Siasa zina wakati wake...
Hiyo ndio maana yao...
Siasa ni wakati wa uchaguzi wakti huu mwingine watu wajenge nchi...
Hawajalataa siasa, ila ni wakati gani unafanya siasa? Hilo ndilo tatzo kwao.....
Siasa hazina wakati maalum. Siasa kwa mwananchi ni sawa na hewa kwa mwanadamu.
Kama unakubaliana na dhana ya siasa ina wakati wake basi hata kwenye hii thread basi ulikuwa huna haja ya kuingia. Hii ni thread ya siasa, labda umesahau, nakukumbusha.
Kukataza siasa kwa kisingizio uchaguzi umeisha, ni sawa na kukataza kutumia choo kwenye bar.
Ukilalamika mfumuko wa bei, ni siasa
Ukilalamika matibabu duni, ni siasa
Ukilalamika elimu dhaifu, ni siasa
Ukilalamikia, miundombinu, ni siasa
Ukilalamikia, ongezeko la mshahara, ni siasa
Kama tusifanye siasa basi na bunge livunjwe baada ya uchaguzi, in fact, lisiwepo.
Kama tusifanye siasa baada ya uchaguzi basi wabunge wasiwe na vyama baada ya uchaguzi
Kama tusifanye siasa basi ipigwe marufuku mavazi yote yanayoashiria chama cha siasa.
Kama tusifanye siasa baada ya uchaguzi, ruzuku za vyama vya siasa zifutwe baada ya uchaguzi.
Politics does not begin in Apr and end in May
Politics is for yesterday, today, tomorrow & everyday.
Mimi mwenyewe si muumini wa siasa za mkusanyiko wa maelfu wa watu wakati ujumbe ungeweza kufika kwa kutumia media. Lakini hili liwe kwa wote sio kwa upinzani tu.