Siasa za chuki, uonevu na kubambikiana kesi matukio yaliyokosa wa kusuluhisha

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Wadau nawasalimu.

Lengo la maada hii ni kutaka kuwataadhalisha viongozi wetu juu ya hizi chuki za kisiasa zinazoendelea kujengwa na CCM hasa toka awamu ya 5 iingie madarakani.

CCM imekuwa inatumia nguvu kubwa ya kifedha na vyombo vya ulinzi na usalama kuwatendea visivyo wapinzani,tumeshuhudia ununuzi wa wapinzani,uuaji ,utekaji,kubambikiziwa kesi kufungwa kukamatwa kwa wapinzani kila kukicha ni polisi magereza na mahakama na wapinzani.

Tumeshuhudia uchaguzi wa hovyo kupata kutokea toka nchi imepata uhuru. Tumeshuhudia bunge la hovyo toka kupata uhuru bunge lenye wabunge wasio na chama wanaapishwa na rais analihutubia.

Tumeshuhudia tume ya uchaguzi ya hovyo tume badala ya kusimamia uchaguzi inavuruga uchaguzi.

Tumeshuhudia vyombo vya ulinzi na usalama vikisimamia mateso na uonevu kwa wananchi hasa wapinzani.

Mateso na uonevu huu ungeweza kumalizwa na baba wa taifa kama angewepo mbadala wake.

Niwakumbushe kidogo

Mwaka 1995 wakati augustino mrema anagombea urais wananchi walikuwa wanambeba na kulisukuma gari lake.

Polisi kuona vile wakaanza kuwapiga mabomu wananchi lakini busara za hayati baba wa taifa aliwakataza ccm na polisi kuwazuia wananchi kumbeba kiongozi wao.

Najiuliza haya yanayotendwa na CCM na vyombo vya ulinzi na usalama kwa wapinzani nani anaweza kuyazuia na nchi haina baba wa taifa?

Marais wastaafu hivi kweli hawauoni uonevu huu wanaotendewa wapinzani?

Hivi viongozi wa dini hawaoni huu ubambikiwaji kesi na kamata kamata za polisi kwa wapinzani?

Naomba marais wa staafu licha ya kuwa CCM ni chama chenu

Hebu kuweni sehemu ya upatanishi ili kukomesha hizi chuki uonevu,utesaji na kubambikiana kesi

Kumbukeni mungu atataka kujua kama mlikuwa wapatanishi ktk uhai wenu mtamjibu nini?

Ushauri:
Ni vema taifa likawa na kamati ya upatanishi itakayokuwa ni chombo cha kusimamia amani na haki pale inaonekana upande mmoja unahatarisha amani na haki kwa nchi na wananchi wake.

Na pia kiwe na uwezo wa kukemea kuonya na kuheshimika na wananchi na viongozi wote.
 
Maraisi wastaafu wapo kujipendekeza kwa mtawala ili kuwatengenezea watoto wao njia ya kuukwaa Urais,tuliona hivyo kwa Mzee Mwinyi alivyojikomba kwa dhalim kumtengenezea njia mwanawe na mwisho wa siku akafanikiwa
 
Back
Top Bottom