Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
"Binadamu tunajua mengi. Asiyejua hili anajua lile. Hata hivyo kama kila anayejua atakuwa akikisema kila anachokijua kumuambia yeyote, mahali popote kwa madhumuni yeyote yale hata kama ni mazuri, tutajishusha katika hadhi duni mno kana kwamba hatukupewa akili hata kidogo".
Demokrasia na uhuru wa mwanadamu kwa ujumla wake una misingi yake.Hilo ni jambo linalofahamika dunia nzima na kuzingatiwa na jamii ya watu wote waliostaarabika. Kadhalika wanadamu tumepewa akili ili tuweze kutathmini mambo kulingana na wakati na mazingira.Kufikiri kwamba kwa sababu ya demokrasia na uhuru wa mtu, basi anaweza kufanya au kusema chochote kwa yoyote na mahali popote na kufikiri kuwa huo ndio utarajibu unaoweza kuleta tija kwa mtu binafsi au kwa taifa ni kukosa uzalendo na kuamua kutokuwajibika.
Unaweza ukawa unaongea ukweli au unatoa ushauri wa maana lakini kama utautoa kwa hadhira isiyostahili, au kwa namna isiyostahili, jambo unalolifanya haliwezi kuwa na maana yeyote. Kwa mfano: kama wewe ni mwanamke na mumeo haogi wiki nzima, unafikiri ni kila mtu anapaswa kulijua hilo kwa kuwa una uhuru wa kuongea na kutoa habari na kwa sababu hiyo unatakiwa umuenye kupitia media? unafikiri utakuwa umeisaidia familia!
Hivi ni mantiki gani inayofanya isikubalike kutoa mambo ya ndani nje ya nyumba au mambo ya kikao chochote nje ya kikao n.k?Nafikiri mantiki ni kwamba ni kwa kuwa si kila ambacho mtu anakijua ni lazima akiseme na si kila mtu anayepaswa kuambiwa kila kitu , popote na wakati wote! au sio?.
Katika level , ya nchi ni vivyo hivyo kwamba pamoja na demokrasia na uhuru wetu, ni lazima Watanzania tuangalie kama tunayoyasema yana umuhimu wa kusema, tunasemea sehemu sahihi, na tunaowaambia ndio tunaotakiwa tuwaambie? vinginevyo tunaweza kujikuta tunawalaumu wengine kwa kutokutimiza wajibu wakati nasi ni sehemu ya wasiotimiza wajibu.Nafikiri kuna aina ya mambo hayahitaji siasa.Hata kama una hitilafu na Mumeo au mkeo, si kila kitu cha familia unatakiwa kuelezea wanakijiji hata kama unajua mengi (ya sebuleni hadi chumbani).Na wala haupaswi kusema kwa kuwa tu una fursa au mdomo wa kusemea bali kwa kuwa ufanyavyo ndiyo ikupasavyo kufanya.
Demokrasia na Uhuru wetu ni lazima uendane na Uzalendo na wajibu wetu na muda kidogo wa kufikiri kabla ya kutenda jambo ni bora kuliko kufanya fatiki ya mwaka mzima.Kama watanzania tunataka maendeleo ya maana, ni lazima tujijengee utamaduni wa kuchukua hatua sahihi, wakati sahihi, mahali sahihi na kwa watu sahihi.Kinyume chake hakuna kitu.