Siasa za kihuni hazitajenga Tanzania

Siasa za kihuni hazitajenga Tanzania

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,176
Reaction score
48,460
Hata siku moja hatutafanikiwa kuijenga nchi yetu iwe imara kiuchumi na kijamii kwa kutegemea siasa za kihuni. Siasa ndiyo kila kitu kwenye maisha ya binadamu ingawa si kila binadamu anakuwa kwenye mfumo wa kisiasa!

Waliomo kwenye mfumo wa siasa (wanasiasa) ndiyo hasa wanaopanga mambo ya maendeleo kwa niaba ya wananchi wenzao ambao hawamo kwenye mfumo wa siasa. Lakini hapa Tanzania kumeibuka siasa za kihuni kwa baadhi ya wanasiasa kujifanya wao si wanasiasa bali wapinzani wao ndiyo wanasiasa.

Wakati mwingine utasikia "Hapa hatutaki siasa" au "siasa hazituletei chakula, elimu, matibabu au barabara" Lakini labda anayesema hivyo ni Rais, Waziri, Mkuu wa Mkoa au Wilaya, Meya au Mwenyekiti wa Halmashauri, Diwani na hata Mwenyekiti wa Mtaa, lakini hawa wasiotaka siasa si ndiyo wanasiasa wenyewe?

Yaani mwanasiasa anaposema hataki siasa si unakuwa uhuni? Ni kama vile Golikipa anamwambia fowadi wa timu pinzani hapa hatutaki kufungana kwani kufungana hakuleti furaha, hakuleti mvua wala siyo pumzi, lakini kwa nini Golikipa yupo uwanjani kama kufungana hakuleti yote hayo?

Je, mtu akichaguliwa kwenye nafasi hizo nilizotaja hapo juu za utumishi wa umma anakoma kuwa mwanasiasa? Kama anakoma kuwa mwanasiasa basi ni kwa nini Katiba ya nchi yetu inatambua kuwa chama cha siasa kikimnyang'anya Mbunge, Diwani, au Mwenyekiti wa Mtaa kadi ya chama husika mtu huyo anakoma kuwa kiongozi wa ngazi husika. Inakuwaje wasio wanasiasa utumishi wao ukomeshwe na chama cha siasa?
 
Siasa zina wakati wake...
Hiyo ndio maana yao...
Siasa ni wakati wa uchaguzi wakti huu mwingine watu wajenge nchi...
Hawajalataa siasa, ila ni wakati gani unafanya siasa? Hilo ndilo tatzo kwao.....
 
wanaposema wanatekeleza Ilani ya chama chao haiwi siasa? Soma vizuri halafu tuambie ni wakati gani wa kujenga nchi bila siasa. Hivi unajua sera zote zinazotungwa ni siasa?
 
Hata siku moja hatutafanikiwa kuijenga nchi yetu iwe imara kiuchumi na kijamii kwa kutegemea siasa za kihuni. Siasa ndiyo kila kitu kwenye maisha ya binadamu ingawa si kila binadamu anakuwa kwenye mfumo wa kisiasa!

Waliomo kwenye mfumo wa siasa (wanasiasa) ndiyo hasa wanaopanga mambo ya maendeleo kwa niaba ya wananchi wenzao ambao hawamo kwenye mfumo wa siasa. Lakini hapa Tanzania kumeibuka siasa za kihuni kwa baadhi ya wanasiasa kujifanya wao si wanasiasa bali wapinzani wao ndiyo wanasiasa.

Wakati mwingine utasikia "Hapa hatutaki siasa" au "siasa hazituletei chakula, elimu, matibabu au barabara" Lakini labda anayesema hivyo ni Rais, Waziri, Mkuu wa Mkoa au Wilaya, Meya au Mwenyekiti wa Halmashauri, Diwani na hata Mwenyekiti wa Mtaa, lakini hawa wasiotaka siasa si ndiyo wanasiasa wenyewe?

