Nashindwa kuelewa siasa za Tanzania!!Pale chama fulani kinapopata mafanikio, migogoro inaanza. Nakumbuka mwaka 1995 chama NCCR mageuzi baada ya kupata mafanikio, kwa kupata majimbo mengi kwenye uchaguzi, Baada ya miaka mitatu migogoro ilianza ndani ya chama. ikionekana baadhi ya viongozi wanasaliti chama. Baada ya hapo chama kiligawanyika wengine wakaanzisha chama cha TLP kama JOGOO. Ikapelekea mwaka 2000 kwenye uchaguzi Chama cha NCCR mageuzi kikadolola na hatimaye kikaibuka chama cha CUF na ngangali. Leo tena baada uchaguzi 2010 baada ya kupata umaarufu na kupata majimbo mengi baada ya miaka mitatu baada ya uchaguzi migogoro imeanza ndani ya chama cha CHADEMA, inaonekana kuna viongozi ni wasaliti. Je Tanzania ni kweli kuna vyama vya upinzani?Au ndio tutegemee kama ya NCCR mageuzi kwenye uchaguzi wa mwaka 2000 yaliyotokea? Kwa hali ya migogoro hii mwananchi wa hali ya chini ataamini vipi kuwa tanzania kuna upinzani? Au CCM inatumia mbinu kama iliyotumia baada ya uchaguzi 1995 kuimaliza NCCR mageuzi? Utafiti wa hali ya juu unahitajika ili tufikie siasa ya kweli. Kila chama lazima kuwe na magroup na hata katika maofisi ya kazi watu wanamagoup. Bila hekima na busara tanzania hatutapata mabadiliko ya chama tawala mapema. Napenda mabadiliko. Kwenu wadau!!!!!!!!!