Siasa za matokeo K4 mwaka 2012

Siasa za matokeo K4 mwaka 2012

tz-insider

New Member
Joined
May 13, 2013
Posts
1
Reaction score
0
Republicans wa Tanzania wanafanya kila linalowezekana kutengeneza mgogoro wa matokeo ya K4 kisiasa ili tu kumpaka matope Obama (sic JK)

Wamefeli vijana wetu nchi nzima, majimbo ya CCM CUF na Chadema, wamefeli sio mwaka huu pekeyake, wameanza kufeli miaka mitano iliyopita baada ya upanuzi mkubwa wa elimu. Lakini leo, Republicans wamepata Benghazi yao, mara Kawambwa atoke, mara Mulugo aanze, kama kweli tunataka kuwajibika basi kila Mheshimiwa ambaye jimbo lake wamefeli aachie ngazi! Ili iwe haki bin haki. Aanze Zitto, afuatie Serukamba, Rage, Mwigulu, Mbowe, Lisu na asibakie yeyote. Nyote mmeshindwa kazi tuliyowatuma, mpo Dar na siasa majimboni tunafeli. Nendeni na Waziri wenu, hai na kivuli.

Kwenye hili binafsi naona kinachotakiwa ni kuwatendea haki hawa vijana kama mlivyoshauriwa na TUME. Hamjui nyie nini maana ya kuwa na kijana mwenye D moja kwa sababu tu huko juu mmeamua kujaribu njia mbadala. Mbona hamkutumia huo mbadala mwaka jana, juzi au 2010? Pisheni au achieni ngazi wote maana mmetusaliti.
 
Back
Top Bottom