SoC03 Uwajibikaji wa viongozi huende sambamba na uzingatiaji wa maadili ya utumishi wa umma

Stories of Change - 2023 Competition

dedication

New Member
Jun 1, 2023
1
0
UTANGULIZI
Uwajibikaji, ni kitendo cha kiongozi au mtu yoyote mwenye dhamana ya kutekeleza majukumu na wajibu elekezi ambayo anapaswa kuyatekeleza kwa uaminifu uliotukuka kwaajili ya manufaa na maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla. Uwajibikaji huo huenda sambamba na uzingatiaji wa sheria ili kuepuka migongano katika eneo la kazi. Katika, katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 8 (1) (c) inasema, "serikali itawajibika kwa wananchi" kwa hiyo, serikali ya Tanzania haina budi kuwajibika kwaajili ya kuwaletea wananchi maendeleo. Maendeleo hayo lazima yawe ni ya muda mfupi, na muda endelevu.

MAONI KUHUSU UWAJIBIKAJI

Ni kweli kuwa, suala la uwajibikaji linaweza likatazamwa katika mitazamo mbalimbali kulingana na uelewa tofauti tofauti na mitazamo mbalimbali. Hoja zifuatazo hapa chini ni mitazamo binafsi juu ya uwajibikaji jinsi inavyoweza kuzingatiwa na kila aina ya kiongozi.

Uwajibikaji wa viongozi huende sambamba na uzingatiaji wa maadili ya utumishi wa umma. Mfano, ibara ya 132 ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na masharti ya sheria ya maadilii ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995, inamtaka mtumishi kuzingatia maadili katika kazi yake. Moja ya matakwa ni kuilinda na kuitetea katiba ya jamuhuri kwa moyo wote., Lakini pia anaapa kutotoa huduma kwa upendeleo wala kwa maslahi binafsi. Ni wajibu wao kukumbuka kwa vitendo kiapo hicho.

Kiongozi mwenye dhamana hana budi kuweka mbele maslahi ya umma kwanza. Napenda kurejelea kitabu cha mmarekani "Simon Sinek," "1995" aliandika kitabu kiitwacho "Leaders eats last". Alikuwa anaelezea viongozi bora ni lazima ahakikishe anaowaongoza wawe wamekula kwanza ndo kiongozi naye apate wasaa wa kula. Hii inawakumbusha viongozi wote kuwajibika kwaajili ya raia wake anaowaongoza nkwa kutanguliza maslahi ya raia kwanza na kuwatatulia changamoto zao kwa uaminifu na bila upendeleo.

Kiongozi anawajibika kuwa ni chombo au chachu ya kuunganisha au kiunganishi muhimu ndani ya jamii husika. Napenda kurejelea hotuba ya mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1995 kuhusu muungano, "mwalimu alikemea vikali suala la Upemba, unguja, na ukabila". Nia hiyo inaonesha dhamira ya dhati ya mwalimu kwa kutaka watu wote wawe kitu kimoja. Kiongozi mwenye nia dhabiti na njema hana budi kutilia maanani suala hilo kwa weledi sana. Na viongozi lazima wazingatie kauli zao wawapo majukwaani , wakati mwingine huwa na lugha za uchochezi.

Uwajibikaji wa kiongozi lazima uende sambamba na upatanishi. Mfano mzuri hapa ni rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa dkt Samiah Suluhu Hassan, ameweza kufikia maridhiano kati ya chama tawala na vyama vya upinzani. ma uangazie suala la upatanishi. Upatanishi ni kitendo cha kuleta marufu pale Mheshimiwa rais alikuja na mbinu mpya ya R-nne, nazo ni;.
  • Resilince (ujasiri).
  • Reconciliation (upatanishi).
  • Rebuilding (kujenga tena).
  • Reforms (marekebisho).

Rais Samiah amekuja na r nne kwa lengo la kujenga ustawi wa kisiasa kwenye vyama vya siasa.

Uwajibikaji huenda sambamba na uzingatiaji na kuheshimu haki za binadamu. Haki za binadamu ni mahitaji ya msingi ya mwanadamu yoyote ambayo ana haki ya kuyapata pasipo kupungua, mfano wa haki hizo ni kuishi, kujieleza, kusikilizwa,kula,kuishi,faragha, na kadhalika. (Rejea Universal Decralation of Human Rights UNDHR 1948). Tukienda mbali zaidi, wenye dhamana hawana budi kuzingatia utiifu wa sheria bila shuruti, kuheshimu sheria elekezi na sheria mama. Na hiyo ndio tunu bora kwa maendeleo ya taifa letu. Mwalimu Nyerere alitaja mambo makuu matatu ambayo ni viungo muhimu kwa ustawi wa nchi yetu nayo ni "watu, ardhi na siasa safi" mambo haya ni muhimu kuzingatiwa na kufanyiwa utekelezaji kwa vitendo kwa juhudi ya hali ya juu.

Kwa muktadha uleule na mlengwa uleule wa kusimamia kila anachokiamini chenye manufaa kwa taifa letu. Kiongozi hanabudi kuheshimu, kupokea, kusikiliza, na kuzingatia mitazamo na mawazo ya watu mbalimbali. Hii husaidia kujua na kutambua masuala hata ambayo yeye kama kiongozi mambo asiyoyafahamu. Na huu humsaidia kujua ukweli wa jambo fulani. Licha ya hilo, ni jambo jema pia kuwa tayari kukosolewa kwa staha kutoka kwa wale wanaokinzana nae kiitikadi.

Kwa kuhitimisha, kumekuwa na tuhuma kadha wa kadha kwa baadhi ya viongozi waliopewa dhamana kutowajibika kikamilifu katika majukumu yao, na hii hupelekea malalamiko ya moja kwa moja kutoka kwa wananchi dhidi ya serikali. Hii ni alama tosha kuwa, kuna tatizo mahali, la baadhi ya viongozi kulegalega katika majukumu yao. Ni wajibu wao sasa kujitathmini kwa kina mapungufu yao, na kuwa tayari kurekebika na kuanza uelekeo mpya ambao ni chachu ya maendeleo kwa taifa letu tukufu la Tanzania.

Na Kazi Iendelee.
 
Back
Top Bottom