Siasa za Unafiki, Chanzo cha Umaskini Afrika

Deogratias Mutungi

Senior Member
Joined
Oct 1, 2019
Posts
141
Reaction score
183
Afrika ni bara la pili kwa ukubwa baada ya Asia, Aidha ni bara la kwanza lenye utajiri na utitiri wa mali asili na vyazo vya kila aina ambavyo ni lulu kwa mwafrika, Hata hivyo Afrika ndilo bara lenye watu maskini Kuliko Mabara mengine. Ukitafakari kwa kina na kusoma tafiti za wanazuoni na wasomi walio bobea utagundua kuwa umaskini wetu Waafrika umejifunga kwenye kundi moja " Ombwe la Uongozi",
Inasemekana kwa karne nyingi Afrika imekosa viongozi wenye maono na dira katika kuipambania Afrika Kama ilivyokuwa enzi za akina Mansa Mussa na wengineo. Ukisoma Walter Rodney kwenye Kitabu chake cha "How Europe underdeveloped Africa" Utagundua kuwa kweli Afrika tunanyonywa na tunahitaji kiongozi mwenye uthubutu na uzalendo usio mithilika kupambana na wahuni wa Nchi za Magharibi.

Kwa bahati mbaya Waafrika tumekuwa tukihujumiana wenyewe kwa wenyewe hasa vijana wa kileo wamekuwa mstari wa mbele kuhoji na kudadisi mambo yasiyokuwa na msingi kupitia kivuli cha uhuru kujieleza.

Swali Kuu ni kwa nini Waafrika tunahujumiana na kujengeana fitina pale tunapompata kiongozi mwenye udhubutu wa kufuta uteja tunaonyoshewa kidole na Wazungu kuwa hatuna viongozi imara na shupavu, Je ni usasa au pengine ni ushamba. Kwanini tunapowapata viongozi bora wazungu utugawa kwa dhana za ukosefu wa demokrasia na ubakaji wa katiba na sisi ukubali kugawanyika kirahisi, tatizo ni nini hasa?

Ni wajibu wetu kuwaunga mkono viongozi wanao onyesha njia ya mabadiliko katika usimamizi wa rasili mali zetu, tusiwasikilize ndumila kuwili wa Magharibi, tushikamane hili tusonge mbele kimaendeleo na kiuchumi, tuwe makini tunaweza kujikita kwenye harakati za kudai demokrasia isiyoeleweka wakati taifa letu linaendelea kuzama kwenye wimbi la umaskini.

Vijana tujifunze kuwasilisha mawazo mbadala kwa misingi ya kuisaidia nchi, Amerika ya leo ilijengwa na vijana wazalendo wakati huo baada ya kupata uhuru wake, tuache kulalamika bali kutafakari ni kwa jinsi gani tumewasaidia viongozi wetu na nchi yetu katika kustawisha nchi.
 
Vijana tujifunze kuwasilisha mawazo mbadala kwa misingi ya kuisaidia nchi, Amerika ya leo ilijengwa na vijana wazalendo wakati huo baada ya kupata uhuru wake, tuache kulalamika bali kutafakari ni kwa jinsi gani tumewasaidia viongozi wetu na nchi yetu

Umeongea mambo mazito
Africa wanasiasa Wengi wanajipendekeza kwa Mabeberu wakidhani wanapendwa kumbe wanatumika kuharibu Nchi zao

Tumuunge mkono Magufuli kujenga Tanzania imara kwa ajili ya kizazi cha leo na kijacho
 
Ulichokisahau tu ni kwamba hata Wewe hapo ulipo kama ni Mwafrika basi nawe ni Mnafiki vile vile kwani Waafrika karibia Wote tumebarikiwa kwa Unafiki tena ule ' uliotukukuka ' kabisa hivyo ukiwa unawasema tu hawa Viongozi / Watawala wetu naona ni kama vile unawakosea.
 
Muandishi imejichanganya sana; mara ooh changamoto ya Afrika ni viongozi hapo hapo unasifia kiongozi mzuri anapopatikana anakomaa na kupambana na ubeberu lakini anawaminya wenzake demokrasia; mara oooh vijana tumuunge mkono kwa kuleta mawazo yanayojenga umesahau kama hashauriki; unalalamikia unafiki wakati wewe mwenyewe ni typical mnafiki mkubwa, wachumia tumbo nyie ndio mnatuharibia nchi yetu kwa kivuli cha kupambana na ubeberu. Jifunze sifa za kiongozi bora alafu ndio uje umlinganishe na huyo wako unayetaka kujishaua nae hapa. Shwain!!!
 
Umeongea mambo mazito
Africa wanasiasa Wengi wanajipendekeza kwa Mabeberu wakidhani wanapendwa kumbe wanatumika kuharibu Nchi zao

Tumuunge mkono Magufuli kujenga Tanzania imara kwa ajili ya kizazi cha leo na kijacho
Na waliosaini mikataba ya kijinga na kupora rasilimali zetu kuwapa mabeberu tokea tupate uhuru wote hao hawafai kwenye africa yetu.
 
Tatizo ni kwamba tunaiga mifumo ya utawala ya wazungu wakati wao wamepitia mifumo mingi kabla ya kufikia mfumo walio nao leo. Na pia tusisahau kuwa wazungu hawa wana mila, destuli 'na historia tofauti tofauti. Sisi pia tunahitaji kuwa 'na mfumo wetu, si tu kama waafrika bali kama watanzania.
 
So tuache kutumia smartphone tuanze na tpyewritter ili tuende hatua kwa hatua mpaka tuwakute walipo leo. Halafu unaona umekuja na mawazo ya maana?
 
