Siasa za kitoto zinatutia hasara sanaa

Siasa za kitoto zinatutia hasara sanaa

666 chata

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
1,710
Reaction score
4,044
Kumekuwepo na hama hama za wabunge kutoka chama flani kwenda chama flani, sababu kubwa ikikisiwa kua et wamemkubali Rais, na japo kuna stori za chini ya kapeti ambazo sio rasmi zinadai kumekuwepo na ununuzi wa watu hao au kubanwa kwenye biashara zao na vitisho vingi, sasa sisi wananchi hatuna shida na maamuzi yao na makubaliano yao, ila tunataka tu kuwakumbusha tu kuhama kwao kwa sababu za kawaida na za kitoto kama hizo zinatutia hasara kubwa sanaa.

Uchaguzi mmoja wa jimbo unaweza kugharimu mpaka bilion 5 kwa estimation za kawaida, pesa ambayo inaweza kujenga mahospital na mashule kadhaa kwenye jimbo husika, au kukarabati na kujenga barabara za jimbo kwa kiwango kizuri sanaa.

Tunawaomba wabunge wote wamkubali rais ili tusave pesa muda au basi wamkubali wakiwa huko huko kwenye vyama vyao na sidhani kama wananchi tutawaelewa vibaya.

Na wale wanaotuhumiwa kununua hao wanao hama wakumbuke tu kua wanafanya kazi bure wenye maamuzi ni sisi wananchi na kamwe hatuwezi kubadilisha misimamo yetu ya kisiasa et kisa mbunge kabadilika basi ata tu win na sisi, no hawatofanikiwa. Wananchi wa sasa wanajua karibu kila kitu kinavyoendelea hakuna jipya.

NEC andaeni mpango hawa wanaojiuzuru kwa njia za namna hii basi wajue kabisa hakutakua na uchaguzi mwingine mpaka 2020, walio wengi hawana impact kwenye majimbo yetu yaani wawepo au wasiwepo ni sawa tu.
 
Mwenye nchi yupo mbinguni we ndo unajifanya mwenye nchi...pambaneni na hali zenu
 
Umeongea point sana,
Ila hizo siasa ulizosema za kitoto wenzio ndio wanazipena sana,
Wanawaza kukomoana tu badala ya kujenga nchi
Tumechoka mkuu, mtu hawezi kututia hasara ya mabilion kwa kauli yake ya kipuuzi kabisa et ana hama chama kumuunga mkono rais.
 
Alipojiuzulu nyalandu hatukusikia uharo huu,hapa ndii utaona ubovu wa akili za wapinzani wa nchi hii
Yaani mtu akitoka ccm huyo hakufanya utoto,ila akihama upinzani inakua nongwa
 
Alipojiuzulu nyalandu hatukusikia uharo huu,hapa ndii utaona ubovu wa akili za wapinzani wa nchi hii
Yaani mtu akitoka ccm huyo hakufanya utoto,ila akihama upinzani inakua nongwa

Sisi wapinzani wa ukweli tumemponda sana na tumewashangaa cdm kumpokea mtu wa aina yake. Hatujaishia hapo sasa hivi tunaendesha kampeni ya kuhakikisha wapinzani wasijisihusishe na upigaji kura. Huu ni upuuzi wa kiwango cha juu, nchi inaendeshwa kwa mikopo ya kimyakimya huku mchezo wa kipuuzi wa kuendesha uchaguzi hatarishi kwa maisha ya wananchi ikishika kasi.
 
Mbona enzi za JK hii hamahama ilikuwa hamna?inaelekea mwenye boma wa kipindi hiki hajiamini,!!anatumia garama kununua upendo.!!?
Sasa hivi tumepatikana ndugu yangu, huyu wa sasa ni bure sanaaa na hana vision yoyote zaidi ya uoga tu.
 
Sisi wapinzani wa ukweli tumemponda sana na tumewashangaa cdm kumpokea mtu wa aina yake. Hatujaishia hapo sasa hivi tunaendesha kampeni ya kuhakikisha wapinzani wasijisihusishe na upigaji kura. Huu ni upuuzi wa kiwango cha juu, nchi inaendeshwa kwa mikopo ya kimyakimya huku mchezo wa kipuuzi wa kuendesha uchaguzi hatarishi kwa maisha ya wananchi ikishika kasi.
Very true mkuu.
 
Back
Top Bottom