Yaani mwanasiasa anaposema hataki siasa si unakuwa uhuni? Ni kama vile Golikipa anamwambia fowadi wa timu pinzani hapa hatutaki kufungana kwani kufungana hakuleti furaha, hakuleti mvua wala siyo pumzi, lakini kwa nini Golikipa yupo uwanjani kama kufungana hakuleti yote hayo?

Jee mtu akichaguliwa kwenye nafasi hizo nilizotaja hapo juu za utumishi wa umma anakoma kuwa mwanasiasa? Kama anakoma kuwa mwanasiasa basi ni kwa nini Katiba ya nchi yetu inatambua kuwa chama cha siasa kikimnyang'anya Mbunge, Diwani, au Mwenyekiti wa Mtaa kadi ya chama husika mtu huyo anakoma kuwa kiongozi wa ngazi husika. Inakuwaje wasio wanasiasa utumishi wao ukomeshwe na chama cha siasa?
Kero kero kero jamani,serekali, hawa watu wanaoitwa (MAJEMBE) je ni mahakama wameshindwa kazi wakawapa ruhusa au wamesomea wapi huwatesa wananchi,tunahamu ya kujua hiyo ni degree ya aina gani wamechukua.kweli tunaomba serekali ipige marufuku kabisa hawa wat,wawaachie mahakama wafanye hizo kazi ni sehemu ya kazi zao,maana hao majembe wenyewe ni wezi wezi wakubwa,wananchi wanateseka.hawajui pa kuanzia.
 
wanaposema wanatekeleza Ilani ya chama chao haiwi siasa? Soma vizuri halafu tuambie ni wakati gani wa kujenga nchi bila siasa. Hivi unajua sera zote zinazotungwa ni siasa?
Unapotekeleza ilani ya chama maana yake unatekeleza kile ambacho uliwahaidi watu wako nini utawafanyia hadi wakakupa kura.
Kwahiyo unawafanyia maendeleo yale uliyowaambia utawapa...
Kwahiyo hapo tunaizungumzia serikali... Ambayo inaundwa na chama fulani.....
 
Hicho chama fulani ni cha siasa si cha siasa?
 
wanaposema wanatekeleza Ilani ya chama chao haiwi siasa? Soma vizuri halafu tuambie ni wakati gani wa kujenga nchi bila siasa. Hivi unajua sera zote zinazotungwa ni siasa?
wanaposema wanatekeleza Ilani ya chama chao haiwi siasa? Soma vizuri halafu tuambie ni wakati gani wa kujenga nchi bila siasa. Hivi unajua sera zote zinazotungwa ni siasa?
Unajua kipindi cha uchaguzi vyama vyote vinaandaa sera zinatoa twasira kuwa kama chama hicho kikipata ridhaa kitatekeleza. Baada ya uchaguzi inabidi chama kilichopata ridhaa serikali inayoundwa inafanya chini juu kuandaa mipango ya muda mrefu na mfupi kuteleza ilani ya chama kilichoshika dola. Kazi kubwa ya upinzani ni watchdog na kueleza palipo mapungufu kuwa ingekuwa wao wangefanya hivi ilikuleta mafanikio. Cha msingi ni vyama vyetu kuelewa kila kitu wanachokifanya ni kwa maslahi ya taifa hill.
 
Hicho chama fulani ni cha siasa si cha siasa?
Ni cha siasa..
Ila hapo hakiwi katika majukwaa, bali huwa katika maovisi kikitenda kile kinachotakiwa kufanywa ili kufanikisha kile walichokiahidi kwa watu..
Na hapo mdipo tunaposema maendeleo....
Sio kila siku za mwaka mnakiwa katika mjukwaa kulumbana kuhusu hili na lile...
Hapa kati tunashirikiana wanachama wa vyama na wasiokuwa na vyama pamoja na serikali yao ili kuleta maendeleo ya Taifa letu....
 
nyanzaki hicho chama kinachoshinda kinaruhusiwa kutumia dola kugandamiza wapinzani wao kisiasa? Kwa mfano Rais anahutubia anamkaribisha Mwenyekiti wa Mkoa kuhutubia katika mkutano unaorushwa kwenye tv ya Taifa kwa kodi ya wananchi, jee wapinzani nao watapewa fursa kama hiyo siku ingine?
 