Afrika ni bara la pili kwa ukubwa baada ya Asia, Aidha ni bara la kwanza lenye utajiri na utitiri wa mali asili na vyazo vya kila aina ambavyo ni lulu kwa mwafrika, Hata hivyo Afrika ndilo bara lenye watu maskini Kuliko Mabara mengine. Ukitafakari kwa kina na kusoma tafiti za wanazuoni na wasomi walio bobea utagundua kuwa umaskini wetu Waafrika umejifunga kwenye kundi moja " Ombwe la Uongozi",
Inasemekana kwa karne nyingi Afrika imekosa viongozi wenye maono na dira katika kuipambania Afrika Kama ilivyokuwa enzi za akina Mansa Mussa na wengineo. Ukisoma Walter Rodney kwenye Kitabu chake cha "How Europe underdeveloped Africa" Utagundua kuwa kweli Afrika tunanyonywa na tunahitaji kiongozi mwenye uthubutu na uzalendo usio mithilika kupambana na wahuni wa Nchi za Magharibi.

Kwa bahati mbaya Waafrika tumekuwa tukihujumiana wenyewe kwa wenyewe hasa vijana wa kileo wamekuwa mstari wa mbele kuhoji na kudadisi mambo yasiyokuwa na msingi kupitia kivuli cha uhuru kujieleza.

Swali Kuu ni kwa nini Waafrika tunahujumiana na kujengeana fitina pale tunapompata kiongozi mwenye udhubutu wa kufuta uteja tunaonyoshewa kidole na Wazungu kuwa hatuna viongozi imara na shupavu, Je ni usasa au pengine ni ushamba. Kwanini tunapowapata viongozi bora wazungu utugawa kwa dhana za ukosefu wa demokrasia na ubakaji wa katiba na sisi ukubali kugawanyika kirahisi, tatizo ni nini hasa?

Ni wajibu wetu kuwaunga mkono viongozi wanao onyesha njia ya mabadiliko katika usimamizi wa rasili mali zetu, tusiwasikilize ndumila kuwili wa Magharibi, tushikamane hili tusonge mbele kimaendeleo na kiuchumi, tuwe makini tunaweza kujikita kwenye harakati za kudai demokrasia isiyoeleweka wakati taifa letu linaendelea kuzama kwenye wimbi la umaskini.

Vijana tujifunze kuwasilisha mawazo mbadala kwa misingi ya kuisaidia nchi, Amerika ya leo ilijengwa na vijana wazalendo wakati huo baada ya kupata uhuru wake, tuache kulalamika bali kutafakari ni kwa jinsi gani tumewasaidia viongozi wetu na nchi yetu katika kustawisha nchi.

Ww ni mmoja ya watu wajinga mnaojifanya mna mawazo ya kizalendo kumbe upuuzi mtupu. Sisi hatuna muda wa kumuunga mkono kiongozi maana tukishatoka dunia ya kusujidia viongozi, tunataka mifumo imara itajayomuwajibisha mtu yoyote bila kujali nafasi yake. Kama wa unamsujudia kiongozi mtu na sio mifumo imara mchukue akiongozwa huko nyumbani kwako, na ukiweza mpishe kitandani awe analala na mkeo ili awaongeze vizuri.

Umuunge mkono kiongozi anayeonesha ubaguzi wa wazi kwa wananchi wenye itikadi tofauti na yeye, kwenye dunia hii ya sayansi na technologia hilo haliwezekani? Dunia hii nchi huendeshwa kwa mifumo imara tu na sio porojo za mtu mmoja. Ukimaliza hizi porojo zako uweke deni la taifa ni kiasi gani mpaka sasa.
 
Mkuuu naona umeenda mbali zaidi, why?
 
Muandishi imejichanganya sana; mara ooh changamoto ya Afrika ni viongozi hapo hapo unasifia kiongozi mzuri anapopatikana anakomaa na kupambana na ubeberu lakini anawaminya wenzake demokrasia; mara oooh vijana tumuunge mkono kwa kuleta mawazo yanayojenga umesahau kama hashauriki; unalalamikia unafiki wakati wewe mwenyewe ni typical mnafiki mkubwa, wachumia tumbo nyie ndio mnatuharibia nchi yetu kwa kivuli cha kupambana na ubeberu. Jifunze sifa za kiongozi bora alafu ndio uje umlinganishe na huyo wako unayetaka kujishaua nae hapa. Shwain!!!
unapangua hoja badala ya kujibu hoja
 
Umeongea mambo mazito
Africa wanasiasa Wengi wanajipendekeza kwa Mabeberu wakidhani wanapendwa kumbe wanatumika kuharibu Nchi zao

Tumuunge mkono Magufuli kujenga Tanzania imara kwa ajili ya kizazi cha leo na kijacho
Kwani hakopagi nakupokea misaada kutoka huko ubeberuni
 
ulikua na point ila baada ya kutoka kweny point ukaanza kuwachambua vijana akili zikakutoka kabixaa na ukaonekana ww ndo mnafiki kwel kwel,hiv kama kiongoz hatakiw kuhojiwa kuendana na mienendo yake?kumbuka yy n binadamu na n lazma afuatu pia ushauri wa wenzake,ona man leadership ilikua kipnd cha uongoz wa kifalme,sas iv tu kweny reinnaissance,kipnd cha kuhoji na mtu kuja na hoja na c kulazimishana na kuonyesha ubabe majukwaan kutafuta fame,huyo unaemuona mzalendo alikua anakula nchi hii pamoja na hao anaowanadi kuwa n fisadi,ss mtu unashindwa kuelewa kua usalendo aliokua anatuhubiria mwalim Nyerere n huu wa kujitangaza majukwaan au kuwatumikia wananchi na kukubali kukosolewa pale inapobidi
 
Back
Top Bottom