Gurta
JF-Expert Member
- Sep 17, 2010
- 2,234
- 531
Nchi hii imejengwa katika misingi na sera za kijamaa -- sijui kama ilikuwa ni extreme form of it, lakini najua kitu kimoja. Siasa hizi zime-demonise dhana ya mtu binafsi (individual prosperity) kuwa na mali (utajiri).
Najiuliza, kwanini tumekuwa nchi ambamo hatuwezi kuamini kuwa inawezekana mtu kuwa tajiri? Kwamba ili kuwa tajiri lazima kuna 'siri chini ya kapeti'? (Tuta-speculate ndumba, rushwa, kujuana, kupendelewa, n.k.) Tumekuwa watu ambao hatutaki kuona kama kuna jitihada binafsi za watu katika kuchuma mali, hata katika kipindi hiki ambamo tumeshaikufuru siasa ambayo bado imo kwenye katiba ya nchi.
Kwa nini utajiri uwe 'dhambi' katika nchi hii?