Sielewi msimamo wa serikali ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sielewi msimamo wa serikali ya Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Livanga, Mar 10, 2011.

 1. Livanga

  Livanga JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Apr 15, 2010
  Messages: 458
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  wandugu


  Baada ya kusikia kuwa serikali imemzuia Mchungajio msaafu Ambilikil Mwasapila nimebakiwa na maswali mengi sana kwa serikali. Sababu waliotoa ni kwamba hana kibali hilo ndilo kubwa usafi ni nyongeza tu ila muhimu pia.
  • Maswali yangu kwa serikali ni kwamba walikuwa wapi siku zote mpaka babu amewahudumia watu wengi kiasi hicho wasimfungie?
  • kama hakuwa na kibali kwanini walimpa usafiri na vikombe na sufuria?
  • kwa mujibu kwa maelezo tuliyonayo alianza kutoa huduma mwaka jana na serikali ililijua hilo je mlikuwa mnasubiri wananchi wengi wajue ndio mumfungie?
  • kwanini hamkufanya hivyo kabla habari hazijasambaa kwa upana kiasi hiki?
  • Ni nini maana ya marufuku yao kama zaidi ya watu elfu 12,000 wameshapata huduma?
  • katika watu walihudhuria kupata huduma ni pamoja viongozi wa juu wa serikali na vyama je nao hawakujua kuwa hana kibali?
  • siku zote kitu kinachohusikia na imani hakipimiki, kama vipimo vyao vikionyesha hiyo dawa ni sumu na watu wengi wameshakunywa hawajadhurika je watatangaza hadharani?
  • kama wakimfungia moja kwa moja na nchi nyingine wakaomba kumuamisha kwa ajili ya kundelea na huduma serikali itafanyaje juu ya hilo?
  Ushauri wangu kwa serikali ni
  1. Kwa kuwa wananchi wamekubali na kudridhia kwa kiwangi kikubwa na
  2. kwakuwa serikali ni wananchi na kwakuwa wananchi wameonyesha kusikitishwa kwa kitendo chaserikali kumfungia babu na
  3. kwakuwa kuna waliodhibitisha kuwa wamepona nio bora serikali ikamuacha babu aendelee na huduma na waache kutoa kisingizio kuwa ni hali ya uchafu wakati hawaonyeshi juhudi zozote za kujenga temporary toilets to save those who are there for pastors service.
  4. Serikali iweke wazi kuwa wao hawatahusika na lolote litakalowapata wananchi kutokana na dawa iyo then babu aendelee na huduma yake. walioko pale wameshapoteza muda mrefu na mali ni bora wakaondoka wakiwa wameshapata huduma.
   
 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nyongeza kwa maswali yako; kwanini kunakuwepo ubanguzi linapokuja suala la huyo mchungaji, maana kila mtu anajua kwamba waganga wengi wa kienyeji, akiwemo wananduma, ambao inasemekana wana wateja wengi miongoni mwa viongozi wa juu nchini, wanatoa matibabu yao katika mazingira yasiyokuwa nadhifu, na hata dawa zao hazikupimwa. Mbona sijasikia wanapigwa stop!
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hizi thread za kulalamika kufungiwa huyu mchungaji zimekuwa nyingi mno.
  Mods mngeziweka pamoja.
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mimi nakubaliana na Serikali. Hakuna haja ya kujaza watu zaidi ya 1000 shemu isiyo na huduma. Mimi nashauri huyu mzee awe na wakala Arusha mjini ambaye atakuwa anapokea maombi (appointment) ya wagonjwa wanaotaka kwenda kunywa dawa na awe anaruhusu idadi ndogo ambayo inaweza kwenda siku moja na kupatiwa huduma siku hiyo hiyo. Njia nyingine, Serikali ingejenga AIR STRIP na kuruhusu Scheduled flights kupeleka watu huko maana kiasi cha TShs. 150,000 kinachotoza na wenye magari kinatosha kabisha kulipia usafiri wa ndege.
   
 5. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  hivi huduma za waganga wa asili au watibuji wa asili uwa zinafungwa?au mambi ya kanisani ya uponyaji uwa yanafungwa?
  mtu si anaenda kwa hiari yake mwenyewe au?
  kama suala ni afya kutokana na mazingira,basi either serikali itafute namna izo huduma ziwepo hapo au ndo ivo ni huduma ya hiari watu tu wanaweza anzisha "biashara zao" hapo za magesti,mama lishe,maduka nk nk

  watu wanafata uzima kwa hiari yao wenyewe
   
 6. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Taarifa ya habari ITV saa 4 wametangaza kuwa KKKT Arusha wameshafanya evaluation kwa ajili ya kujenga mjengo mkubwa utakaotumika kama kituo cha afya kwa ajili ya waendao kwa babu. Big up Askofu Laizer..
   
 7. Livanga

  Livanga JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: Apr 15, 2010
  Messages: 458
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Unfortunately jana sikuwahi kuona taarifa ya habari ila kama wamesema hivyo that is real good news coz kama mlivyoona na kusikia wananchi bado wanaendelea kumiminika bila kujali amri ya serikali sasa serikali wameshaonyeshwa njia they have to follow now. Big up KKKT Arusha esp Laiser
   
 8. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Wanajenga mjengo mkubwa wana mawasiliano na Mungu kwamba huyo mganga ana miaka mingapi ya kuendelea kuwepo hapa Duniani? Kama dawa lazima itolewe kwa mkono wake wakijenga hilo jengo na Mungu akaamua kumchukua kiumbe wake hili jengo bado litatumika kwa tiba hii au nyingine?
   
Loading...