Kishoka2
Member
- Aug 23, 2017
- 16
- 13
Siasa za leo nyingi ni siasa uchwara, siasa za kuchafuana majina, siasa za kutukanana, siasa za kukashifiana. Siasa gani hizi zinawatenganisha watu katika jamii? Siasa hizi zinawafanya watu wasiombane chumvi, ni siasa gani hizi?
Siasa hizi wengine wanaziita siasa za maji taka, ni maji taka kweli. Watu bila hofu hutajana kwa majina na kupeana sifa chungu mbovu. Siasa gani hizi za kushambulia wanadamu wengine kwa mabunduki? Hizi ni siasa ngeni Tanzania yetu hii.
Wengine wanatumia mitandao kuchafua na kusambaza taarifa zisizo thibitishwa. Mara yule kafanya hivi, yule kafanya vilee. Haitusaidii hata kidogo kama watanzania kufikia malengo ya kukua kiuchumi. Watanzania wengi bado ni maskini, tunahitaji maendeleo. Sio brahbrah tu kila uchao.
Watu wengine bila haya wala aibu wanaliibia taifa au kushirikiana na wezi kutoka mataifa yaliyoendelea, hakika hii ni aibu sana.
Wacha tu niishie hapahapa...