wakufanya ni mwingi, mambo ya kusoma ni mengi, vitu vya kujifunza ni vingi, mambo ya kuacha ni mengi n.k hapo sasa utajikuta unaanza kuwajibika na mambo yako na yale uliyokabidhiwa.
 
Back
Top Bottom