Unajua kipindi cha uchaguzi vyama vyote vinaandaa sera zinatoa twasira kuwa kama chama hicho kikipata ridhaa kitatekeleza. Baada ya uchaguzi inabidi chama kilichopata ridhaa serikali inayoundwa inafanya chini juu kuandaa mipango ya muda mrefu na mfupi kuteleza ilani ya chama kilichoshika dola. Kazi kubwa ya upinzani ni watchdog na kueleza palipo mapungufu kuwa ingekuwa wao wangefanya hivi ilikuleta mafanikio. Cha msingi ni vyama vyetu kuelewa kila kitu wanachokifanya ni kwa maslahi ya taifa hill.
Uanchokisema ni sawa kabisa.
Na hapo ndipo wakaliunda BuNGE, ambako mawazo na mipango ya maendeleo kutoka kwa watu wa serikali pamoja na hawa mawatchdog ( wapinzani ) yanakotolewa kwa utaratibu nzuri kabisaaaaa ili kuleta maendeleo ya nchi yetu.
Na pale walioko serikalini wakikosea, basi hawa mawatchdog wanakosoa kwa hoja na kutoa altenatives za namna bora ya kuboresha hapo walipokosea ili kuenda sawa kwa mustakali wa nchi yetu.
Ila unapokwenda kubishana, kukejeri na kutukana katika majukwaa, hapo ndipo tunaposema siasa wakati wa kujenga nchi sio nzuri...
Tushirikiane ( serikali na wapinzani ) ili kujenga nchi na sio kulumbani na kukejeriana na kutishiana na Kuumizana katika majukwaaaa...
Hayo mambo tunayategemea wakati wa uchaguzi tuuuuuuu....
Nafikiri hilo ndio hasa wazo la hao wanaosema sio wakati wote ni wa siasa,,,...
 
Magufuli sina matatzo naye kwani yye huwa ni Raisi ni mtendaji.
Huwa anatembelea watu wake na kuongea nao. Kwa kiwa wanakuwa wengi lazima atumie majukwaa kuwaeleza hawa watu nini atakifanya au nini kakifanya kutoka katika yale aliyowahaodi watu wake....
Ila tatzo langu kwake ni NINI ANAKIONGEA AKIWA HUKO JUKWAANI..
PIA NACHUKIA SANA NINAPOONA KIONGOZI WA SERIKALI KAMA RAISI ANAPOKUJA SEHEMU, WATU WANENDA NA SARE ZA VYAMA... HUWA NACHUKIA SANA KWANI HAPO WANAMAANISHA KAMA VILE AMEKUJA KUHUTUBIA WANACHAMA BADALA YA WANACHI AMBAO WENGINE HAWANA VYAMA NA WENGINE NI WAPINZANI...
kwahiyo, Magufili kuwa katika majukwaa sina tatzo nalo, ila labda nini anakiongea ndio tatzo....
 
Siasa zina wakati wake...
Hiyo ndio maana yao...
Siasa ni wakati wa uchaguzi wakti huu mwingine watu wajenge nchi...
Hawajalataa siasa, ila ni wakati gani unafanya siasa? Hilo ndilo tatzo kwao.....
Unakubaliana na hii dhana?
 
