Siasa za Chuki huwa ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa za Chuki huwa ni nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by QUALITY, Mar 25, 2011.

 1. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tangu uchaguzi kuisha mwaka jana, kuna sentenssi zimeibuka na zinatumiwa na wana siasa na viongozi wa serikali kusema kuna "Siasa za Chuki". Ambapo ukisikia malalamiko hayo, ujue kuwa wahusika wameisema serikali iliyoko madarakani au CCM. Swali linakuja, Je Siasa za chuki na siasa zisizo za chuki ni zipi?
  Nawasilisha
  :teeth:
   
 2. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ukibwatukia maslahi yangu kisiasa kwa nini nisikubandike una siasa za chuki?
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  [​IMG] JF Senior Expert Member [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]


  Join Date : 14th November 2010
  Posts : 2,110
  Thanks 100 Thanked 402 Times in 248 Posts

  Rep Power : 25


  [​IMG] Re: CUF -- kwa nini siku hizi mnafanya mikutano yenu vichochoroni?

  [​IMG] Originally Posted by only83 [​IMG]
  Nikikuwa nachat na Mtatiro kupitia facebook,jamaa kachoka yani kapotea njia lakini jinsi ya kurudi anashindwa anaona aibu.....wale wakristo mnamkumbuka farisayo Nicodem aliyekwenda usiku kumuuliza maswali Yesu maana aliogopa macho ya watu mchana...Mtatiro ashauriwe jamani.Hope wapo hapa wanaJF waliosoma nae pale UDSM anaweza kuwasikiliza.......................

  WABUNGE NA VYAMA VINAVYOTAMANI KUHESABIWA UMAKINI TANZANIA:
  TAFUTENI HARAKA ELIMU SAHIHI JUU YA MAANA, CHANGAMOTO NA USHIRIKI WA MAFANIKIO NDANI YA MFUMO MPYA WA 'SIASA ZA USHINDANI' ILI MUENDELEE KUMUDUU NA KUDUMU

  Ingawaje mwenye kutundika thread hii katusababishia wengi kucheka mbavu kuuma lakini baada ya kicheko ni wazi kwamba kuna mambo mengi sana ambayo watu na vyama, kama washiriki, kwa bahati mbaya hawajagundua kwamba tayari yamebadilika kabisa na kamwe hayatokaa yarudi kuwa kama zamani kisiasa nchini.

  Kweli ni masikitiko makubwa sana kwamba watu wengine hufikiria kwamba mtu unaweza tu ukaingia kwa jambo lililoitwa 'jipya' lakini bado ukatumia tu mbinu zile zile, lugha zile zile, na kashfa zile zile na bado ukaendelea tu kufanikiwa; laa hasa!! Pindi usikiapo kuna mabadiliko, kwa wale watu wadadisi wa mambo, ni sharti utafute kujua ya kwamba (1) ni kitu gani hasa kilichobadilika, (2) kivipi kimebadilika, (3) kwa sababu zipi, (4) na huko nyuma hali ilikuaje na sasa yakoje, (5) je mimi mwenyewe naendana na au siendani na mfumo huo mpya kwa kiasi gani hasa, (6) nifanye jitihada zipi (si kwenda Mlingotini) zinazokubalika ili niendane na mfumo mpya kwa namna ambavyo nitapata uhakika wa kung'ara KIUTENDAJI (si ki-ndumba) ndani na nje ya chama changu kusudi nisiwe mzigo wa chama na wapiga kura wala kulazimika kupanda BP kila wakati ...

  ... na maswali kama hayo yafanyiwekazi KIUHAKIKA NA UNYENYEKEVU zaidi wa kutafuta kule upya wa KUJIVUA GAMBA LA ZAMANI kwa wakati mwafaka na kujivisha GAMBA MPYA NA INAYOKUBALIANA NA MAZINGIRA YALIOPO na kwa mtindo utakaompendeza zaidi yule bosi na au mlaji wako wa mwisho ambaye ni MHESHIMIWA MPIGA KURA.

  Bila kufanya hivo basi niwaambieni HABARI MBAYA SANA kwamba kwa kipindi cha miaka michache ijayo, kwa tafsiri yangu ya mambo kitaaluma, bunge letu huenda ikabahatika kupata ugeni mkubwa wa Wabunge Vijana zaidi, Wasomi zaidi, na hata wakawashangaza zaidi wazee kwa kushinda kwao Uchaguzi kiurahisi zaidi bila hata kuhitaji utajiri mkubwa wa kuhonga mtu alimradi mtu huyu aje asome ninayoyaandika humu, akayafanyia HOMEWORK ya kufa mtu ndani ya miaka miwili mitatu hivi na kisha anapojitokeza ulingoni atakuta anazungumza lugha inayooana zaidi na mazingira yaliopo, akawa anazungumza na baadaye kushughulikia zaidi matatizo hasa yanaokubaliana fika na matarajio ya mabosi wake; waheshimiwa wapiga kura.

  Nirudie kwamba kwa sasa hivi ni rahisi mno kwa mtu anayejua dhana ya SIASA ZA USHINDANI unaotegemea nguvu za idadi na U-smart wa watu wanaojitokeza kugombea ukilinganisha na kuendana kwao na mahitaji halisi ya wakati uliopo wa mlaji wa mwisho wa HUDUMA ZA KIUONGOZI anazotarajia kutoa akishinda.

  Ndio nasema kwamba wapo wanasiasa wengi ambao bado huendesha mambo yao kisiasa lakini kwa kutumia fikra na mbinu za zamani katika kipindi ambacho ni tofauti kabisa. Huko nyuma siasa za fitina, majungu, kuunda zengwe, kupiga domo na kumwaga hewa tupu, kununua vyeo na wapiga kura, mtoto kurithiswa chama cha siasa cha kufuata, kurithishana uongozi na mambo kama hayo yote yalihesabiwa kuwa ndio ujanja zaidi mtu kuitwa mwanasiasa mahiri. Hii hali inaelezea hasa kwa nini Tanzania tumejitawala wenyewe karibia miaka 50 na mambo bado ni ki-mishen tauni tu toka ngazi ya kata hadi ofisi inayostahili heshima ya hali ya juu inayoitwa ikulu nchini. Ajabu kote huko kumebakia woga tu na wala si heshma kwao.

  Kwa wale ambao walau tumewahi japo hata kusikia kitu 'MFUMO WA SIASA ZA USHINDANI' napenda niseme kwamba hii ni sayari nyingine kabisa ambayo pale bungeni kwetu Dodoma, kama sikosei, zaidi ya ile dadi kubwa ya wabunge karibia 400 huenda chini ya asilimia 10% tu ndio wanaoifahamu kwamba ni kitu gani hasa hiki. Lakini kwa kuwa siku zote wanasiasa huhesabika kuwa ni watu mashuhuri kwa kujua kila kitu (MR / MS I-KNOW-ALLS) naona nafasi ni finyu sana kwa wale wengine zaidi ya 360 kuhiari walau kujishusha na kwenda kutafuta elimu juu ya hili ili uwepo wao bungeni uendelee kuwa na uhakika pamoja na tija kwa jamii kutokana na yeye mwenyewe na au chama chake kama kundi zima.

  Guys, an imagination of a possible political landscape without CUF around just but most ungratifying to witness.

  The case would never be the same as it would apply to TLPs, NCCR-Mageuzis and the UDPs of this World that has practically been consigned into political Limbo courtesy of the prominently trenched Self-Seeking behaviour, The Politics of Double-Tongue lashing and Own Course Self-Agrandisement by many in their ranks.

  Niliposema kwamba Juliasi yule wa DARUSO enzi zile wala si huyu hapa na kwamba kwa bahati mbaya mno akina Maalim Seif wamemfichia mi-faili nyeti zenye kuonyesha (1) sura halisi ya CUF, (2) Malengo ndani ya sera yao mpya ya 'Kujiunga Muafaka na Nguruwe Kuchakaza shamba Mabua yote' na hatima yake.

  Ndio, na wamemficha pia Juliasi faili iliobeba (3) tafsiri za wananchi Bara na Visiwani kama kweli walichokua wanakitafuta CUF ilikuani UTULIVU tu Zanzibar au AMANI KAMILI kwa kurejesha kwanza HAKI NA MASLAHI KWA UMMA wa nchi hii.

  Si utani na mikutano ya wenzetu inapoondoka Kidongo Chekundu pale kweupe Mnazi Mmoja hadi kule mitaa ya Mwisho wa Lami Gongolamboto, Mtoni kwa Azizi Ali Mara Manzese Kwa Bibi Mfuga Nyau ... kweli hii ni a Big Change in the Wrong Direction; yes it is a most demoralising experience and transition that bothe CUF are currently walking dow the political memory valleys kwa kupingana tu na Maslahi ya Wapigakura nchini.

  In fact, a more compelling question that analysts would soon surrender to evader no more is that 'of what use is an army commander if all foot soldiers are long-gone?' I just tend to hope that the NOW apparent CUF Career Presidential Candidates Hon Maalim Seif Sharrif Hamad (Visiwani) and Prof Ibrahim Haruna Lipumba will, at least, seek an escape to some remote hotels may be around Uluguru Mountains and conduct a most sincere Worst-Scenario Self-Evaluation.

  Yes, they would certainly need to do that long before they could similarly seek an independent expert hand to equally do the same to the very CUF as a party and ultimately hand down the CUF Secret Files stored far away in Chake Chake - Pemba to Juliasi Mtatiro and other remnant youths to help chat out a possible next course of action - either to Revive or Survive their own way and a lot sooner the better!!

  To this end, I just DON'T see myself leaving out CHADEMA for a more freequent (4-Month Periodical Independent & Credible) monitoring and evaluation about their yesterdays, todays and tomorrows. Waberoya, Mwanakijiji and myself can most competetly string them to this own-face behind the mirror scene for a more re-assuring future.

  And this is where all political parties, just like any other business establishment known around, are bound to most willingly go or never!! The market-based COMPETITIVE POLITICS that we tirelessly seek to live to-date (Democratic Multipartism) is just but more dynamic, most enveloping and so demand both at group and personal levels such that a POLITICAL HERO / HEROES of yesterday is NEVER guaranteed tomorrow unless they 24 / 7 choose to obay Philip Kotler's dictates to keep their eyes to the ground to catch the most correct scale of the electorates' next-day heartbeats and seek to serve them in the best way possible on TIME and in a WAY that a competitor (another political Party or an opponent within your party or across) would never far easily pick a match.

  In a nutshell, after luoghing of my friend Julious Mtatiro's most impending political misfortunes, like is lately the case with CCM, with his political party CUF that daily diminishing in value in the eyes of the HONOURABLE ELECTORATES, may I point here that the Political Landscape is fast-adjusting with youth on the steerwheels, things turning high-tech almost in a speed of a click of a computer mouse away such that the yerteryears inherently incompetence and majungu / fitina in political arena shall soon NEVER be tolerated BUT only practical positive results in public goods to the general public that shal be mattering and not even a mere name of a political party of the neighbours shall ever count.

  Wazee, huku ndiko tunakokwenda; hakuna watu kulala tena bungeni na kujigeuza wataalam wa kuzungusha maneno badala ya matunda kuonekana. Huko katika ulimwengu ulioendelea utasikia pengine chama chake Obama kimeshinda kwa wingi leo na keshokutwa kwenye Mid-term elections ukasikia wamepigwa chini zaidi ya nusu na Waheshimiwa Wapiga kura kwa kutoridhisha kiutendaji.

  Nasema na ieleweke kwamba ule utamaduni wa 'HIKI NI CHAMA CHANGU NA FAMILIA YETU NZIMA tangu enzi za babu hivyo sitoweza kukihama' itakuja kutoweka bila hata ya wengi wetu kujua. Hatutopigia kura tena (1) SURA za watu, (2) MAJINA YA VYAMA bali tu (3) kwa kiasi Gani Wametuletea sisi Wapiga Kura Matunda tuliokua tukiyatarajia.

  Hizo ndizo misingi halisi za siasa za ushindani huko tunakoelekea ambapo VIJANA WENGI NA WASOMI nchini ndio idadi yao inaendelea kuwa kubwa nchini. Hivyo kitendo cha Chama kubahatika kupewa ka-nafasi ya kuongoza na kisitumie vizuri KUJING'ARISHA mbele ya macho ya wapiga kura; badala yake kikajiroga kwenye kujiingiza kwenye Vitendo vya Kifisadi, basi siku kikipoteza nafasi hiyo ujue fika chama hicho kitatiwa LOCK-UP na wapiga kura kwa muda usiojulikana sawa yake KANU wa Kenya ambacho hivi leo kisiasa wala hakizungumzwi hata kwenye nafasi ya nne ki-umaarufu.

  Na atakayesoma maoni haya ampitishie na kiongozi wake wa chama chake, kata, wodi, jimbo na taifa ili tukija kuwatia LOCK-UP kwa uwezo wa kura zetu wasije wakasingizia hawakuelewa kama sheria za mchezo wa siasa za ushindani ni tofauti kiasi hicho.

  Mwisho nimalizie kwa kusema kwamba enyi mlioko madarakani ambao bado ndio mnaoonekana wakubwa kwa sisi Wapiga kura, malizieni salama utamu huo kwa vile wengi wetu hawajaeleweshwa; tangu hapo 2015 na kuendelea MPIGA KURA NDIYE ATAKAYEGEUKA MFALME kwa kipindi chote na wala si kwa wakati wa wiki 2 au 3 za uchaguzi tu.

  Chukua hatua ewe unayefikiria kuja kua kiongozi wa ngazi yoyote hapo baadaye kidogo ili usije ukafa bure na shinikizo la damu kwenye mfumo mpya wa siasa ndani ya mipaka yetu!!
   
 4. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwa Tanzania hii inalalamikiwa na chama tawala,wao ukweli ukielezwa kwa wananchi wanasema ni siasa za chuki,kwa Tanzania ya leo nawashauri watumie mbinu mpya za kujiweka zaidi karibu na wananchi kwa kusikiliza na kutatua shida zao,leo hii inanishangaza kuona wao ndio wanadai wanaonewa kitu ambacho si cha kweli,wanalumbana kila kukicha wenyewe kwa wenyewe,CDM ambao ndio wapinzani wakubwa wanazidi kujijenga na kukubalika kwa siasa zao safi na za uwazi.binafsi naona hakuna siasa za chuki bali ni kutapatapa kwa watawala baada ya kuona mambo yanazidi kwenda kombo.
   
 5. n

  ngoko JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Siasa za chuki ni zile zinazobeza wanasiasa wa upande mwingine . Kwa mujibu wa sisiemu , siasa za chuki ni siasa za CDM, upande mwingine hotuba zilizojaa vijembe za kufunga kampeni za sisiem Dar nazo pia zina qualify kuwa siasa za chuki. sasa kwa kulielewa hilo mwenyekiti wa sisemu kama mdau wa siasa hizo alisema wazi kuwa kampeni zimeacha majeraha ambayo yanahitaji kupata dawa ... HOW ? sijui
   
Loading...