Siasa za siasa: Kafulila ni kichwa jamani

Siasa za siasa: Kafulila ni kichwa jamani

Njanga Tz

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2015
Posts
843
Reaction score
655
Aisee yani nimekaa na bosi wangu tumebaki kushangaa uwezo mkubwa wa huyu jamaa. Anajua na anachambua mambo kwa uzuri sana kafanya tustop kufanya kazi.

Kumbe nchi haiendelei kwasababu ya vitu vidogo tu.

Kubwa zaidi ni hili; Makampuni ya simu na madini yawekwe kwenye soko la hisa ili mitaji yao ijulikane na wa Tanzania wapate fursa yakumiliki hisa sheria ipo ila kanuni wamegoma kuzitengeneza.

Hongera Carol kipindi kilikua hot na kizuri sana
 
ukawa tumesha pata replacement wa zito
 
kafulila ni kichwa maji yule hana lolote,kazi yake kupayuka tu! nimesoma naye shybush na tumemaliza naye f6 2004,ni kilaza mkubwa na ni mtu wa kukurupuka,anataka kuhamia act eti...!

Hongera kwa kusoma ma Mkombozi wa Taifa.....

Kilaza kaingia kwenye historia iliyotukuka ya taifa lako, wewe kipanga una kipi cha kujivunia?

Uandishi wako tu unadhihilisha wewe siyo kilaza tu bali uharo wa homa ya kali ya ngoma.
 
Hongera kwa kusoma ma Mkombozi wa Taifa.....

Kilaza kaingia kwenye historia iliyotukuka ya taifa lako, wewe kipanga una kipi cha kujivunia?

Uandishi wako tu unadhihilisha wewe siyo kilaza tu bali uharo wa homa ya kali ya ngoma.

Eeeh...asante!
 
Wakulima Tanzania ni 70%, hivyo basi kikwete anaposema hakufanikiwa kwenye idara hii ya watanzania walio wengi ni sawa na kusema hajatatua tatizo la Umasikini ndani ya watanzania.
Ikumbukwe hata Mkapa alishindwa kuendeleza idara hii ipasavyo.

Hongera sana mh. D. KAFULILA
 
nilitamani waongezewe muda yaan nondo tamu saana nilikuwa nachukua notes daaah
 
kafulila ni kichwa maji yule hana lolote,kazi yake kupayuka tu! nimesoma naye shybush na tumemaliza naye f6 2004,ni kilaza mkubwa na ni mtu wa kukurupuka,anataka kuhamia act eti...!

Yeye yuko Bungeni wewe uko wapi? Acheni tabia za kubeza watu bila sababu. Tujenge utamaduni wa kukubaliana na wanaotuzidi maana wakati mwingine utajifanya kushindana na mtu mwenye kipaji utaumia wewe tu.

Nikiachana na wewe.....Mimi kafulila namwona kama mtu anayesukumwa na uzalendo. Hizi ni tabia za watu wazelendo yaani kuipenda nchi yako. Ningetamani sana uwepo mdahalo kati ya Kafulila na Nape, hata wakipewa mada inayohusu taifa stars itatosha watu tuburudike.
 
Huyu bwana nilikuwa simfatilii.Nilimsikiliza kipindi kimoja cha dakika 45 ITV nilishangaa sana alivyomuelewa wa mambo.Jamaa yuko sawasawa.
 
Njanga Tz

Mitaji yao ikijulikana yeye anapata nini? Bora angewaomba nyie pia mnunue hisa, kama anataka kujua mitaji si awaulize wenye kampuni kuliko kuzunguka
Kama yeye kichwa basi we na bosi wako mtakuwa sijui sehemu gani ya mwili, , Soko la Hisa sio sawa na mahakama ya ndizi kila mtu anaenda.
 
Last edited by a moderator:
Huyu bwana songambele naona yuko tofauti sana na jina lake analojipambanua nalo
Nadhani nitakuwa sijamkosea nikimwita Songanyuma,
Kwanza kabisa hajui chochote kuhusu soko la hisa ndiyo maana anasema siyo sawa na mahakama ya ndizi.
Cha kujiuliza hisa ni nini?
Hisa ni uhalali wa kumiliki sehemu ya kampuni kutegemea na uwezo wako wewe, unaweza kuwa na hisa za shilingi elufu Tano tu za CRDB BANK, nawe utakuwa ni sehemu ya wamiliki wa CRDB BANK
Kwa hiyo Elimu inahitajika kwa watu kama huyu nakutakia tafakuri njema ila nitoe angalizo kabla ya kuchangia tafakari kama una uwezo nalo.
 
Back
Top Bottom