Siasa za Trump na biashara za Ulaya

Siasa za Trump na biashara za Ulaya

bhikola

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,132
Reaction score
1,668
Wanasema joka ukililea ndani, ipo siku litakumeza.

Wakati US inaanza chokochoko na Russia, umoja wa Ulaya waliona sawa tu kwasababu wote wana visa au uadui na Russia.

Ilipokuja kwa Mchina, hawakushtuka sana kwasababu nao kwa upande mwingine kukua kwa China wanakuangalia kwa jicho la husda.

Mara ikaja issue ya Iran na mpango wa NUC. Hapa jamaa wakaanza kushtuka kidogo. Kwamba huyu jamaa anakoelekea siyo maana mkataba ule ulikuwa na maslahi kwao.

Sasa jamaa kawageukia na wao. Kuongeza kodi katika bidhaa za chuma na bati, ambazo ndizo hasa wanazopeleka zaidi US, kumeawaamsha.

Jambo la kufurahisha zaidi hapa ni kwamba, kwa upande mwingine, imewafanya umoja wa ulaya wakae karibu zaidi China ili waangalie jinsi ya kum-confront US.

Je, hatua hizi inaweza kuwa mwanzo wa mwisho ya dominance ya US kwenye ushawishi wa biashara ya kimataifa?

Je, Mnyukano huu, unaathari gani katika biashara na ustawi wa Afrika?
 
Aisee Trump noma anatwanga kotekote....ila hiyo nimeipenda....tunakoenda nchi za Ulaya zitaacha ujinga wa kukubaliana kunyanyasa nchi zingine kisa Marekani kasema...

Maana walikuwa wanashabikia kila ujinga unaofanywa na Marekani kisa wao hauwahusu.!
 
Mwaache apige kotekote na mshika mawili moja humponyoka, anang'ang'ana na vikwazo mrusi yuko bize kufanya biashara ya s- 400 sytem, India wana mpango wa kuyachukua kama ma 5 , Qatar naye anampango wa kuyachukua mshirika wake saud arabia katishia kuivamia endapo itanunua system hiyo. Naona mrusi anazidi kufanya biashara yeye anazidi kupiga mikwara ni njia mojawapo ya kupitwa mda si mrefu nafasi hiyo anakabidhi kwa wengine
 
vipi slaa hajakupa hajakuungisha kibarua ya kusafisha vyoo ubalozi wetu stockholm?
 
US want to control the whole world. While china and Russia are there are to strong enough
 
Greatest enemy of the world is USA.
Bila shaka nchi za Ulaya somo limeanza kuwaingia vizuri.

Na amedhihirishahilo kwa vitendo. Haiwezekani yeye ajione ni bora kuliko kila nchi, na ajione anaweza kufanya chochote bila yeye kuathirika. Kisa tu tchnolojia anazowauzia. Siyo muda mrefu ataisoma no.
 
Asipojiangalia kuiwekea vikwazo kila nchi atajikuta yeye ndo anajitoa kwenye line. Mfano saizi urusi hajali vikwazo vya marekani zile nchi zilizowekewa vikwazo na marekani, mrusi hachezi mbari nazo

Very well said,
Sasa ajiangalie sana kuhusu colabo ya Asian giants (China, Singapore, Malysia na India), na EU. Ikija ikatokea hiyo, jamaa atakuwa amepotea mazima. Kwasasa Africa hana share kubwa kivile, China kashika soko. Sasa akilipoteza la Ulaya na Asia, wakati huo huo kaharibu kwa majirani zake - Canada
 
Mwaache apige kotekote na mshika mawili moja humponyoka, anang'ang'ana na vikwazo mrusi yuko bize kufanya biashara ya s- 400 sytem, India wana mpango wa kuyachukua kama ma 5 , Qatar naye anampango wa kuyachukua mshirika wake saud arabia katishia kuivamia endapo itanunua system hiyo. Naona mrusi anazidi kufanya biashara yeye anazidi kupiga mikwara ni njia mojawapo ya kupitwa mda si mrefu nafasi hiyo anakabidhi kwa wengine

Mkuu vipi, unaona kuna athari zozote kwa biashara za africa? au siye hatuna cha kujivunia?
Kwasababu, kwa soko la Mashariki ya kati, wanauza zaidi silaha na teknolojia za kiulinzi. Lakini pia anaweza kuwa njiani kupoteza soko la Asia kwasababu ya kile wanachovutana na China.
Hapo ndipo Russia na China watakapomuona jamaa hamnazo kabisa
 
Trump akili yake inamtosha mwenyewe....yaani kwasasa rafiki wa kweli wa Trump na si Marekani ni Israel basi ikisema chochote anaisikiliza lkn wengine wote anawaona vichaa tu...[emoji2]
 
Mwacheni aangukie kisogo. Kwanza katuharibia Dunia yetu sana huyu mmarekani
 
Kwa Trump, USA kwanza.
Nawapa mfano wa hapa Tanzania. Viwanda vingi vimekufa kwa sababu ya uingizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi. Viwanda vya nguo, maziwa, sabuni vimeathirika sana. Hakuna sera inayoweza kulinda bidhaa zetu kisa WTO na mikataba ya kimataifa. Bila kulinda vuwanda vya ndani kwa makusudi kwa visingizio vya biashara ya kimataifa hakuna viwanda. Trump anataka kufufua sekta za chuma zilizodorora kwa sababu ya uingizaji wa bidhaa hizo nchini kwake. Nakubaliana nae sana ninapolinganisha na sera zetu.
 
Na amedhihirishahilo kwa vitendo. Haiwezekani yeye ajione ni bora kuliko kila nchi, na ajione anaweza kufanya chochote bila yeye kuathirika. Kisa tu tchnolojia anazowauzia. Siyo muda mrefu ataisoma no.
Namba atakuwa kaishaanza kuzisoma turkey kasema asipomuuzia ndege Su - 35 ataangalia pengine na pengine si nje ya urusi, hivyo tayari ni dalili za kuonyesha kuwa kuna nguvu mbili tofauti na hapo nyuma kidogo kila kitu alikuwa yeye, sazi watu wanakuwa na chaguo.
 
Si Su-35 mkuu ni F-35 unaposema Su ni Jamii ya ndege za kirusi hizo....
 
Back
Top Bottom