Kwa mie naona iko sawa...
Ila sio kuwakataza wasiokuwa wabunge kuendelea na mambo ya kijenga chama.
Waruhusiwe watu kufanya VIKAO katika sehemu tofauti na kila mtu na chama chake na kwa wakati wake,.
Ila wakati huo wale waliopata bahati kutuwakilisha kule BUNGENI waendelee na mambo ya kuishauri serikali namna bora ya kujenga nchi yetu....
Wapunguze kashfa na maneno ya kejeri kwa kila mtu..
 
nyanzaki hicho chama kinachoshinda kinaruhusiwa kutumia dola kugandamiza wapinzani wao kisiasa? Kwa mfano Rais anahutubia anamkaribisha Mwenyekiti wa Mkoa kuhutubia katika mkutano unaorushwa kwenye tv ya Taifa kwa kodi ya wananchi, jee wapinzani nao watapewa fursa kama hiyo siku ingine?

Haya yote ni kuzunguka tu. Ukifanya homework yako ukaenda kijijini kwa mtu flani ukaongea na wazee wakupe historia ya baba na babu utashika kichwa. Sheria ya mtandao inabana
 
Siasa zina wakati wake...
Hiyo ndio maana yao...
Siasa ni wakati wa uchaguzi wakti huu mwingine watu wajenge nchi...
Hawajalataa siasa, ila ni wakati gani unafanya siasa? Hilo ndilo tatzo kwao.....
Ninamashaka na ufahamu wako post IPO wazi kabisa hapo ww hujaelewa.
 
Killerman Magufuli hafanyi mikutano sasa hivi na kwenye mikutano hiyo wana CCM na viongozi wao si ndiyo wamekuwa wanajazana. Hayo siyo majukwaa. Kwenye hiyo mikutano nchi inajengwaje?

SEHEMU, WATU WANENDA NA SARE ZA VYAMA... HUWA NACHUKIA SANA KWANI HAPO WANAMAANISHA KAMA VILE AMEKUJA KUHUTUBIA WANACHAMA BADALA YA WANACHI AMBAO WENGINE HAWANA VYAMA NA WENGINE NI WAPINZANI...
kwahiyo, Magufili kuwa katika majukwaa sina tatzo nalo, ila labda nini anakiongea ndio tatzo....
Ninamashaka na ufahamu wako post IPO wazi kabisa hapo ww hujaelewa.

Mtoa post na mimi hatujakashfiana tangia chati zetu..
Wewe ulitakiwa kunielewesha kama unaona mimi sijaelewa....
Sio unakuja na maneno hayo..
Nieleweshe wewe, huo ndio mtazamo wangu...
Na usitake kila mtu aelewe vile wewe unataka.....
 
Siasa zina wakati wake...
Hiyo ndio maana yao...
Siasa ni wakati wa uchaguzi wakti huu mwingine watu wajenge nchi...
Hawajalataa siasa, ila ni wakati gani unafanya siasa? Hilo ndilo tatzo kwao.....
Na huo wakati ni sasa, sio kesho wala.keshokutwa. Siasa ni maisha kama hujui.
Rais aliyeko madarakani ametokana na siasa. Anatekeleza ilani ya chama cha siasa na sera za chama cha siasa. Alipotembelea baadhi ya mikoa hivi karibuni alichokuwa anafanya ni siasa.
Katika maendeleo tunahitaji ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora. Hakuna namna ya kukwepa siasa.

Tatizo letu tunaipa siasa tafsiri finyu sana. Kwamba ni kuandamana na kufanya mikutano ya kampeni basi.
 
Siasa zina wakati wake...
Hiyo ndio maana yao...
Siasa ni wakati wa uchaguzi wakti huu mwingine watu wajenge nchi...
Hawajalataa siasa, ila ni wakati gani unafanya siasa? Hilo ndilo tatzo kwao.....
sasa kama unadhan pakiwa na wakati maalum wa kfanya siasa , je vyama vitapataje wanachama na je kwa namna gn vitaimarika na kukua? siasa ni kazi kama kazi tuzifanyazo donot tell me such stuff asee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom